Mambo Hatarishi Yanayohusiana na Saratani?

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Jambo hatarishi ni jambo linalokuweka katika uwezekano (hatari) zaidi wa kupata ugonjwa fulani.

  • Ikiwa una jambo hatarishi kwa saratani, inamaanisha kuwa una uwezekano zaidi kupata saratani kuliko mtu wa wastani

  • Hata hivyo, kuwa na jambo hatarishi hakumaanishi kuwa utapata saratani

Mambo hatarishi yanayohusiana na saratani ni pamoja na?

  • Kuwa na jeni fulani (sifa unazorithi kutoka kwa babu/bibi na wazazi wako)

  • Kuwa karibu na kemikali fulani kazini au kwenye mazingira

  • Kula au kunywa vitu fulani

  • Kuathiriwa na miali hatarishi

  • Kuwa na maambukizi ya aina fulani

Kasinojeni ni vitu ambavyo wakati mwingine husababisha kansa. Kwa kawaida, uko hatarini zaidi ya kuugua saratani ikiwa umeathiriwa na kiasi kikubwa cha kasinojeni au umeathiriwa kwa muda mrefu.

Ni zipi sifa hatarishi za kijeni zinazohusiana na kansa?

Kila seli ya mwili wako ina jeni. Jeni ni maagizo yanayoelekeza kila seli ya mwili wako jinsi ya kufanya. Jeni huambia seli wakati wa kukua, wakati wa kuacha kukua, na vitu zinavyopaswa kutengeneza.

Wakati mwingine jeni zako zinaweza kufanya seli iwe na saratani ikiwa:

  • Jeni hiyo iliharibiwa na kitu kilichokuathiri (kitu kilicho kwenye mazingira)

  • Jeni hiyo ilinakiliwa visivyo wakati wa ukuaji wa kawaida wa seli

Kwa nadra, unaweza kuwa ulirithi jeni ya kansa kutoka kwa mmoja wa wazazi wako. Wakati mwingine watu wa familia moja wanaweza kuwa na uwezekano zaidi wa kuugua saratani ya aina fulani. Huenda jeni inayosababisha kansa inapatikana katika familia hiyo. Jeni moja inayosababisha ugonjwa wa saratani iitwayo BRCA huongeza hatari ya kuugua saratani ya matiti.

Ni mambo gani hatarishi ya kimazingira yanayohusiana na kansa?

Kuwa karibu na vitu fulani kunaweza kuongeza uwezekano wako wa kuugua saratani ikiwa ni pamoja na:

  • Moshi wa tumbaku: Saratani ya mapafu, mdomo, koo, umio, figo, na kibofu cha mkojo

  • Asbesto (nyuzi za madini zinazotumiwa kuhami majengo ili yahifadhi joto na vitu vingine vya kujengea): Saratani ya mapafu na mesothelioma (saratani kwenye tishu zinazotengeneza utando wa mapafu)

  • Miale ya jua: Saratani ya ngozi

  • Eksirei: Lukemia na saratani kwenye ogani iliyoathiriwa na miali hatari

  • Radoni (gesi yenye miale nunurishi inayotoka ardhini na inaweza kufikia viwango hatari katika sehemu za nyumba zilizojengwa chini ya ardhi): Saratani ya mapafu

Baadhi ya kemikali zinazotumika kazini (kama vile benzini, kromati, nikeli, dawa fulani za kuua wadudu na kloraidi ya vinyl) zinaweza kusababisha saratani.

Jiografia (mahali unapoishi) inaweza kuathiri uwezekano wako wa kuugua saratani. Sababu moja ni kuwa watu katika maeneo tofauti wanaweza kuathiriwa na viwango tofauti vya kasinojeni. Sababu nyingine ni kuwa watu katika maeneo tofauti wanaweza kuwa na sifa tofauti hatarishi za kijeni.

Je, ni mambo gani mengine hatarishi yanayohusiana na saratani?

Umri wako:

  • Zaidi ya nusu ya magonjwa yote ya saratani hutokea kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65 pengine kwa sababu watu wazee wameathiriwa na kasinojeni (vitu vinavyosababisha kansa) kwa muda mrefu zaidi.

Mlo:

Kuwa na uzani kupita kiasi kunaweza kuongeza hatari ya kuugua saratani ya matiti, uterasi, utumbo mpana, figo, na umio.

Dawa fulani:

  • Istrojeni na diethylstilbestrol (DES): Saratani ya matiti

  • Baadhi ya dawa za kutibu saratani huongeza hatari ya kupata aina nyingine ya saratani baadaye

Kuathiriwa na miali hatari, iwe ni kimakusudi kwa madhumuni ya matibabu au kwa bahati mbaya:

  • Kutoka kwenye vipimo vya kimatibabu (eksirei, uchanganuzi wa CT) au tiba ya mionzi

  • Kuathiriwa kibahati mbaya na vitu yenye miali nunurishi au miali ya kinyuklia kutokana na ajali ya mtambo wa nishati

Maambukizi ya virusi na bakteria fulani:

Matatizo yanayosababisha kuvimba (uvimbe wa muda mrefu wa ogani fulani) unaweza kuongeza hatari ya kuugua saratani: