Saratani ya tumbo ni nini?
Saratani ni ukuaji wa seli mwilini kwa namna isiyoweza kudhibitiwa. Seli ni elementi ndogo zinazoshikamana kuunda viungo vya mwili wako. Seli zina majukumu maalum. Viungo tofauti vimeundwa na aina tofauti za seli. Aina yoyote ya seli inaweza kuwa yenye saratani.
Saratani ya tumbo ni saratani ambayo huanzia tumboni mwako.
Dalili za saratani ya tumbo ni pamoja na tumbo kutokutulia, kupoteza uzani na udhaifu
Saratani ya tumbo husambaa kirahisi kwenye viungo vingine vya mwili wako na mara nyingi ni hatari sana
Daktari ataitibu kwa upasuaji
Je, nini husababisha saratani ya tumbo?
Husababishwa na:
Maambukizi ya bakteria anayeitwa H. pylori kwenye tumbo lako
Jenetiki (kitu unachorithi kutoka kwa mzazi mmoja au wote wawili)
Dalili za saratani ya tumbo ni zipi?
Dalili za mwanzo sio kali na huenda usizigundue. Zinajumuisha:
Maumivu ya tumbo kuwaka moto
Kushiba baada ya kula mlo mdogo
Dalili za baadaye zinaweza kujumuisha:
Kupungua uzani na udhaifu
Anemia (idadi ndogo ya seli nyekundu za damu)
Wepesi wa kichwa
Kutapika damu au kutoa kinyesi chenye weusi wa kahawia
Saratani inayosambaa inaweza kusababisha dalili kama vile:
Homa ya nyongo ya manjano (ngozi na weupe wa macho kuwa manjano)
Kukusanyika kwa majimaji na tumbo lako kuvimba
Mifupa dhaifu, hivyo kusababisha mifupa kuvunjika
Madaktari wanawezaje kujua kama nina saratani ya tumbo?
Madaktari hukagua uwepo wa saratani ya tumbo kwa:
Endoskopia (bomba la kutazama linalopinda hupitishwa kwenye koo lako ili kutazama ndani ya tumbo lako na kuchukua sampuli kwa ajili ya vipimo)
Ikiwa vipimo vya endoskopia na uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi vitaonyesha saratani ya tumbo, mara nyingi madaktari watafanya:
Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) na kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa kifumbatio ili kukagua kama imesambaa katika viungo vingine
Vipimo vya damu
Je, madaktari wanatibu vipi saratani ya tumbo?
Madaktari hutibu saratani ya tumbo ambayo haijasambaa kwa:
Upasuaji
Kuondoa uvimbe wote kabla ya kusambaa ndiyo nafasi pekee ya kupona. Kwa saratani ya tumbo ambayo imesambaa, matibabu hayawezi kuponya ugonjwa huo. Madaktari wanaweza kutibu dalili na kumfanya mtu apate afadhali kwa:
Upasuaji