Tiba ya Mionzi ya Saratani

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2023

Tiba ya mionzi ni nini?

Tiba ya mionzi ni matibabu ya saratani yanayotumia mionzi ya ununurishi ili kuharibu seli za saratani na kupunguza uvimbe wa saratani.

  • Madaktari hutumia mionzi kutibu aina nyingi za saratani, ikiwa ni pamoja na saratani ya kichwa, shingo, ubongo, na matiti

  • Huenda tiba ya mionzi isiharibu seli zote za saratani na inaweza kuharibu seli za kawaida, hali inayoweza kusababisha madhara

  • Madaktari wanaweza kutibu kansa yako kwa kutumia mionzi na aina nyingine ya matibabu ya saratani, kama vile tibakemikali

  • Tiba ya mionzi inaweza kuongeza uwezekano wako wa kupata kansa za aina nyingine katika siku za usoni

Tiba ya mionzi huua aina zote za seli mwilini mwako, si seli za saratani pekee. Mionzi ni lazima ilenge kwa umakini ili ifikie seli za kansa haswa wala si tishu ambazo hazijaathiriwa.

Aina za tiba ya mionzi

Aina nyingi za tiba ya mionzi hutumia mashine inayotuma mwonzi wa mnunurisho kwenye sehemu ya mwili iliyo na kansa. Kuna aina mbili za mionzi ya mnunurisho?

  • Miale ya gamma

  • Mionzi ya protoni

Mionzi ya protoni inaweza kulenga sehemu mahususi zaidi kuliko miale ya gamma. Kwenye mionzi yoyote ile, watu wengi hupata tiba ya mionzi kila siku kwa wiki 6 hadi 8.

Njia nyingine wanayotumia madaktari ili kuepuka kudhuru tishu zingine ni kuelekeza mwonzi kwenye kansa yako kutoka pande tofauti za mwili wako na katika pembe tofauti. Kwa kufanya hivyo, mwonzi hugusa kansa kila wakati, lakini tishu ambayo haijaathiriwa haiguswi kila mara.

Aina nyinginezo za tiba ya mionzi ni pamoja na:

  • Dutu ya mnunurisho ambayo madaktari hudunga kwenye mshipa wako inayosafirishwa na damu yako hadi kwenye seli za saratani

  • Chembe ndogo za mnunurisho (mbegu) ambazo madaktari huweka kwenye uvimbe wa saratani

Ni zipi athari mbaya za tiba ya mionzi?

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Vidonda vya mdomo

  • Matatizo ya ngozi, kama vile kuwa nyekundu, kuwashwa na kuchunuka

  • Maumivu unapomeza

  • Kuvimba kwenye mapafu yako

  • Kuhisi mgonjwa kwenye tumbo lako au kutapika

  • Kuhisi kama unahitaji kukojoa (kwenda haja ndogo) zaidi kuliko kawaida au maumivu wakati wa kukojoa

  • Kuvimba kwa urahisi

Tiba ya mionzi inaweza kuharibu tishu za kawaida na kufanya uwe na uwezekano mkubwa zaidi wa kuugua kansa za aina nyingine katika siku za usoni. Hatari zinategemea umri wako na sehemu ya mwili wako inayopata tiba ya mionzi.