Nini maana ya tiba mseto ya saratani?
Tiba mseto ya saratani ni wakati madaktari wanatibu kansa yako kwa kutumia zaidi ya aina moja ya matibabu. Mkusanyiko huo unaweza kuwa mseto wa upasuaji, tiba ya mionzi (hutumia kiwango cha juu cha mionzi kupunguza uvimbe wa saratani na kuharibu seli za saratani), na tibakemikali (dawa za kuharibu seli za kansa).
Madaktari wanaweza kukupa aina kadhaa za tibakemikali kwa wakati mmoja (tibakemikali mseto)—kila dawa hufanya kazi kivyake kuharibu seli zako za saratani, kwa hivyo dawa hizo huharibu seli nyingi zaidi za kansa kwa pamoja
Madaktari wanaweza pia kutibu saratani yako kwa kutumia aina kadhaa za matibabu—kwa mfano, tibakemikali na upasuaji kwa pamoja
Madaktari huamua iwapo wangependa kutumia tiba moja au tiba mseto kulingana na hatua na aina ya saratani unayougua
Kwa nini madaktari hutumia tiba mseto ya saratani?
Baadhi ya kansa haziwezi kutibiwa kwa kutumia upasuaji au tiba ya mionzi pekee
Upasuaji au tiba ya mionzi inaweza kutibu uvimbe ulio sehemu moja ya mwili wako, ilhali tibakemikali hutibu seli za saratani zilizoenea kwenye sehemu nyinginezo za mwili
Tiba ya mionzi au tibakemikali inaweza kupunguza uvimbe wako kabla ya upasuaji, ili sehemu ndogo tu ikatwe
Baada ya upasuaji, tiba ya mionzi na tibakemikali inaweza pia kusaidia kuharibu seli za saratani ambazo mpasuaji hangeweza kuondoa
Tibakemikali mseto inaweza kusaidia kurefusha maisha yako na kupunguza dalili