Upasuaji wa Saratani

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2023

Madaktari hutumia upasuaji kutibu kansa wakati gani?

Upasuaji wa saratani ni wakati madaktri wanafanya upasuaji ili kuondoa uvimbe wenye kansa. Kwa kawaida, madaktari hufanya upasuaji wakati tu:

  • Kansa haijasambaa (haijaenea) mahali pengine

  • Mwili wako una nguvu za kutosha kufanyiwa upasuaji

Ikiwa kansa yako haijaenea mwilini, upasuaji unaweza kukuponya. Lakini kansa ikishaenea, kukata sehemu ambapo kansa ilianza hakutakuponya. Kansa iliyosalia itaendelea kukua na kuenea. Daktari wako atafanya vipimo kabla ya upasuaji ili kubaini iwapo kansa imeenea. Huenda ukafanyiwa uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta), MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku), au vipimo vingine.

Hata hivyo, vipimo hivyo vinaweza kupata chembechembe ndogo sana za kansa. Kwa hivyo, wakati wa upasuaji, daktari wako huondoa tezi limfu zilizo karibu na uvimbe. Tezi limfu ni ogani ndogo zenye umbo la haragwe ambazo ni sehemu ya mfumo wa kinga wa mwili wako. Kansa mara nyingi huenea kwenye tezi limfu hizi zilizo karibu. Maabara yatapima tezi limfu ili kuona iwapo kansa imeanza kuenea.

  • Kuondoa tezi limfu zilizo na kansa (tezi limfu "zilizopatikana kuwa zimeathiriwa") hakusaidii kukuponya

  • Ikiwa kansa imepatikana kwenye tezi limfu zilizoondolewa na daktari wako, takribani kila wakati kansa hiyo huwa imeenea kwenye sehemu zingine pia

Ikiwa daktari wako anajua kuwa tezi limfu zako zina kansa, basi unaweza kupata matibabu mengine kama vile tibakemikali au tiba ya mionzi.

Ikiwa nimefanyiwa upasuaji, je, nitahitaji matibabu mengine?

Baada ya uvimbe wako kuondolewa, huenda ukafanyiwa upasuaji zaidi. Kwa mfano, baada ya upasuaji wa matiti (kuondolewa titi) ili kutibu saratani ya matiti, huenda ukafanyiwa upasuaji ili kureshesha umbo na mwonekano wa titi lako, mchakato uitwao urejeshaji.

Kwa kutegemea aina ya saratani unayougua, huenda daktari wako pia akakupa:

Huenda ukapata matibabu haya kabla au baada ya upasuaji wako.