Maarifa ya Matibabu ya Kimataifa
Maudhui yalibadilishwa mwisho Apr 2024
Wito wetu ni rahisi: Miongozo, iliyochapishwa mara ya kwanza kama Mwongozo wa MSD mnamo 1899, inayojulikana sasa kama Miongozo ya MSD nje ya Marekani na Kanada ni miongoni mwa vyanzo vinavyotumika zaidi vya taarifa za matibabu. Miongozo imejitolea kufanya taarifa bora zaidi za sasa za matibabu kupatikana kwa hadi wataalamu na wagonjwa bilioni 3 katika kila bara.
Tunaamini kwamba taarifa za afya ni haki ya wote na kwamba kila mtu ana haki ya kupata taarifa sahihi na zinazoweza kufikiwa za matibabu. Tuna wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kushiriki taarifa bora zaidi za sasa za matibabu ili kuwezesha kufanya maamuzi ambapo wahusika wana uelewa zaidi, kuimarisha mahusiano kati ya wagonjwa na wataalamu na kuboresha matokeo ya huduma za afya duniani kote.
Maarifa ya matibabu ni nguvu. Wajulishe wengine.
KWA HESABU
Pata maelezo zaidi kuhusu athari ya wito wetu:







Siku ya Utambuzi wa Maarifa ya Matibabu ya Kimataifa
Siku ya Utambuzi wa Maarifa ya Matibabu ya Kimataifa hufanyika kila mwaka tarehe 15 Oktoba na hutoa wito kwa wataalamu wote wa huduma za afya, wanafunzi wa tiba na watumiaji kuadhimisha na kukuza uwezo wa taarifa za afya zinazoweza kutekelezeka. Tulianza kuadhimisha siku hii kila mwaka baada ya kufikia lengo letu la kufanya Mwongozo wa MSD kupatikana kwa wataalamu na wagonjwa bilioni 3 katika kila bara mnamo Oktoba 2020. Hivi ndivyo unavyoweza kujihusisha:
• Pata Ustadi Kuhusu Afya Yako: Imarisha maarifa yako ya afya kwa kujifunza kuhusu uhusiano kati ya maarifa bora ya matibabu na matokeo bora ya afya. Jitolee kusoma makala moja ya afya kwa wiki na kushiriki katika kujifunza wakati wote kuhusu maarifa ya matibabu.
• Hakikisha Vyanzo vyako vya Afya Vinaaminika: Jifunze kinachotofautisha taarifa bora za afya na jinsi ya kuhakiki vyanzo vya kimatibabu vya mtandaoni. Alamisha tovuti kama vile Miongozo ya MSD na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Centers for Disease Control and Prevention). Zungumza na mtoa huduma wako wa afya kuhusu jinsi ya kupata habari kuhusu afya yako mwenyewe.
• Endelea Kushiriki Maarifa Sahihi na ya Sasa ya Matibabu: Onyesha kujitolea kwako kwa kuongeza beji ya Maarifa ya Matibabu ya Kimataifa kwenye wasifu wako wa mitandao ya jamii na kuzungumza na familia na marafiki kuhusu umuhimu wa maarifa sahihi ya matibabu.
Kwa hatua hizi, watu wanahimizwa kuchukua hatua mahususi, ikiwemo kuongeza Beji ya Maarifa ya Matibabu ya Kimataifa kwenye wasifu wao wa mitandao ya jamii, kualamisha MSDManuals.com na kufanya mazungumzo na marafiki na wanafamilia kuhusu umuhimu wa taarifa za sasa za kuaminika za matibabu.