Programu za Vifaa vya Mkononi

Maudhui yalibadilishwa mwisho Aug 2023

Tunajivunia kufanya Miongozo ipatikane bila malipo kwa njia ya kidijitali kwa wataalamu na wagonjwa kote duniani. Hakuna uandikishaji au usajili unaohitajika.


Kila programu ya vifaa vya mkononi ya Miongozo iliundwa kwa ajili ya hadhira mahususi: Watoa huduma wa matibabu, wataalamu wa tiba ya mifugo, wanafunzi, wagonjwa, watunzaji na familia.

 

 



Nembo ya Programu ya Kitaalamu

Ya Kitaaluma

Kwa wataalamu na wanafunzi wa tiba


Programu hii muhimu ya marejeleo ya tiba huangazia etiolojia, patholojia na fiziolojia, na machaguo ya tathmini na matibabu ndani ya nyanja zote kuu za tiba na upasuaji. Mada huandikwa na kusasishwa mara kwa mara na zaidi ya madaktari 350 wa kitaaluma.  Vipengele vya ziada ni pamoja na:


  • Picha na vielelezo
  • Video fupi za mafundisho
  • Tahariri* zinazoandikwa na wataalamu bora wa tiba
  • Maswali*
  • Taarifa za marejeleo ya dawa* (Kiingereza pekee)
  • Uigaji wa hali halisi* (Kiingereza pekee)
  • Habari na maoni ya tiba* 



Nembo ya Mwongozo wa Programu ya MSD

Mwongozo wa MSD wa Tiba ya Uzazi

Kwa wataalamu wa huduma za afya wanaohudumia wagonjwa wa uzazi


Mwongozo wa MSD wa Tiba ya Uzazi sasa unapatikana ndani ya Marekani na Kanada na ni seti ndogo ya Mwongozo wa Kitaalamu wa MSD. Unajumuisha mada 99 zinazoeleweka wazi na fupi, na video 14 zinazoangazia:


  • Ujauzito wa kawaida na huduma za kabla ya kujifungua
  • Tathmini na udhibiti wa dalili na matatizo ya ujauzito
  • Ujauzito wenye hatari kubwa
  • Leba ya kawaida na tata na kujifungua
  • Huduma na matatizo ya baada ya kujifungua
  • Utunzaji wa awali wa mtoto mchanga, ikiwemo kuamsha fahamu kwa mtoto mchanga
  • Kupanga uzazi na ushauri wa kijenetiki kabla ya kujifungua

Lugha Zinazopatikana




Nembo ya Programu ya Mtumiaji

Mtumiaji

Kwa wagonjwa, wazazi na watunzaji


Programu ya matibabu inayoaminika ya Mtumiaji ya Mwongozo wa MSD kwa ajili ya marejeleo ya nyumbani ina maelezo wazi na rahisi kuelewa kwa maelfu ya matatizo ya afya, ikiwa ni pamoja na dalili na kile ambacho madaktari hufanya ili kutambua na kutibu magonjwa. Inajumuisha:


  • Picha, vielelezo na video kuhusu maelfu ya matatizo ya afya na magonjwa
  • Uhuishaji unaoonyesha magonjwa na matibabu kwa michoro
  • Maswali shirikishi* ili kupima maarifa kuhusu mada za afya
  • Mwongozo wa taarifa za dawa na tiba* unaojumuisha Maingiliano ya dawa, Kitambulishi cha vidonge na dawa, na dawa zinazouzwa dukani bila agizo la daktari (Kiingereza pekee)
  • Tathmini za binafsi* ili kuangalia viwango vyako vya afya na siha



Nembo ya Programu ya Tiba ya Mifungo

Tiba ya Mifungo

Kwa matabibu wa mifugo, wanafunzi na wataalamu wengine wa afya ya wanyama


Programu ya marejeleo ya tiba ya mifugo inayotumika zaidi duniani inajumuisha maelfu ya mada zinazoandikwa na kusasishwa na zaidi ya wataalamu 400 wa tiba ya mifugo kutoka zaidi ya nchi 20. Inatoa ufafanuzi wazi na wa lugha ya kawaida wa maelfu ya maradhi ya mifumo yote ya mwili na inaangazia etiolojia, patholojia na fiziolojia na machaguo ya utambuzi magonjwa na matibabu. Vipengele vya ziada ni pamoja na:


  • Maktaba ya kina ya picha na video
  • Maswali*
  • Uigaji halisi wa hali*
  • Ukokotoaji wa data ya tiba,
  • Miongozo ya marejeleo na mamia ya majedwali muhimu
  • Maudhui ya afya ya wanyama vipenzi*

Lugha Zinazopatikana


*Ufikiaji wa mtandao unahitajika