Vinundu vya Limfu Vilivyovimba

(Tezi zilizovimba; Kuvimba kwa Kifundo cha Limfu)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Hali ya tezi/vinundu vya limfu vilivyovimba ni nini?

Tezi za limfu ni sehemu ya mfumo wako wa limfu, ambao husaidia kupambana na maambukizi na saratani. Tezi za limfu ni sehemu za mkusanyiko zenye ukubwa wa njegere ambazo huchuja vijidudu na seli kutoka kwenye majimaji ya limfu. Tezi za limfu zimesambaa kila sehemu kwenye mwili wako, lakini nyingi zimejikusanya kwenye shingo lako, chini ya mikono yako, na kwenye kinena chako. Huvimba pale mwili wako unapopata maambukizi au saratani.

  • Sababu ya kuvimba mara nyingi ni maambukizi ya ngozi au tishu iliyo karibu au virusi visivyo hatarishi ambavyo hupotea vyenyewe

  • Wakati mwingine sababu huwa ni maambukizi makali au saratani

  • Tezi/vinundu vya limfu vilivyovimba vinaweza kuuma, au vinaweza visiume

  • Wakati mwingine daktari wako anaweza kufanya vipimo vya baadhi ya maambukizi au saratani

  • Iwapo uvimbe kwenye tezi za limfu zako haupotea ndani ya wiki 3 au 4, madaktari wanaweza kuondoa kipande cha tishu kwa uchunguzi (kuondoa sehemu ya tishu ili kuichunguza kwenye hadubini)

Watu huviita vinundu vya limfu vilivyovimba "tezi zilizovimba" ila tezi za limfu kiuhalisia si tezi.

Je, nini husababisha tezi/kinundu cha limfu kuvimba?

Kuna sababu nyingi za tezi/vinundu vya limfu kuvimba. Sababu za kawaida ni pamoja na:

  • Maambukizi kwenye tishu zilizo karibu na vinundu vya limfu vilivyovimba

  • Maambukizi ya mwili wote

Kwa mfano, koo lililovimba au mafua yanaweza kufanya tezi za limfu kwenye shingo lako zivimbe. Au maambukizi ya zinaa (STI) yanaweza kufanya tezi za limfu kwenye kinena chako zivimbe.

Maambukizi ya mwili wote kama vile mononukleosisi, maambukizi ya VVU au kifua kikuu yanaweza kufanya tezi za limfu kwenye mwili wako wote zivimbe.

Sababu hatarishi zaidi zinazo sababisha tezi za limfu kuvimba ni:

Kwa kawaida, ulinzi wako wa kingamwili huua vijidudu vyovyote vilivyo hai ambavyo huingia kwenye tezi za limfu. Lakini wakati mwingine, baadhi ya vijidudu huendelea kuishi na kusababisha maambukizi. Tezi ya limfu yenye maambukizi inauma, na ngozi iliyo juu yake hubadilika rangi na kuwa nyekundu.

Mara nyingi seli za saratani hujiondoa kwenye saratani na kusafiri kupitia mishipa ya limfu hadi kwenye tezi za limfu zilizo karibu. Kwa mfano, saratani ya matiti mara nyingi husambaa kwenye tezi za limfu kwenye kwapa lililopo upande ambao una saratani. Wakati mwingine ulinzi wako wa kingamwili huua seli za saratani. Lakini wakati mwingine seli za saratani huota kwenye tezi zako za limfu. Saratani hufanya tezi za limfu kuwa ngumu na kugandana.

Hata hivyo, yumkini ni chini ya asilimia 1 ya watu wenye tezi/vinundu vya limfu vilivyovimba huwa na saratani.

Je, napaswa kumwona daktari lini?

Si kila mtu mwenye tezi/vinundu vya limfu vilivyovimba anahitaji kuonana na daktari mara moja.

Onana na daktari wako mara moja ikiwa tezi yako ya limfu:

  • Chungu sana 

  • Inatiririka usaha (majimaji mazito, meupe au ya njano)

Mpigie simu daktari wako ikiwa una mojawapo ya dalili hizi za onyo za ziada:

  • Tezi ya limfu ambayo ni kubwa sana (inch moja au zaidi kutoka upande mmoja hadi mwingine katikati)

  • Tezi ya limfu ambayo ni ngumu, kama jiwe

  • Sababu hatarishi za maambukizi ya VVU (kama vile kuchomwa na sindano ambayo imetumiwa na mtu mwingine au kufanya shughuli za ngono zenye hatari kubwa)

  • Sababu hatarishi za kifua kikuu (kama vile kuishi au kufanya kazi na mtu ambaye ana kifua kikuu au umehama siku za karibuni kutoka katika eneo ambalo lina maambukizi makubwa ya kifua kikuu)

  • Homa

  • Kupungua uzani pasipo sababu

Daktari ataamua uharaka wa kukuona kutegemea na ishara za onyo au dalili nyingine. 

Ikiwa huna ishara za onyo na unajihisi vizuri, unaweza kusubiri kwa wiki moja ili uone kama tezi itarudi kuwa kawaida kabla ya kumpigia simu daktari.

Je, nitarajie nini nikienda kumwona daktari?

Daktari wako atakuuliza maswali kuhusu dalili na ishara za onyo ulizonazo na kukuchunguza. Kama kiuhalisia una tatizo ambalo si hatarishi, madaktari watasubiri na kuona kama uvimbe wa tezi limfu utapotea. Vinginevyo, madaktari watafanya vipimo kwa kutegemea na kile ambacho wanafikiri kimesababisha tezi zako za limfu kuvimba. Vipimo vinaweza kujumuisha:

Je, madaktari hutibu vipi tezi/vinundu vya limfu vilivyovimba?

Madaktari hutibu chanzo cha kuvimba kwa tezi/vinundu vya limfu.