Mononukleosisi ya Kuambukizwa (mono)

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Je, nini husababisha mononukleosisi?

Maambukizi ya mononukleosisi, mara nyingi huitwa mono, ni maambukizi ya virusi ambavyo huwapata sana watoto na vijana.

  • Mono husambazwa kwa mgusano wa karibu, kama vile kuwabusu watu wenye maambukizi

  • Dalili zake ni pamoja na koo lenye vidonda, kuchoka kupita kiasi na kuvimba vinundu vya limfu kwenye shingo lako

  • Watu wenye mono mara nyingi hupata nafuu baada ya takribani wiki 2, lakini watu wengine wanaweza kuhisi uchovu kwa wiki kadhaa au hata miezi

  • Acetaminophen or ibuprofeni hushusha homa na kupunguza maumivu

Je, nini husababisha mono?

Mono husababishwa na virusi vya Epstein-Barr, aina ya kirusi cha herpesi. Maambukizi ya virusi vya Epstein-Barr (EBV) ni ya kawaida, lakini si kila anayepata maambukizi hayo hupata mono. Watu wengi wenye maambukizi ya EBV huwa hawana dalili au wanakuwa na dalili za kawaida sana.

Je, dalili za mono ni zipi?

Dalili za mono ni pamoja na:

  • Uchovu kupita kiasi—hali hii huwa mbaya sana wakati wa wiki ya 2 hadi 3

  • Homa, hadi 103° F (39.4° C)

  • Koo lenye vidonda vingi—kunaweza kuwa na usaha katika sehemu ya nyuma ya koo lako

  • Vinundu vya limfu vilivyovimba, hasa kwenye shingo lako (vifundo vya limfu ni sehemu ndogo zenye umbo la haragwe za mfumo wako wa kingamwili ambazo husaidia kupambana na maambukizi)

Unaweza kupata mono pasipo kupata dalili hizi zote.

Takribani nusu ya watu wenye mono huwa na bandama zilizovimba. Bandama yako ni ogani iliyopo upande wa kulia wa tumbo lako chini tu ya kizimba cha ubavu wako. Ina takribani ya ukubwa wa ngumi. Bandama hutengeneza seli za damu ambazo husaidia mfumo wako wa kingamwili na kuondoa seli za damu ambazo zimezeeka au zenye kasoro. Bandama ina uwezekano mkubwa wa kupasuka ikiwa tumbo lako litajeruhiwa wakati bandama yako ikiwa imevimba.

Ikiwa mono ni kali sana, inaweza kusababisha kiwango cha chini cha damu na matatizo ya ini lako, na neva.

Je, madaktari wanawezaje kufahamu ikiwa nina mono?

Madaktari wanaweza kushuku kuwa una mono kutokana na dalili zako, hasa ikiwa una vinundu vya limfu vilivyovimba kwenye shiko lako. Ili kuthibitisha, watafanya vipimo vya damu.

Je, madaktari hutibu vipi mono?

Hakuna dawa za kuponya mono. Dawa za kuzuia maambukizi ya virusi hazisaidii. Madaktari watafanya:

  • Watakwambia upumzike kwa wiki moja au mbili, pale unapokuwa unajihisi kuchoka sana na dhaifu

  • Watakufanya utumie acetaminophen or ibuprofeni ili kusaidia kupunguza homa na maumivu

  • Watakufanya utumia kotikosteroidi, iwapo vifundo vyako vimevimba sana na vina maumivu makali kiasi kwamba unapata shida ya kumeza na kupumua

Baada ya wiki 2, unapoanza kupata nafuu, unaweza kuanza kujishughulisha zaidi—lakini usibebe kitu chochte kizito au kucheza michezo ya kugusana (kama mpira wa miguu) hadi daktari wako atakapokwambia kwamba bandama yako imerudi katika ukubwa wake wa kawaida.