Virusi ni kiumbe hai.kidogo. Viumbe wengine wa kawaida madogo zaidi wanajumuisha bakteria. Virusi ni vidogo sana kuliko bakteria na vinaweza kuonekana tu kwa hadubini zenye nguvu zaidi.
Tofauti na bakteria, virusi haviwezi kuzaana. Kwa hivyo virusi huingia kwenye mwili wako, vinachukua seli fulani na kutumia maumbo kwenye seli hizo kutengeneza nakala zaidi za virusi. Kawaida, hii huharibu na kisha kuua seli. Hata hivyo, virusi vingine vinaweza kukaa kwenye seli kwa muda mrefu bila kuua seli hizo.
Kuna virusi vya aina nyingi sana. Baadhi ya virusi huambukiza watu. Vingine huambukiza wanyama pekee. Ni aina chache tu ya virusi vinavyoweza kuambukiza watu na wanyama.
Maambukizi ya virusi ni nini?
Maambukizi ya virusi ni ugonjwa unaosababishwa na virusi.
Virusi vinaweza kuingia kwenye mwili wako kupitia kupumua hewa (kwa mfano, virusi ambavyo vinasababisha COVID-19), kushiriki katika ngono, kugusa kitu kilicho na virusi au kuumwa na mdudu kama vile mbu au kupe
Kwa kawaida virusi vinaambukiza aina moja ya seli peklee—kwa mfano, virusi ambavyo vinasababisha mafua vinaambukiza seli zilizo kwenye mapua, mdomo na koo pekee
Unapopata kirusi, seli zako nyeupe za damu zinakivamia—seli hizi zinakumbuka pia jinsi ya kupigana navyo ikiwa kirusi sawa kinaingia mwilini mwako tena.
Virusi vingi vinakufanya mgonjwa muda mfupi baada ya kuvipata na kisha huisha
Virusi vingine havitaisha na vinaweza kukufanya uwe mgonjwa kwa muda mrefu baada ya kuvipata (kwa mfano, virusi vya VVU na herpesi)
Dawa za kuua bakteria, ambazo zinatibu maambukizi ya bakteria, haziwezi kutibu maambukizi ya virusi
Baadhi ya virusi hubadilisha jinsi seli zako zinavyofanya kazi, na hali hii inaweza kusababisha saratani. Kwa mfano, virusi vya homa ya ini ya B na C vinaweza kusababisha saratani ya ini. HPV (virusi vya papilloma vya binadamu) inaweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi.
Madaktari wanawezaje kujua kama nina maambukizi ya virusi?
Kulingana na dalili zako, daktari anaweza kutambua ikiwa una maambukizi fulani ya kawaida ya virusi. Huenda pia:
Vipimo vya damu
Culture (wakati madaktari wanachukua sampuli kutoka mwilini mwako na kujaribu kukuza vijidudu kutoka kwake kwenye maabara)
Madaktari wanatibu aje maambukizi ya virusi?
Kwa kawaida madaktari hawawezi kufanya zaidi kutibu virusi vingi. Kwa sana watapendekeza matibabu ili kutibu dalili zako na kukusaidia kuhisi vizuri. Kwa mfano, ikiwa una mapua yaliyofungana, madaktari wanaweza kukwambia utumie vitu vya kukwamua.
Kwa baadhi ya virusi, madaktari wanaweza kukupatia dawa ya kuua virusi. Dawa za kuua virusi zinatumiwa kwa virusi chache pekee, ikijumuisha:
Mafua (homa ya mafua)
Dawa za kuua bakteria ni dawa ambazo zinaua bakteria. Dawa za kuua bakteria haziui virusi.
Ninawezaje kuzuia maambukizi ya virusi?
Tunza afya yako—kwa mfano, osha mikono yako mara nyingi kwa kutumia sabuni na maji na ushiriki ngono kwa njia salama.
Pata chanjo inayopendekezwa
Chanjo ni sindano ambazo zinafunza mfumo wako wa kingamwili jinsi ya kupigana na maambukizi fulani. Kwa kawaida unapata chanjo kabla ya kupata maambukizi.
Lakini kwa baadhi ya virusi, unaweza kudungwa sindano baada ya wewe kuwa kwenye sehemu yenye maambukizi. Sindano hizi zinajumuisha kingamwili (immunoglobini) ambayo inasaidia kupigana na virusi. Kwa mfano, hizi ni sindano za immunoglobini za: