Chunjua wa Sehemu za Siri

(Maambukizi ya Papillomavirus ya Binadamu, au Maambukizi ya HPV)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

HPV (papillomavirus ya binadamu) ni nini?

HPV ni virusi vinavyosababisha chunjua. Kuna aina nyingi za HPV

  • Baadhi ya aina za HPV husababisha chunjua kwenye ngozi yako

  • Aina nyingine za HPV husababisha chunjua kwenye sehemu zako za siri (chunjua wa sehemu za siri)

Baadhi ya aina za HPV zinazosababisha chunjua kwenye sehemu za siri husababisha pia saratani.

Saratani unayopata kutokana na HPV hutokea katika sehemu ya mwili wako ambapo maambukizi yapo. Kwa hivyo ikiwa maambukizi yapo kwenye shingo la kizazi (sehemu ya chini ya uterasi yako inayofunguka hadi kwenye uke wako), unaweza kupata saratani ya mlango wa kizazi. Ikiwa maambukizi yako kwenye koo, unaweza kupata saratani ya koo.

Je, ninapataje maambukizi ya HPV?

HPV huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine Mtu huambukizwa aina za HPV zinazosababisha chunjua kwenye sehemu za siri kwa mgusano wa kingono, kama vile ngono ya kinywa, na mtu aliyeambukizwa.

Mtu wanaweza kuwa na maambukizi ya HPV bila kujua, kwa hivyo inawezekana usijue ikiwa mtu unayeshiriki mapenzi naye ameambukizwa. Huenda usijue kuwa una maambukizi ya HPV kwa sababu:

  • Maambukizi hayakusababisha chunjua zozote

  • Hukugundua chunjua(kwa sababu zilikuwa ndogo sana au zilikuwa ndani ya uke au rektamu yako)

Chunjua za sehemu za siri ni nini?

Chunjua za sehemu za siri ni matuta madogo ndani au karibu na eneo la uzazi.

  • Chunjua za sehemu za siri huwapata watu wengi—wanawake 8 kati ya 10 huambukizwa angalau mara moja kufikia umri wa miaka 50

  • Chunjua zinaweza kutokea kwenye msamba wako, kwenye tundu la haja kubwa, kwenye uume wako (wanaume), au ndani ya uke wako (wanawake)

  • Maambukizi mengi hutoweka yenyewe baada ya mwaka 1 hadi 2

  • Maambukizi ambayo hayatoweki huongeza uwezekano wa saratani

  • Kuna chanjo za kuzuia aina nyingi za chunjua za sehemu za siri zinazosababisha saratani

Dalili za ugonjwa wa chunjua za sehemu za siri?

  • Viuvimbe vidogo vidogo, laini, na unyevunyevu wa waridi au kijivu kwenye msamba, karibu na tundu la haja kubwa, kwenye uume wako (wanaume), au ndani ya uke wako (wanawake)

  • Wakati mwingine matuta hukua zaidi na kuwa mbaya na kutofautiana, kuonekana kama koliflawa ndogo

  • Wakati mwingine chunjua huuma au kuwasha

Madaktari wanawezaje kujua kama nina chunjua za sehemu za siri?

  • Madaktari kawaida hutambua chunjua za sehemu za siri kulingana na jinsi zinavyoonekana

  • Ikiwa chunjua hazionekani kama chujua za kawaida za sehemu za siri, daktari wako anaweza kufanya vipimo vya saratani na kaswende.

Ili kupima saratani, daktari wako anaweza kutoa chunjua na kuzipeleka kwenye maabara. Ikiwa chunjua ziko kwenye mlango wa kizazi, daktari wako anaweza pia kufanya kipimo cha Pap. Katika kipimo cha Pap, daktari huchukua sampuli ya seli kutoka kwa mlango wa kizazi wakati wa uchunguzi wa uzazi kwa ajili ya uchunguzi chini ya hadubini.

Ili kupima kaswende, daktari wako atakufanyia kipimo cha damu.

Madaktari hutibu vipi chunjua kwenye sehemu za siri?

Huenda daktari:

  • Kutumia leza, kugandamisha chunjua kwa kutumia dawa, au kufanya upasuaji ili kuondoa chunjua kwenye sehemu za siri kwenye mwili wako.

  • Kukupa mafuta ya kupaka kwenye chunjua zilizopo kwenye sehemu ya nje ya mwili wako

  • Kufanya upasuaji au kukupa chanjo za dawa kwa ajili ya chunjua zilizopo kwenye sehemu ya ndani ya mwili wako

Matibabu inaweza kuwa chungu au kuacha makovu. Ikiwa wewe ni mzima wa afya, madaktari wanaweza kuacha chunjua zitoweke zenyewe

Ninawezaje kuzuia chunjua za sehemu za siri?

Chanjo (inayotolewa kwa kudungwa) inaweza kuzuia HPV.

  • Wasichana na wavulana wanapaswa kupata chanjo hiyo wakiwa na umri wa miaka 11 hadi 12 au kabla ya kuanza kushiriki ngono ya aina yoyote, ikijumuisha ngono ya kinywa.

Kondomu husaidia, lakini haziwezi kuzuia kikamilifu chunjua za sehemu za siri kwa sababu ngozi ambayo haijafunikwa na kondomu inaweza kuambukizwa na HPV.