Saratani ya Mlango wa Kizazi

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023
Nyenzo za Mada

Saratani ya mlango wa kizazi ni nini?

Saratani ya mlango wa kizazi ni kansa ya shingo ya kizazi. Mlango wa uzazi ni sehemu ya chini ya (inayofunguka kwenye) uterasi yako (tumbo la uzazi). Inaunganisha uterasi yako na uke wako.

  • Saratani ya mlango wa kizazi mara nyingi husababishwa na maambukizi ya HPV (human papillomavirus), virusi vinayotokea sana ambavyo unaweza kuvipata kwa kufanya ngono bila kinga.

  • Huenda usionyeshe dalili hadi saratani itakapokua au kuenea

  • Saratani ya mlango wa kizazi inaweza kuenea kwa viungo vingine karibu na mlango wa kizazi au mwili wako wote

  • Matibabu inaweza kujumuisha upasuaji, minururisho, na tibakemikali

  • Madaktari wanaweza kugundua saratani ya mlango wa kizazi mapema sana kwa kufanya kipimo cha Pap

  • Chanjo ya HPV husaidia kuzuia saratani ya mlango wa kizazi

Internal Female Reproductive Anatomy

Ni nini husababisha saratani ya mlango wa kizazi?

Saratani ya mlango wa kizazi mara nyingi husababishwa na virusi vya HPV (human papillomavirus). Unaweza kupata HPV kwa kufanya ngono bila kinga. HPV pia husababisha chunjua kwenye sehemu za siri.

Je, dalili za saratani ya mlango wa kizazi ni zipi?

Saratani ya mlango wa kizazi mara nyingi haina dalili za mapema.

Dalili ya kwanza kwa kawaida ni:

  • Hali ya kuvuja damu kutoka ukeni isivyo kawaida, mara nyingi baada ya kushiriki ngono

Dalili za baadaye za saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na:

  • Kutokwa na damu nyingi zaidi wakati wa hedhi au kutokwa na damu kati ya hedhi moja na nyingine

  • Kutokwa na uchafu (majimaji) wenye harufu mbaya kwenye uke wako

  • Maumivu katika eneo la fupanyonga (sehemu iliyopo chini ya tumbo lako na kati ya nyonga)

  • Maumivu ya mgongo wa chini

Isipotibiwa, saratani ya mlango wa kizazi inaweza kusababisha kifo.

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nina saratani ya mlango wa kizazi?

Madaktari wanaweza kutumia kipimo cha pap kugundua saratani ya mlango wa kizazi na displasia ya mlango wa kizazi (ukuaji wa seli zinazoweza kusababisha saratani) Uchunguzi wa Pap unafanywa wakati wa uchunguzi wa fupanyonga.

  • Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huchunguza sehemu ya ndani ya uke wako kwa kuufungua akitumia kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu

  • Katika uchunguzi wa Pap, daktari wako huchukua seli kidogo kutoka kwa seviksi yako kwa kutumia usufi

  • Seli hizo huchunguzwa kwenye hadubini

Daktari akiona kuwa seli zako zinaonekana kuwa si kawaida, atachukua kipande kidogo cha seviksi yako ili kukichunguza kwa hadubini (kuondoa kipande cha tishu kwa uchunguzi).

Ikiwa una saratani ya mlango wa kizazi, madaktari wataona ukubwa wa saratani hiyo na imeenea kwa kiasi gani kwa kutumia vipimo kama vile:

Je, madaktari hutibu vipi saratani ya mlango wa kizazi?

Matibabu yanaweza kujumuisha:

Saratani ya mapema ambayo bado haijasambaa nje ya uso wa seviksi yako inaweza kuondolewa kwa upasuaji. Madaktari wanahitaji kutoa kipande cha kizazi chako tu (sio seviksi au uterasi yako yote) na upasuaji hufanywa kupitia uke wako. Taratibu zinajumuisha:

  • LEEP—waya nyembamba inayotumiwa pamoja na umeme kuondoa saratani

  • Leza—utaratibu huu unaweza kufanywa ofisini kwa daktari wako kwa kutumia dawa ya kutia ganzi kwenye maeneo ya tishu isiyo ya kawaida kwanza.

  • Upasuaji—upasuaji huu unafanywa hospitalini ukiwa umelala

Upasuaji huu hauathiri uwezo wako wa kupata mimba. Hata hivyo, utalazimika kujifungua watoto wako kupitia Upasuaji.

Saratani iliyoendelea zaidi ambayo haijaenea sana inaweza kutibiwa kupitia histerektomia. Katika histerektomia, daktari hutoa uterasi yako na wakati mwingine tishu zilizo karibu nayo. Wakati mwingine, madaktari watafanya tiba ya mionzi baada ya histerektomia. Ikiwa saratani imeenea, madaktari wanaweza kukupa tiba ya mionzi pamoja na tibakemikali pekee. Baada ya tiba ya mionzi na tibakemikali, wakati mwingine madaktari hufanya upasuaji ili kuondoa saratani iliyobaki.

Ninawezaje kuzuia saratani ya mlango wa kizazi?

Uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi unapendekezwa kwa kila mtu aliye na kizazi kuanzia umri wa miaka 21 hadi 25. Vipimo vya uchunguzi kwa kawaida hufanywa kila baada ya miaka 3 hadi 5, kulingana na umri wako na aina ya kipimo.

Unaweza kugundua saratani ya mlango wa kizazi kabla ya saratani kukua au kuenea kwa kufanya uchunguzi wa Pap mara kwa mara. Uchunguzi mwingine ni kipimo cha HPV ambacho hugundua uwepo wa HPV, virusi ambavyo vinaweza kusababisha ukuaji wa chunjua za sehemu za siri, seli zisizo za kawaida kwenye shingo ya kizazi, au saratani ya mlango wa kizazi.

Unaweza kusaidia kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa kupata chanjo ya HPV (sindano) ukiwa mdogo.

  • Chanjo hii hutolewa kwa dozi 2 au 3, kulingana na umri wa mtoto wakati wa kupata chanjo ya kwanza

  • Madaktari wanapendekeza wasichana na wavulana kupata chanjo hiyo wakiwa na umri wa miaka 11 au 12

Ikiwa hukupata chanjo ukiwa na miaka 11 au 12, unaweza kupewa na madaktari hadi ufikishe miaka 27.

Watu wazima wenye umri wa miaka 27 hadi 45 ambao hawajachanjwa wanapaswa kuzungumza na madaktari wao kuhusu iwapo wanapaswa kupewa chanjo.