Je, virusi vya herpesi ni nini?
Virusi vya herpesi ni kikundi cha virusi ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi mbalimbali. Ugonjwa ambao watu wengi wanauita "herpesi," unaoitwa herpesi simpleksi, ni mojawapo ya aina ya virusi vya herpesi.
Mara baada ya kupata maambukizi ya virusi vya herpesi, virusi hukaa mwilini mwako wakati wote wa maisha yako. Hii inamaanisha kuwa katika hali fulani, virusi vinaweza kuanza kufanya kazi. Vinapofanya hivyo, vinaweza au haviwezi kusababisha dalili tena.
Je, ni maambukizi gani yanayosababishwa na virusi vya herpesi?
Aina nyingi za virusi vya herpesi zinaweza kukuambukiza. Maambukizi yafuatayo kila moja husababishwa na aina maalumu ya kirusi cha herpesi:
Je, madaktari hutibu vipi maambukizi ya virusi vya herpesi?
Matibabu hutegemea aina ya maambukizi uliyonayo. Kwa mfano, kwa CMV na baadhi ya maambukizi ya virusi vya herpesi, madaktari hukupatia dawa za kuzuia virusi. Kwa tetekuwanga, madaktari hutibu dalili zako.
Chanjo zinaweza kuzuia tetekuwanga na malengelenge. Hakuna chanjo ya aina zingine za maambukizi ya virusi vya herpesi.