Posthepetiki Nyurolajia

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Baada ya kuwa na tetekuwanga, virusi vilivyoisababisha hukaa katika mwili wako maisha yako yote. Virusi vinapoanza kushughulika tena, unapata mkanda wa jeshi. Mkanda wa jeshi ni upele wenye uchungu wa malengelenge yaliyojaa majimaji.

Je, posthepetiki nyurolajia ni nini?

Kwa baadhi ya watu ambao wana mkanda wa jeshi, maumivu huendelea baada ya upele kupotea. Kwa sababu tetekuwanga na mkanda wa jeshi husababishwa na kirusi cha herpesi zosta, matatizo yanayotokea baada ya kupata mbwe huitwa "posthepetiki." Nyurolajia ni maumivu ya neva. Hivyo maumivu yanayoendelea baada ya kupata mkanda wa jeshi huitwa posthepetiki nyurolajia.

  • Kwa kawaida maumivu huwa katika eneo ambalo ulipata upele wa mkanda wa jeshi

  • Madaktari hawajui ni kwanini baadhi ya watu hupata posthepetiki nyurolajia

  • Watu wengi ambao hupata posthepetiki nyurolajia ni wenye umri wa zaidi ya miaka 50

  • Dawa za maumivu na malai huweza kusaidia kupunguza maumivu yako

  • Chanjo za tetekuwanga na mkanda wa jeshi zinaweza kusaidia kuzuia mbwe na posthepetiki nyurolajia

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa bado unahisi maumivu baada ya mkanda wa jeshi kupotea. Matibabu yanapaswa kuanza haraka iwezekanavyo.

Je, nini husababisha posthepetiki nyurolajia?

Baada ya kupata tetekuwanga, virusi hubaki kwenye mizizi ya neva zako, karibu na uti wako. Wakati mwingine virusi huanza kushughulika tena na kusababisha upele unaouma sana (mkanda wa jeshi) kwenye sehemu ya ngozi yako iliyoungana na mzizi wa neva wenye maambukizi.

Upele wa mkanda wa jeshi hujiondoa wenyewewe. Lakini kwa baadhi ya watu huendelea kuwa na maumivu makali katika eneo lililokuwa na upele. Madaktari hawajui ni kwanini hali hii hutokea kwa baadhi ya watu na kwanini haitokei kwa watu wengine.

Je, dalili za posthepetiki nyurolajia ni zipi?

Utakuwa na maumivu ya kuungua katika sehemu ya ngozi ambayo ulipata mkanda wa jeshi. Maumivu yanaweza:

  • Kuwa endelevu au kuja na kupotea

  • Kuwa mabaya nyakazi za usiku au wakati wa joto au baridi

  • Kudumu kwa miezi 3 au zaidi—takribani mtu 1 kati ya watu 5 atakuwa na maumivu yatakayodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina posthepetiki nyurolajia?

Madaktari watafahamu kwa kutegemea dalili zako na kwa sababu ulikuwa na mkanda wa jeshi hivi karibuni. Pia watakuchunguza ili kuthibitisha kuwa maumivu hayasababishwi ni kitu kingine.

Je, madaktari hutibu vipi posthepetiki nyurolajia?

Ikiwa una maumivu kiasi tu, madaktari watakwambia utumie dawa za maumivu za kununua kwenye duka la dawa (kama vile acetaminophen) au malai (kama vile capsaicin au lidocaine) ili kupunguza maumivu.

Hakuna tiba ya posthepetiki nyurolajia. Kwa watu wengi hupotea yenyewe ndani ya mwezi 1 hadi miezi 3.

Ikiwa una maumivu makali, madaktari watakutibu kwa:

  • Kukuandikia dawa ambazo huathiri jinsi neva zako zinavyofanya kazi

  • Kukuandikia dawa za kutuliza maumivu

  • Wakati mwingine, sindano za botox kwenye maeneo yenye maumivu

Je, ninawezaje kuzuia posthepetiki nyurolajia?

Vitu ambavyo vinazuia tetekuwanga na mkanda wa jeshi hupunguza uwezekano wa kupata posthepetiki nyurolajia Madaktari hupendekeza: