Muhtasari wa Mfumo wa Limfu

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Je, mfumo wa limfu ni nini?

Mfumo wa limfu ni mtandao wa mishipa na tezi za limfu ambao hubeba majimaji yanayoitwa limfu. Mfumo wa limfu ni sehemu ya mfumo wa kingamwili, ambayo husaidia kukulinda dhidi ya maambukizi na saratani.

Limfu ni majimaji yanayotoka kwenye mishipa yako midogo zaidi ya damu. Majimaji huingia katikati ya seli zako na huleta virutubishi na kubeba seli zilizoharibiwa, seli za saratani, na viini vilivyoangamizwa.

Mishipa ya limfu ni bomba ndogo zinazosafirisha limfu kutoka kwenye tishu hadi kwenye tezi limfu na kisha kutoka kwenye tezi limfu kurudi kwenye mishipa yako ya damu.

Tezi limfu ni sehemu za mkusanyiko zilizojaa seli nyeupe za damu maalum ambazo huchuja vijidudu na seli kutoka kwenye limfu. Hizi tezi na seli nyeupe za damu husaidia mwili wako kukukinga dhidi ya maambukizi na saratani. Na hii ndio sababu wakati mwingine maambukizi au saratani hufanya tezi limfu zilizo karibu zivimbe. Kwa mfano, maambukizi ya koo yanaweza kufanya tezi za limfu shingoni kuvimba. Watu huziita "tezi zilizovimba," lakini mafundo ya limfu sio tezi haswa.

Unaaweza ukawa na mishipa ya limfu kwenye mwili wako wote. Tezi za limfu zina tabia ya kukusanyika katika baadhi ya sehemu kama vile pembezoni mwa shingo lako, chini ya mikono yako, au kwenye kinena chako.

Mfumo wa Limfu: Kusaidia Kujikinga Dhidi ya Maambukizi

Mfumo wa kingamaradhi ni nini?

Mfumo wa kingamwili ni mfumo wa ulinzi wa mwili wako. Kazi ya mfumo wa kingamaradhi ni kushambulia vitu visivyo vya mwili wako, pamoja na:

  • Viini kama vile bakteria, virusi na kuvu

  • Vimelea

  • Seli za saratani

  • Vitu vingine vinavyoweza kuingia mwilini mwako, kama vile chavuo

Sehemu muhimu za mfumo wa kingamaradhi ni pamoja na:

  • Seli nyeupe za damu

  • Kingamwili

  • Mfumo wa limfu

Mfumo wa limfu unaweza kupata matatizo gani?

Mfumo wa limfu unaweza usifanye kazi vizuri kwa sababu ya:

  • Kuziba: Ikiwa mishipa ya limfu au tezi zitaziba kwa sababu ya upasuaji, tiba ya mionzi, jeraha, au maambukizi, limfu hukusanyika na kusababisha kuvimba kunakoitwa limfedema

  • Maambukizi: Ikiwa mwili wako hauwezi kuua vijidudu vyote vilivyoletwa kwenye tezi za limfu, tezi za limfu nazo zinaweza kupata maambukizi

  • Saratani: Ikiwa mwili wako hauwezi kuua seli za saratani zote zilizoletwa kwenye tezi limfu, saratani inaweza kukua kwenye tezi limfu