Je, eksirei ni nini?

Eksirei ni upimaji unaopiga picha ya sehemu za ndani za mwili wako. Inatumia kiasi kidogo cha miali ya eksirei. Eksirei huonyesha sehemu za mwili kulingana na uzito (ugumu) wake.

  • Madaktari hutumia eksirei kubaini matatizo ya sehemu ngumu za mwili kama vile mifupa yako

  • Eksirei si bora kama upimaji wa aina nyingine unaotumia picha kuonyesha sehemu nyororo za mwili kama vile misuli, kano, na ogani za ndani

  • Madaktari wanaweza kuunganisha eksirei kuunda picha za mwendo zinazoonyesha sehemu ya mwili ikifanya kazi, kama vile moyo ukipiga

Ninaweza kuhitaji eksirei kwa sababu gani?

Madaktari hutumia eksirei kuangalia iwapo kuna matatizo kama vile:

Kitu gani hufanyika wakati wa uchunguzi wa eksirei?

Kabla ya eksirei

Kwa kawaida hauhitaji kufanya chochote kabla ya eksirei.

Wakati wa eksirei

  • Utakaa tuli kabisa huku mashine ya eksirei ikipiga kila picha

  • Kila eksirei itachukua dakika chache tu

  • Kwa kawaida unahitaji eksirei kadhaa za kila sehemu ya mwili ili madaktari waweze kuona picha kutoka pembe mbalimbali

Baada ya eksirei

Unaweza kuendelea na shughuli zako za kawaida.

Uchunguzi wa eksirei una madhara gani?

Hatari kuu ya eksirei ni mionzi hatarishi. Madaktari hujaribu kupunguza jumla ya miali hatarishi unayopata katika maisha yako yote. Kupata mionzi kwa wingi kunaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani.

  • Eksirei nyingi hukuweka hatarini ya kiasi kidogo sana cha miali

  • Ikiwa wewe ni mjamzito au unashukiwa kuwa mjamzito, madaktari watakinga tumbo yako dhidi ya miali hatarishi