Uchunguzi wa tomografia ya utoaji wa positron (PET) ni nini?
Uchunguzi wa PET ni kipimo wanachofanya madaktari ili kupiga picha za ogani na tishu zako. Kwanza, madaktari hukudunga kiasi kidogo cha chembechembe nunurishi (elementi ya kuchunguza). Elementi hiyo ya kuchunguza huunganishwa na kemikali inayotumiwa na mwili wako, kama vile sukari (glukosi). Mashine kubwa yenye umbo la donati hufanya uchunguzi wa mwili wako huku ikitumia elementi ya kuchunguza. Kompyuta huchukua matokeo ya uchunguzi huu na kuunda picha zenye maelezo ya kina ya jinsi sehemu za ndani ya mwili wako zinavyofanya kazi. Kila picha inaonekana kama kipande kilichochukuliwa kutoka sehemu moja ya mwili wako. Kompyuta pia inaweza kuunda picha ya 3-D ya sehemu ya ndani ya mwili wako.
Uchunguzi wa PET ni bora katika kuonyesha jinsi ubongo au moyo wako unavyofanya kazi
Madaktari hufanya uchunguzi wa PET ili kubaini iwapo kuna saratani au kufuatilia iwapo saratani imeenea
Unapata miali zaidi hatarishi kuliko inayotokana na eksirei
Uchunguzi wa PET ni ghali na haupatikani katika baadhi ya maeneo
Ninaweza kuhitaji uchunguzi wa PET kwa sababu gani?
Madaktari hufanya uchunguzi wa PET kuangalia matatizo ya aina nyingi, ikiwa ni pamoja na:
Matatizo ya usafirishaji wa damu yako
Matatizo ya utendakazi wa ubongo au moyo wako
Kuchunguza saratani
Kuangalia iwapo matibabu yako ya saratani yanafanya kazi vizuri au iwapo saratani yako imeenea
Kitu gani hufanyika wakati wa uchunguzi wa PET?
Kabla ya kupimwa
Daktari wako atakwambia usinywe pombe, kahawa, tumbaku, au dawa fulani kwa kipindi cha muda fulani kabla ya upimaji. Mwambie daktari wako kama wewe ni mjamzito au unanyonyesha.
Wakati wa kupimwa
Madaktari hukupa elementi ya kuchunguza kwa kuidunga kwenye mshipa wako. Huwa inachukua kati ya dakika 30 na 60 kwa kinakilishi kuzunguka kwenye mwili wako wote.
Utalala kwenye meza nyembamba yenye vigurudumu. Madaktari watatelezesha meza hiyo kwenye sehemu ya katikati ya mashine ya uchunguzi yenye umbo la donati. Utalala tuli kwa dakika 45 huku mashine ikikuchunguza. Huenda ukasikia sauti za mwaliko au za kuvurumisha. Wakati mwinine, madaktari hukuomba ufanye mambo fulani, kama vile kujibu maswali, wanapochunguza ubongo wako.
Baada ya kupimwa
Unaweza kuendelea na shughuli zako za kawaida.
Uchunguzi wa PET una madhara gani?
Mionzi
Uchunguzi wa PET hukuweka kwenye mionzi hatari kuliko eksirei moja. Madaktari hujaribu kupunguza mara ambazo unawekwa kwenye mionzi. Mionzi kwa wingi inaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani.
Athari kutokana na elementi ya kuchunguza
Mmenyuko wa mzio kutokana na elementi ya kuchunguza inayotumiwa wakati wa uchunguzi wa PET ni nadra lakini unaweza kutokea kwa baadhi ya watu.