Angiografia (angiogramu) ni nini?
Angiografia ni uchunguzi wa kimatibabu ambao huhusisha kuchukua picha za mishipa yako ya damu kwa kutumia eksirei. Picha inayochukuliwa inaitwa angiogramu.
Kwa kawaida madaktari huhitaji picha 1 au 2 tu za mishipa ya damu katika eneo lenye tatizo, si mishipa yako yote ya damu. Ili kupata picha hii, madaktari hutumia sindano kuweka katheta (mrija mwembamba, unayonyumbulika) kwenye mshipa wa damu karibu na eneo lenye tatizo. Kisha huingiza kiowevu (majimaji yenye kutofautisha) kupitia katheta. Majimaji yenye kutofautisha huonekana kwenye eksirei (video au picha), kwa hivyo huonyesha sehemu ya ndani ya mishipa ya damu. Picha zinaonyesha kama damu yako inapitishwa vizuri na ikiwa kuna matatizo kwenye mishipa yako ya damu.
Madaktari kwa kawaida huingiza katheta kupitia mkato mdogo kwenye kinena au mkono wako
Angiografia hutumiwa kugundua matatizo katika mishipa yako ya damu
Wakati wa angiografia, madaktari wanaweza pia kutibu tatizo wanaloona kwenye mishipa yako ya damu
Ninaweza kuhitaji angiografia kwa sababu gani?
Unaweza kuhitaji angiografia ikiwa madaktari wanadhani una matatizo ya mishipa ya damu:
Kuziba (kama vile damu iliyoganda iliyosababisha shambulio la moyo au kiharusi)
Kubanika (kama vile kunakosababishwa na ateri kuwa ngumu)
Uvimbe kwenye ukuta wa mshipa dhaifu wa damu (perema)
Kuchanika kwa mshipa wa damu
Kwa kawaida madaktari hufanya angiografia kwenye ateri. Ateri ni mishipa ya damu ambayo husafirisha damu kutoka kwa moyo wako hadi kwa mwili mzima ikiwa ni pamoja na kwenye misuli ya moyo. Angiografia katika ateri inaitwa ateriografia.
Ingawa ni nadra, madaktari hufanya angiografia katika mishipa. Vena ni mishipa ya damu inayorudisha damu kwenye moyo wako. Angiografia katika mishipa inaitwa venografia.
Ni nini hufanyika wakati wa angiografia?
Kipimo kinaweza kudumu kwa chini ya saa moja hadi saa kadhaa, kulingana na mishipa ya damu ambayo madaktari wanataka kuona.
Kabla ya kupimwa
Madaktari watakuagiza usile au kunywa chochote kwa saa 12.
Wakati wa kupimwa
Utapata dawa ya kukusaidia kutlia lakini usilale
Madaktari watakupa dozi ya kufisha ganzi eneo ambalo wataweka mkato mdogo, kwa kawaida kwenye kinena chako au wakati mwingine kwenye mkono wako.
Wataingiza katheta kwenye sehemu iliyokatwa na kuiweka kwenye mishipa wanayotaka kuchunguza
Wataingiza majimaji yenye kutofautisha kupitia katheta
Mashine za eksirei zitapiga picha wakati majimaji yenye kutofautisha yanapita kwenye mishipa yako ya damu
Wakati wa uchunguzi, madaktari wanaweza kuvuta pumzi nyingi, ushikilie pumzi yako, au ukohoe
Baada ya kupimwa
Madaktari huondoa katheta na kuweka shinikizo kwenye mkato ili kuzuia damu kuvuja. Unaweza kuhitajika kujilaza kwa saa kadhaa. Wakati mwingine, unaweza kuhitaji kulazwa usiku mzima hospitalini. Madaktari wanaweza kukuambia upumzike na kunywa maji ya ziada.
Hatari za angiografia ni zipi?
Mionzi
Angiografia hukuweka kwenye mnururisho zaidi kuliko eksirei moja. Kwa mfano, kipimo cha mnururisho katika angiografia ya moyo ni mara 350 hadi 750 zaidi ya kile kinachotumiwa katika eksirei ya kifua. Madaktari hujaribu kupunguza mara ambazo unawekwa kwenye mionzi katika maisha yako yote. Mionzi kwa wingi inaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani.
Matatizo mengine
Sindano zinaweza kuwa chungu kidogo
Wapo watu ambao huhisi usumbufu majimaji yenye kutofautisha yakiingia
Wengine hupata mmenyuko wa mzio kutokana na majimaji yenye kutofautisha (kama vile kupiga chafya, upele, au shida ya kupumua)
Ikiwa una matatizo ya figo, majimaji yenye kutofautisha yaweza kufanya matatizo yako ya figo kuwa mabaya zaidi
Sehemu ya mwili wako ambapo madaktari huingiza katheta inaweza kutoka damu, kupata maambukizo, au kuwa na uchungu