Shambulio la moyo

(Shambulio la Moyo)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Shambulio la moyo ni nini?

Shambulio la moyo ni wakati mtiririko wa damu kwenye sehemu ya moyo wako umezuiwa ghafla na sehemu ya misuli ya moyo wako inakufa.

  • Nenda kwenye kitengo cha dharura na utafune tembe ya aspirini ikiwa unafikiri kuwa unapata shambulio la moyo

  • Huenda ukahisi shinikizo kwenye kifua, kushindwa kupumua, na hisia ya uchovu ikiwa unapata tatizo la moyo

  • Wakati mwingine shambulio la moyo linaweza kusababisha dalili ndogo au lisisababishe dalili zozote (shambulizi tuli la moyo)

  • Madaktari hufanya vipimo vya damu na ECG/EKG (elektrokadiografia) ikiwa una dalili za shambulio la moyo

  • Daktari atakupa dawa na kukutibu ili kujaribu kuelekeza damu zaidi kwenye sehemu ya moyo wako iliyoathirika

Je, ni nini husababisha shambulio la moyo?

Moyo ni msuli unaosukuma damu. Kama ilivyo kwa misuli yote, moyo unahitaji damu ya kutosha ili kufanya kazi. Damu inayosukumwa moyoni haifikii msuli wa moyo. Badala yake, msuli wa moyo hulishwa na ateri zake zenyewe. Ateri hizi zinaitwa ateri za moyo.

Mashambulizi mengi ya moyo hutokea wakati mojawapo ya ateri zako za moyo imezuiwa ghafla na damu iliyoganda.

Kwa kawaida, damu huganda kwenye ateri za moyo ukiwa na tatizo la atherosklerosisi:

  • Usanisi wa mishipa ya damu unajulikana kama kugandamana kwa ateri

  • Usanisi wa miship ya damu ni pale kolesteroli na utando wa mafuta mengine unarundika polepole kwenye ateri zako

  • Mrundiko huu unaitwa atheroma au utando

  • Utando unaweza kupasuka ghafla, na kusababisha donge la damu ambalo linaziba ateri

Ateri iliyozibwa hairuhusu damu ipite hadi kwenye sehemu ya musuli wa moyo wako. Mtiririko wa damu ukikatishwa kwa zaidi ya dakika chache, sehemu hiyo ya musuli wa moyo wako hufa. Musuli uliokufa hauwezi kupiga damu, kwa hivyo moyo wako huwa dhaifu. Midundo ya moyo wako inaweza pia kuathiriwa, na kuufanya upige kwa haraka sana au polepole sana. Wakati mwingine, moyo wako utasimama kabisa (mshtuko wa moyo) na utakufa.

Sehemu ya musuli wa moyo wako inapokufa, huwa hairudi. Musuli uliokufa hubadilika na kuwa tishu ya kovu.

Dalili za shambulio la moyo ni zipi?

Dalili za shambulio la moyo ni sawa na za angina, lakini maumivu huwa makali zaidi, yanadumu kwa muda mrefu, na hayapungui unapopumzika.

  • Huenda ukahisi maumivu katikati ya kifua

  • Maumivu yanaweza kusambaa mgongoni, kwenye taya, au mkono wa kushoto

  • Japo ni nadra, wakati mwinigne maumivu husambaa kwenye mkono wa kulia

  • Maumivu yanaweza kutokea kwenye sehemu moja au zaidi kati ya hizi na wala si kwenye kifua

  • Huenda ukahisi woga au kutokwa jasho

  • Midomo, mikono, au miguu yako huenda ikabadilika na kuwa bluu kidogo

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nina shambulio la moyo?

Madaktari hufanya vipimo kama vile:

  • ECG/EKG—kipimo cha kuchunguza jins moyo wako unavyofanya kazi

  • Kufanya vipimo vya damu kuchunguza elementi fulani zinazoonyesha matatizo ya moyo

Madaktari hutibu vipi shambulio la moyo?

Utalazwa hospitalini. Madaktari watajaribu:

  • Kufungua ateri iliyozibwa ili kuokoa kiwango kikubwa cha musuli wa moyo wako kadiri iwezekanavyo

  • Kutibu tatizo lililosababisha shambulio la moyo wako

Madaktari pia:

  • Kudhibiti mapigo ya moyo wako na shinikizo la damu

  • Kukupa dawa za kuzuia damu kuganda

  • Kukupa dawa za kufanya moyo upige kawaida

Watafungua ateri zilizozibwa

Kwa kutegemea mahali ateri zako za moyo zimezibwa, madkatra wanaweza:

  • Kukupatia dawa kupitia kwenye mshipa ili kuyeyusha damu iliyoganda

  • Kufanya upasuaji wa kufungua mshipa

  • Kufanya upasuaji wa kukwepa

Dawa za kuyeyusha damu iliyoganda unayopewa kupitia kwenye mshipa (IV) zinaweza kufungua ateri ya moyo iliyozibwa. Hata hivyo, dawa hizo hufanya kazi iwapo tu utazipata ndani ya saa chache baada ya shambulio la moyo wako kuanza. Pia, dawa za kuyeyusha damu iliyoganda hazifai kwa kila mtu. Huenda zisiwe salama kwa watu waliopata kiharusi au upasuaji mkubwa hivi majuzi, au watu ambao wana shinikizo la damu la juu.

Wakati wa upasuaji wa kufungua mshipa:

  • Daktari hutia mrija mwembamba, unaoweza kupinda (katheta) kwenye mshipa wa sehemu ya juu ya mguu wako (kinena) au kwenye kifundo cha mkono

  • Katheta inasukumwa ndani kwenye ateri hadi kwenye moyo wako kisha kwenye moja ya ateri za moyo

  • Puto ndogo kwenye ncha ya katheta inatiwa hewa

  • Puto husukuma na kuzibua mshipa

  • Kisha daktari anatia mrija wenye wavu (kipanuzi) mwisho wa katheta na kuisogeza sehemu iliyozibwa.

  • Mrija wenye wavu husaidia kupanua sehemu iliyozibwa

Wakati wa upasuaji wa kupandikiza mshipa:

  • Daktari huchukua kipande cha ateri au mshipa usio na tatizo kutoka sehemu nyingine ya mwili wako

  • Anapandikiza ncha moja ya kipande hicho cha ateri au mshipa kwenye aota yako (mshipa mkuu unaobeba damu kutoka kwenye moyo hadi sehemu nyingine zote za mwili)

  • Anapachika upande wa pili wa ateri yako iliyoziba bila kupitia sehemu hiyo

  • Kisha damu yako inatiririka kupitia mkondo huu mpya, bila kizuizi

Kutibu kisababishi cha shambulio la moyo wako

Kutibu tatizo lililosababisha shambulio la moyo wako, kwa kawaida madaktari hukupa:

Daktari pia atakuruhusu ubadili tabia zozote zinazoumiza moyo wako, kama vile kuvuta sigara, kutofanya mazoezi, na kutokula lishe bora.

Je, ninawezaje kuzuia shambulio la moyo?

Epuka tabia zinazoweza kuudhuru moyo wako

  • Kula vyakula bora kwa afya, kama vile matunda na mboga na vyakula vingine vyenye nyuzinyuzi kwa wingi

  • Kula mafuta kidogo kutoka kwenye nyama, maziwa, na vyakula vilivyotengenezwa viwandani (kama vile piza iliyogandishwa au chakula kinachopashwa moto kwa maikrowevu)—zungumza na daktari wako kuhusu kiasi na aina za mafuta unazopaswa kula

  • Kupunguza uzani ikiwa unahitaji

  • Kufanya mazoezi kwa kutumia uzani au kutembea

  • Kuacha kuvuta sigara, kunywa pombe, au kutumia dawa haramu—inaweza kuwa vigumu kuacha kutumia dawa hizi, kwa hivyo zungumza na daktari au mshauri wako wa kisaikolojia kuhusu jinsi ya kupata usaidizi

Kumeza dawa zako inavyofaa