Muhtasari wa Ugonjwa wa Ateri za Moyo (CAD)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Ugonjwa wa ateri za moyo ni nini?

Moyo ni msuli unaosukuma damu. Kama ilivyo kwa misuli yote, moyo unahitaji damu ya kutosha ili kufanya kazi. Damu inayosukumwa moyoni haifikii msuli wa moyo. Badala yake, msuli wa moyo husafirishiwa damu na ateri zake zenyewe. Ateri hizi zinaitwa ateri za moyo.

Ugonjwa wa ateri za moyo (ugonjwa wa moyo) hutokea pale ambapo mtiririko wa damu kwenye ateri za moyo umezuiwa kidogo au kabisa.

  • Ugonjwa wa ateri za moyo ndiyo kisababishi kikuu cha angina, angina isiyo thabiti, na shambulio la moyo

  • Una uwezekano zaidi wa kuugua ugonjwa wa ateri za moyo ikiwa wewe ni mzee, mwanamume, au una mzazi, nyanya au babu ambaye alipata ugonjwa wa ateri za moyo kabla ya kufikisha umri wa miaka 50

  • Sababu iliyozoeleka ni kugandamana kwa ateri (atherosklerosisi)

Angina isiyo thabiti na shambulio la moyo vinaweza kusababisha midundo ya moyo isiyo ya kawaida au ifanye moyo wako uache kupiga. Unaweza kuaga dunia usipotibiwa haraka. Pia, shambulio la moyo husababisha madhara ya kudumu ya moyo.

Supplying the Heart With Blood

Like any other tissue in the body, the muscle of the heart must receive oxygen-rich blood and have waste products removed by the blood. The right coronary artery and the left coronary artery, which branch off the aorta just after it leaves the heart, deliver oxygen-rich blood to the heart muscle. The right coronary artery branches into the marginal artery and the posterior interventricular artery, located on the back surface of the heart. The left coronary artery (typically called the left main coronary artery) branches into the circumflex and the left anterior descending artery. The cardiac veins collect blood containing waste products from the heart muscle and empty it into a large vein on the back surface of the heart called the coronary sinus, which returns the blood to the right atrium.

Nini husababisha ugonjwa wa ateri za moyo?

Sababu iliyozoeleka zaidi ya ugonjwa wa ateri za moyo ni atherosklerosisi, ambao kwa kawaida hujulikana kama kugandamana kwa ateri. Katika atherosklerosisi, lehemu na utando wa mafuta mengine hurundikana polepole kwenye ateri zako. Mrundiko huu unaitwa atheroma au utando. Utando huo unaweza:

  • Kufanya ateri iwe nyembamba na kuzuia kwa kiasi fulani damu inayokwenda kwenye moyo wako

  • Kupasuka ghafla na kusababisha damu iliyoganda inayoziba ateri na kusababisha shambulio la moyo

Sababu zisizotokea sana ni pamoja na mkazo wa ghafla wa ateri ya moyo, hususan kutokana na matumizi ya dawa haramu kama vile kokeni. Wakati wa mkazo huu, ateri hubana ghafla na kufunga. Ikikaa katika hali hiyo ya kufungwa kwa muda mrefu, unaweza kupata shambulio la moyo. Kwa kawaida mkazo huo huacha na ateri kufunguka tena.

Ni zipi hatari zinazohusiana na ugonjwa wa aateri za moyo?

Hatari ambazo unaweza kudhibiti au kuzuia:

Hatari ambazo ni muhimu kuzifahamu lakini haziwezi kudhibitiwa:

  • Kuwa na watu kwenye familia yako waliopata ugonjwa wa ateri za moyo kabla ya kufikisha miaka 55

  • Kwa wanaume

  • Kukua zaidi

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa ateri za moyo?

Daktari wako atakuuliza maswali kuhusu dalili zako na kukufanyia uchunguzi wa kimwili na vipimo vya damu.

Ikiwa una dalili za ateri iliyozibwa, daktari wako anaweza kufanya vipimo:

  • Kipimo cha shinikizo—kipimo cha kubaini ikiwa moyo wako unapata damu ya kutosha unapofanya kazi nzito (ukihitaji kusukuma damu upesi), kama vile unapofanya mazoezi

  • ECG/EKG (elektrokadiografia)—kipimo kinachopima shughuli za umeme za moyo wako, ambazo zinaweza kuwa si za kawaida ukiwa na ugonjwa wa ateri za moyo

  • Uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta—kipimo kinachoruhusu madaktari kuona iwapo ateri zako zimeziba na mahali ambapo zimeziba kwa kuweka katheta ndefu nyembamba (tyubu ndogo inayopindika) kwenye mshipa wa ateri wa mkono au mguu wako, kuelekea kwenye moyo wako na ndani ya ateri zako za moyo kisha wanadunga dutu ya kutofautisha inayoonekana kwenye eksirei

  • Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta)—kipimo cha picha cha kuchunguza kugandamana kwa ateri za moyo

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa ateri za moyo?

Madaktari hutibu tatizo linalosababisha ugonjwa wako wa ateri za moyo, ambalo kwa kawaida huwa kugandamana kwa ateri. Huenda daktari akafanya yafuatayo:

  • Kukupa dawa za kupunguza mzigo wa kazi kwenye moyo, kama vile dawa za shinikizo la damu

  • Kukupa dawa za kupunguza lehemu yako

  • Kukuomba ubadili tabia zozote mbaya zinazoweka kuumiza moyo wako—kama vile kuvuta sigara, kutofanya mazoezi, na kutokula lishe bora

  • Wakati mwingine kufanya upasuaji ili kufungua ateri iliyozibwa

Kulingana na kiasi cha kugandamana kwa ateri zako za moyo, huenda daktari akafanya upasuaji kukwamua ateri yako. Wanaweza kufanya upasuaji wa kufungua mshipa au kuunda mkondo mpya wa damu (pia inajulikana kama kupandikizwa kwa ateri ya moyo au kupachikwa kwa ateri ya moyo).

Wakati wa upasuaji wa kufungua mshipa:

  • Daktari hutia mrija mwembamba, unaoweza kupinda (katheta) kwenye mshipa wa sehemu ya juu ya mguu wako (kinena) au kwenye kifundo cha mkono

  • Katheta inasukumwa ndani kwenye ateri hadi kwenye moyo wako kisha kwenye moja ya ateri za moyo

  • Puto ndogo kwenye ncha ya katheta inatiwa hewa

  • Puto husukuma na kuzibua mshipa

  • Kisha daktari anatia mrija wenye wavu (kipanuzi) mwisho wa katheta na kuisogeza sehemu iliyozibwa.

  • Mrija wenye wavu husaidia kupanua sehemu iliyozibwa

Wakati wa upasuaji wa kupandikiza mshipa:

  • Daktari huchukua kipande cha ateri au mshipa usio na tatizo kutoka sehemu nyingine ya mwili wako

  • Anapandikiza ncha moja ya kipande hicho cha ateri au mshipa kwenye aota yako (mshipa mkuu unaobeba damu kutoka kwenye moyo hadi sehemu nyingine zote za mwili)

  • Anapachika upande wa pili wa ateri yako iliyoziba bila kupitia sehemu hiyo

  • Kisha damu yako inatiririka kupitia mkondo huu mpya, bila kizuizi

Je, ninawezaje kuzuia au kukomesha ugonjwa wa ateri za moyo?

Epuka tabia zinazoweza kuudhuru moyo wako

  • Kuacha kuvuta sigara—Hii ndiyo njia muhimu zaidi ya kuzuia au kukomesha ugonjwa wa ateri za moyo

  • Kula vyakula bora kwa afya, kama vile matunda na mboga na vyakula vingine vyenye nyuzinyuzi kwa wingi

  • Kula mafuta kidogo kutoka kwenye nyama, maziwa, na vyakula vilivyotengenezwa viwandani (kama vile piza iliyogandishwa au chakula kinachopashwa moto kwa maikrowevu)—zungumza na daktari wako kuhusu kiasi na aina za mafuta unazopaswa kula

  • Kupunguza uzani ikiwa una uzani mkubwa kupita kiasi

  • Kufanya mazoezi kwa kutumia uzani au kutembea

  • Kuacha kutumia dawa haramu—inaweza kuwa vigumu kuacha kutumia dawa hizi, kwa hivyo zungumza na daktari au mshauri wako wa kisaikolojia kuhusu jinsi ya kupata usaidizi

Kumeza dawa zako inavyofaa