Elektrokadiografia

(ECG; EKG)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Ekokadiografia (ECG, EKG) ni nini?

Elektrokadiografia ni kipimo ambacho hupima shughuli ya umeme ya moyo wako. Ni cha haraka, hakina maumivu na madhara.

Matokeo ya kipimo hicho yanaonyeshwa kwenye elektrokadiogramu. Kina mkao wa mstari wa mawimbi ulio na miiba kwenye fito umeme (ya mchoro). Elektrokadiogramu hupea madaktari maelezo kuhusu:

  • Sehemu ya moyo wako ambayo huchochea kila mdundo wa moyo

  • Njia za umeme za moyo wako

  • Mdundo na mpigo wa moyo wako

Kwa nini ninaweza kuhitaji ECG:

Unaweza kufanyiwa ECG:

Je, ECG hufanywa vipi?

  • Sensa ndogo za mviringo (elektrodi) ambazo hunata kwenye ngozi zinawekwa kwenye mikono, miguu na kifua chako

  • Waya ambazo zinajishikilia kwenye sensa zinaunganishwa kwenye mashine

  • Vile moyo wako unadunda, sensa hupima mikondo ya umeme ya moyo wako

  • Mashine hurekodi maelezo kutoka kwa kila sensa na kutengeneza ECG (mstari wenye mkao wa mawimbi na miiba) ili daktari wako asome

Je, kuna athari zozote mbaya za ECG?

Hakuna madhara. ECG haitaumiza hata kidogo wakati wa au baada ya kipimo.

Je, daktari wangu anaweza kujua nini kutokana na ECG yangu?

ECG husaidia daktari wako kujua mambo mengi kuhusu moyo wako, ikijumuisha:

  • Ikiwa umewahi kuwa na au una shambulio la moyo

  • Ikiwa una ridhimu ya moyo isiyo ya kawaida

  • Ikiwa moyo wako haupati damu na oksijeni ya kutosha

  • Ikiwa ukuta wa misuli wa moyo wako ni mnene mno

  • Ikiwa kuna uvimbe kwenye sehemu hafifu za kuta za moyo wako (uvimbe huo unaitwa perema)

Ninapaswa kubeba nakala ya ECG yangu?

Ikiwa umekuwa na matatizo ya moyo, unaweza kuhitaji kujiwekea nakala ya ECG yako (uliza daktari wako kama unafaa). Hivyo, ikiwa una dharura, daktari anayekutibu anaweza kulinganisha ECG yako ya kitambo na ECG mpya.