Kupima Shinikizo

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Kipimo cha shinikizo ni nini?

Kipimo cha shinikizo huruhusu madaktari kuona jinsi moyo wako hufanya kazi wakati uko katika shinikizo, kama vile unapofanya mazoezi. Matatizo mengi ya moyo ni rahisi kwa daktari wako kuyapata wakati moyo wako unatia bidii.

Kwa nini ninaweza kuhitaji kipimo cha shinikizo?

Mara nyingi, unaweza kufanyiwa kipimo cha shinikizo ikiwa unapata maumivu ya kifua. Unaweza pia kuhitaji kipimo cha shinikizo ikiwa una tatizo la moyo na daktari wako anataka kuona kama inakuwa mbaya zaidi.

Kipimo cha shinikizo kinafanywa vipi?

  • Sensa ndogo za mviringo (elektrodi) zinawekwa kwenye mikono, miguu na kifua chako ili kupima mikondo ya umeme ya moyo wako (inaitwa elektrokadiogramu, au ECG)

  • Utavaa mkanda wa shinikizo la damu kwenye mkono wako

  • Utatembea kwenye gurudumu la mazoezi au pedali kwenye baiskeli ya mazoezi, kuongeza kasi baada ya muda

  • Vile unafanya mazoezi, madaktari watatazama ECG yako na kukagua shinikizo la damu yako mara nyingi

  • Ikiwa hauwezi kufanya mazoezi vya kutosha ili kufanya kipimo, madaktari watakupea dawa ili kufanya mpigo wa moyo wako uwe na kasi zaidi na imara zaidi

Madakatri watasitisha kipimo wakati:

  • Kipimo cha mapigo ya moyo wako unakaribia mpigo wa juu kabisa unaopendekezwa kwa umri wako

  • Dalili zako zinaanza kusumbua sana—unaweza kuwa na maumivu ya kifua au kuhisi kana kwamba hauwezi kupumua

  • Rekodi za shinikizo la damu au ECG yako zinaonyesha kitu kisicho cha kawaida

Wakati mwingine badala ya kufanyiwa ECG wakati wa kipimo cha shinikizo, unaweza ukafanyiwa ekokadiografia au upigaji picha kwa isotopu. Vipimo hivi pia huwezesha daktari wako kuona jinsi moyo wako unavyokabiliana na shinikizo. Vipimo hivi ni sahihi zaidi lakini vya bei ghali zaidi.

Je, kuna athari zozote mbaya kutokana na kipimo cha shinikizo?

Kwa kawaida utafanya mazoezi ya kutosha kukufanya uhisi uchovu na kukuhemesha. Ikiwa una tatizo la moyo, unaweza kuhisi maumivu kifuani au kuhisi mapigo ya moyo unapofanya upimaji. Ingawa ni nadra, unaweza kupata shambulio la moyo wakati wa upimaji. Lakini daktari wako atakufuatilia wakati wa upimaji ili kuwa tayari kwa matatizo yoyote.

Je, daktari wangu anaweza kujifunza nini kutokana na kipimo cha shinikizo?

Vipimo vya shinikizo husaidia madaktari:

  • Tafuta dalili za ugonjwa wa ateri ya moyo, ambao ni wakati una mtiririko mdogo zaidi wa damu kwenye moyoni

  • Tambua iwapo una tatizo la moyo au la mapafu, au ikiwa unahitaji tu kufanya mazoezi