Ekokadiografia na Utaratibu mwingine wa ultrasonografia

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Ekokadiografia ni nini?

Ekokadiografia pia wakati mwingine inaitwa ekokadiografia au eko. Eko ni picha iliyopigwa kwa kutumia mawimbi ya sauti kwenye moyo wako. Mawimbi ya sauti huduta kwenye moyo wako ili kuunda picha inayosonga ya moyo wako. Kipimo hiki hakina maumivu, madhara na ni cha haraka.

Aina kuu za eko ni za pande mbili, pande tatu, Doppler na Doppler ya rangi. Mchakato wa kupata vipimo hivi ni sawa, lakini kila kipimo kinaonyesha daktari kitu tofauti. Daktari atakwambia ni kipimo gani ambacho kinakufaa.

Kwa nini ninaweza kuhitaji eko?

Unaweza kuhitaji eko ikiwa daktari wako anashuku aina fulani ya matatizo ya moyo kama vile:

Dalili za matatizo kama hayo zinajumuisha maumivu ya kifua, tatizo katika upumuaji, kuhisi kuzirai na miguu kuvimba.

Je, eko hufanywa aje?

  • Mtaalamu wa upimaji kwa kutumia mawimbi ya sauti atapaka mafuta kwenye kifua chako — mafuta hayo husaidia mawimbi ya sauti kupita kutoka kwenye mashine hadi kwenye mwili wako

  • Mtaalamu anashikilia kifaa cha upimaji kwa kutumia mawimbi ya sauti (wadi) dhidi ya kifua chako

  • Kifaa hicho hutuma mawimbi ya sauti yenye mtetemo ambayo hurejea (kuduta) kwenye moyo wako

  • Mingwi hizi zinabadilishwa kuwa picha ya video ya moyo wako

Ikiwa madaktari wanahitaji kuangalia kwa ukaribu sana sehemu fulani za moyo wako, wanaweza kuweka kifaa cha upimaji kwa kutumia mawimbi ya sauti chini kwenye koo yako. Taratibu hii inaitwa ekokadiografia ya transesofajili. Kabla ufanyiwe kipimo hiki, utapewa dawa ya kufanya ganzi koo yako na dawa nyingine ili kukusaidia kutulia.

Je, kuna athari mbaya zozote zinazotokana na eko?

Eko zinazofanywa kwa kifaa cha upimaji kwa kutumia mawimbi ya sauti kikiwa kimeshikiliwa dhidi ya kifua chako hazina maumivu hata kidogo. Hakuna madhara. Hauwezi kusikia mawimbi ya sauti.

Eko zinazofanywa kwa kifaa cha upimaji kwa kutumia mawimbi ya sauti kikiwa kimeingizwa chini kwenye koo yako zinaweza kukufanya utapike kiuongo. Daktari wako huweka dawa kwenye koo yako ili kuifanya ganzi. Utapewa dawa nyingine ili kukufanya uingie usingizini. Koo yako inaweza kuhisi uchungu kiasi baada ya kipimo.

Je, daktari wangu anaweza kujua nini kutokana na eko?

Uchunguzi wa eko huwaruhusu madaktari kuangalia:

  • Kama misuli ya moyo inasonga kwa njia ya kawaida

  • Kama damu ya kutosha inasukumwa nje kwa kila mdundo wa moyo

  • Kama moyo wako umeongezeka kwa ukubwa

  • Kama vali kwenye moyo wako zinafanya kazi kawaida

  • Kama kiowevu kinakusanyika kando ya moyo wako