Uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta ni nini?

uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta (inayoitwa pia kath ya mishipa ya moyo) ni taratibu ya moyo inayofanyiwa hospitalini. Daktari huweka mrija mwembamba wa plastiki (katheta) kupitia kwenye ateri na kwenye moyo wako. Madaktari huweka mrija huo kwenye moyo wako kwa kuuwekwa aidha kwenye:

  • Ateri kubwa kwenye kinena chako

  • Ateri ndogo kwenye kifundo cha mkono wako

Ateri zako zimeunganishwa kwenye moyo wako. Ili daktari aweze kusukuma katheta kupitia kwenye ateri hadi kwenye moyo wako.

Wakati katheta iko kwenye moyo wako, daktari hunyunyizia kiowevu maalum kupitia kwenye katheta. Kiowevu hicho (kinachoitwa majimaji yenye kutofautisha) huonekana kwa uangavu kwenye eksirei na hubainisha sehemu ya ndani ya moyo wako. Kwa kawaida daktari huweka katheta kwenye kila ateri ambayo inapeleka damu kwenye moyo wako (ateri za moyo) na hunyunyizia majimaji yenye kutofautisha ndani yake. Hio hubainisha sehemu ya ndani ya ateri hizo. Kipimo hiki kinaitwa angiografia ya moyo.

Kwa nini ninahitaji uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta?

Mara nyingi, madaktari hufanya uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta ili:

  • Kuona kana kwamba ateri zinazoingia kwenye moyo zimefungika

  • Kutibu ateri zilizofungika wanapozipata

Madaktari wanaweza kushuku una ateri zilizofungika moyoni mwako (ugonjwa wa ateri ya moyo) ikiwa:

Mara chache, unaweza kuhitaji uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta ili kuona kana kwamba una:

  • Kasoro ya kuzaliwa

  • Uvimbe moyoni mwako

  • Valvu ya moyo mbaya

  • Tatizo kwa mishipa kuu ya damu ambayo hutoka kwenye moyo wako

Uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta unafanywa vipi?

Uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta unafanyiwa katika kitengo maalum kwenye hospitali. Kwa kawaida unaweza kwenda nyumbani baada ya kipimo isipokuwa kama daktari anapata tatizo ambalo linahitaji kulazwa hospitalini.

  • Mrija mmoja au 2 itawekwa moja kwa moja kwenye mshipa (IVs) ili viowevu na dawa ziweze kuwekwa

  • Utashikizwa kwenye mashine ambazo zinafuatilia shinikizo la damu na moyo wako

  • Kipimo hicho kinafanywa wakati haujalala lakini kwa kawaida unapewa dawa kupitia kwenye mshipa ili kusaidia uhisi utulivujki

  • Kwanza daktari hudunga dawa ya kufanya ganzi ngozi iliyo juu ya ateri kwenye mkono au kinena chako

  • Wakati ngozi imefanywa ganzi, wanakata kidogo na kuingiza katheta

  • Wataelekeza katheta kupitia kwenye mishipa yako mikuu ya damu na kwenye moyo wako

  • Madaktari watadunga majimaji yenye kutofautisha kupitia kwenye katheta

  • Kitofautishaji kinatokea kwenye filamu za eksirei ambazo madaktari wanatazama kwenye skrini ya video

Daktari anaweza pia kutumia katheta pamoja na zana fulani kwenye kiishio kama vile:

  • Probu ya leza au upigaji wa picha kwa kutumia mawimbi ya sauti ili kuangalia au kuchukua picha za sehemu ya ndani ya mishipa ya damu

  • Zana za kukata ili kuchukua sampuli ndogo ya tishu ya moyo wako ili kuiangalia kwa kutumia hadubini (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi)

Baada ya kutumia katheta, utakuwa na vazi maalum ambalo linaweka shinikizo kwenye mkono au kinena chako ili kudhibiti kuvuja damu.

Matibabu wakati wa uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta

Wakati mwingine madaktari wanaweza pia kutibu moyo wako wakati wa uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta kwa:

  • Kukwambua ateri iliyozibwa (angioplasti)

  • Kufungua vali ya moyo iliyozibwa sehemu (valvuloplasty)

Wakati wa angioplasti, daktari huvimbisha puto ndogo kwenye kiishio cha katheta. Puto husukuma na kuzibua kizuizi. Mara nyingi daktari pia huweka mrija wenye wavu (stenti) katika kiishio cha katheta hadi kwenye sehemu iliyozibwa. Mrija wenye wavu husaidia kupanua sehemu iliyozibwa.

Wakati wa valvuloplasti, daktari huvimbisha puto kubwa zaidi ili kuzibua vali uliyozibwa.

Hata hivyo, matatizo mengine yanayopatikana wakati wa uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta yanahitaji upasuaji. Matatizo mengine yanweza kutibiwa kwa kutumia dawa.

Je, kuna athari mbaya zozote za uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta?

Kuna aina 3 za athari mbaya zinazotokana na uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta. Hizi zinajumuisha:

  • Majimaji yenye kutofautisha

  • Katheta kwenye moyo wako

  • Shimo lililotengenezwa na katheta kwenye ateri kwenye mkono au mguu wako

Majimaji yenye kutofautisha hufanya mwili wako uhisi wenye joto jingi yanapoingia. Baadhi ya watu huhisi wakiwa wagonjwa tumboni zao. Kwa nadra, unaweza kupata athari mbaya kama vile shinikizo la chini la damu, mmenyuko mkali wa mzio au kuharibika kwa figo.

Katheta iliyo moyoni mwako wakati mwingine huwasha misuli ya moyo na husababisha mdundo wa moyo usio wa kawaida. Mdundo wa moyo usio wa kawaida hukuwa hatari kwa nadra na huhitaji daktari kupea moyo wako mshtuko wa umeme (hii inaitwa difibrilesheni).

Kwa kawaida shimo lililo kwenye ateri yako lina maumivu madogo tu na hupona haraka. Hata hivyo, wakati mwingine huwa linaanza kuvuja damu au hupona kwa njia isiyo ya kawaida. Kwa nadra, ateri huzibwa ili damu isiingie kwenye mkono au mguu wako. Wakati mwingine utahitaji kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha matatizo haya.

Hatari ya matatizo mabaya inategemea sana:

  • Jinsi ulivyo na afya kwa jumla

  • Una miaka mingapi

  • Ugonjwa wa moyo wako ni mbaya kiasi gani

Kwa jumla, hatari yako ya kuwa na tatizo kubwa, kama vile shambulio la moyo au kiharusi au la kufariki kutokana na kipimo liko chini sana.

Daktari anaweza kujua nini kutokana na uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta?

  • Kana kwamba ateri zako ambazo zinapeleka damu kwenye misuli ya moyo (ateri za moyo) zimebanwa

  • Jinsi moyo wako unapiga damu

  • Kana kwamba valvu za moyo wako zimebanwa au zinavuja damu

  • Ikiwa una kasoro ya kuzaliwa au uvimbe kwenye moyo

  • Matibabu bora ni yapi kwa dalili zako