Moyo wako ni msuli unaosukuma damu kwenye mwili wako. Mapigo ya moyo wako ni jinsi moyo wako unavyodunda. Moyo wako unapaswa kuwa na mapigo ya mara kwa mara, yenye mdundo, kama jinsi saa inavyosonga.
Mdundo wa moyo usio wa kawaida ni nini?
Midundo ya moyo isiyo ya kawaida ni midundo ya moyo ambayo:
Si ya kawaida
Ni ya haraka zaidi (takakadia)
Ni ya polepole zaidi (bradikadia)
Midundo ya moyo isiyo ya kawaida pia inajulikana kama mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.
Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida yanayotokea sana hayasababishi dalili, hayana madhara na hayahitaji matibabu
Matatizo ya moyo ndiyo kisababishi cha kawaida sana cha mdundo wa moyo usio wa kawaida
Unaweza kuhisi kuwa vizuri, lakini wakati mwingine unaweza kuhisi mdundo wa moyo wako usio wa kawaida (kile unahisi kinaitwa mpapatiko wa moyo)
Baadhi ya midundo ya moyo isiyo ya kawaida hukufanya uhisi mdhaifu au kizunguzungu
Madaktari wanafanya elektrokadiogramu (ECG/EKG) ili kubaini mdundo wa moyo usio wa kawaida
Midundo ya moyo isiyo ya kawaida mingi si hatari na mingi inaweza kutibiwa
Baadhi ya midundo ya moyo isiyo ya kawaida ni hatari na inaweza kufisha
Ni nini hudhibiti mdundo wa moyo wangu?
Mdundo wa moyo wako unadhibitiwa na:
Seli za kudhibiti mapigo ya moyo kwenye moyo wako
Ubongo wako
Homoni, madini na vitu vingine kwenye damu yako
Kuna seli za kudhibiti mapigo ya moyo maalum kwenye sehemu ya moyo wako zinazoitwa kifundi cha SA (kifundo cha sinoatria).
Seli za kidhibiti mapigo ya moyo hutuma ishara za kawaida za umeme kwa misuli ya moyo wako ubane
Seli za kidhibiti mapigo ya moyo zina mdundo wao halisia wa mawimbi 60 hadi 100 kwa dakika. Hata hivyo, neva kutoka kwenye ubongo wako hutuma jumbe kwenye seli zikiziambia ziharakishe au zipunguze kasi.
Mfumo wa kuendesha moyo wako una vijisehemu vidogo vya tishu kama nyaya za umeme.
Mfumo wa upitishaji hubeba ishara za kidhibiti mapigo ya moyo kwenye sehemu zingine za moyo wako
Mfumo wa upitishaji unajumuisha njia inayoitwa nodi ya AV (nodi triskupidia). Nodi ya AV hudhibiti jinsi mawimbi hupita kutoka sehemu za juu za moyo wako (atiria) kwenda zile za chini (ventrikali). Wakati mfumo wa upitishaji unafanya kazi vizuri, ishara huingia kwenye kila seli ya misuli ya moyo wako kwa wakati tu ili moyo wako utoe mdundo mzuri, thabiti ambao unapiga damu vizuri.
Homoni, kama vile homoni ya dundumio zinazotengenezwa na tezi dundumio, zinaathiri mapigo ya moyo wako. Dawa na kemikali nyingi pia zinaathiri mapigo ya moyo wako.
Unahitaji pia msawazisho mzuri wa madini (elektroliti, kama vile sodiamu na potasiamu) kwenye damu yako ili moyo wako udunde vizuri.
Ni nini husababisha midundo ya moyo isiyo ya kawaida?
Mdundo wa moyo wako unaweza kuwa usio wa kawaida ikiwa kuna tatizo kwenye:
Seli za kidhibiti mapigo ya moyo zako
Mfumo wa upitishaji umeme wa moyo wako
Kemikali au dawa (mfano, pombe, kafeini) kwenye damu yako
Kisababishaji cha kawaida zaidi cha tatizo la mdundo wa moyo ni tatizo la moyo, kama vile:
Matatizo ya vali ya moyo kama vile stenosis ya aota
Ugonjwa wa ateri ya moyo huzuia mtiririko wa damu kwenye sehemu za moyo wako. Hii inaweza kuharibu seli za kidhibiti mapigo ya moyo au mfumo wa upitishaji.
Visababishaji vingine vya midundo ya moyo isiyo ya kawaida inajumuisha:
Dawa
Mambo yasiyo ya kawaida uliyozaliwa nayo
Wakati mwingine madaktari hawawezi kujua ni nini inasababisha mdundo wa moyo wako usio wa kawaida.
Ni zipi dalili za mdundo wa moyo usio wa kawaida?
Dalili zako zinategemea sana kana kwamba moyo wako:
Unapiga damu ya kutosha
Haupigi damu ya kutosha
Ikiwa moyo wako unapiga damu ya kutosha, unaweza kuhisi kawaida. Au unaweza kuhisi kama moyo wako unaruka midundo (inaitwa mpapatiko wa moyo). Baadhi ya watu wanasema mipapatiko thabiti inaweza kuhisi kama samaki ikipapatika karibu na kifua chao.
Ikiwa moyo wako haupigi damu ya kutosha, pia unaweza kuwa na:
Udhaifu
Matatizo katika kufanya mazoezi
Kuishiwa na pumzi
Kuhisi kichwa chepesi au kizunguzungu
Maumivu ya kifua
Kuzirai
Nenda kwa daktari ikiwa una yoyote ya dalili hizi.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina mdundo wa moyo usio wa kawaida?
Daktari huhisi mapigo yako na kufanya:
ECG ni kipimo cha haraka, kisicho na uchungu ambacho hupima mawimbi ya umeme ya moyo kwa kutumia vibandiko na nyaya kwenye kifua, mikono na miguu.
Ikiwa ECG inaonyesha mdundo usio wa kawaida, kwa kawaida madaktari hufanya vipimo vingine kulingana na dalili zako, ikijumuisha:
Vipimo vya damu kubaini viwango vya homoni na elektroliti
Ekokadiogramu (kupiga moyo picha kwa kutumia mawimbi ya sauti)
Ikiwa ECG haionyeshi kitu kisicho cha kawaida, inaweza kuwa ni kwa sababu mdundo wa moyo wako haukuwa wa kawaida wakati ulikuwa unafanyiwa kipimo. Kisha madaktari wanaweza kukwambia:
Uvae kifaa kidogo chini ya mavazi yako ambacho kinarekodi shughuli ya umeme ya moyo wako kwa siku moja au zaidi (kifuatiliaji tukio au kifuatiliaji Holter)
Ikiwa madaktari wanafikiria kuwa una tatizo hatari la moyo, watakulaza hospitalini. Utakuwa kwenye kitengo ambapo kipimo cha mapigo ya moyo na mdundo wako unaweza kurekodiwa na kuonekana na wauguzi na madaktari.
Ikiwa madaktari wanahitaji maelezo zaidi kuhusu mdundo wa moyo wako usio wa kawaida, wanaweza kufanya:
Kipimo cha elektrofisiolojia ni kama uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta. Daktari huingiza mrija mwembamba unaoweza kupinda (katheta) ndani ya mshipa mkubwa wa damu (kwa mfano, ule ulio kwenye mguu wako) na kuuunganisha hadi kwa moyo wako. Katheta ina elektrodi kwenye ncha yake ambayo hurekodi mawimbi ya umeme ya moyo wako kutoka ndani. Katheta pia inaweza kutuma mawimbi ya umeme kwa moyo wako kuona mapigo yake.
Madaktari hutibu aje midundo ya moyo isiyo ya kawaida?
Baadhi ya midundo ya moyo isiyo ya kawaida haina madhara na haihitaji matibabu.
Wakati mwingine, mabadiliko ya mtindo wa maisha yanasaidia, kama vile:
Kubadilisha au kusitisha mojawapo ya dawa zako
Kutokunywa pombe au kafeini
Kutovuta sigara
Kutofanya mazoezi magumu (mdundo wa moyo usio wa kawaida ukifanyika wakati wa mazoezi)
Midundo tofauti isiyo ya kawaida inahitaji matibabu tofauti. Madaktari wanaweza kutumia:
Dawa
Kidhibiti cha mapigo ya moyo bandia (kifaa kidogo cha umeme ambacho madaktari huweka kwenye kifua au tumbo yako ili kuonyesha moyo wako wakati wa kudunda)
Mshtuko wa umeme ili kurejesha mdundo wa moyo wa kawaida (unaoitwa kurekebisha mapigo ya moyo, difibrilesheni au kurekebisha elektriki)
Matibabu yanayoitwa ya kuondoa tishu ili kuharibu tishu ya moyo isiyo ya kawaida
Vidhibiti mapigo ya moyo bandia wakati mwingine vinajumuisha defaibrileta ili kifaa hicho sawa kinaweza kuchochea mpigo wa moyo wa kawaida au kusitisha mdundo usio wa kawaida kwa mshtuko. Kifaa hiki cha muunganisha kinaitwa ICD (defaibrileta ya kupandikiza kwenye moyo).
Madaktari huondoa tishu iwapo watagundua kuwa sehemu ndogo zaidi ya tishu ya moyo inasababisha mapigo yasiyo ya kawaida. Kutoa tishu mara nyingi humaliza tatizo la mdundo. Mara nyingi wanaondoa tishu wakati wa kipimo cha elektrofisiolojia. Wanatumia katheta ili kuleta mkondo wa umeme wa marudio ya juu ambao huharibu sehemu ndogo ya moyo.
Unaweza kuhitaji kuacha kuendesha gari kwa muda hadi madaktari wajue kana kwamba matibabu yanafanya kazi.