Vizuizi vya Moyo

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2024

Moyo wako ni msuli unaosukuma damu kwenye mwili wako. Mapigo ya moyo wako ni jinsi moyo wako unavyodunda. Moyo wako unapaswa kuwa na mapigo ya mara kwa mara, yenye mdundo, kama jinsi saa inavyosonga.

Moyo wako una sehemu nne. Atiria ni chemba mbili za juu kwenye moyo wako. Ventrikali ni chemba mbili za chini kwenye moyo wako. Atiria husukuma damu kwenye ventrikali. Ventrikali husukuma damu kwenye mapafu na mwili wote (rejelea pia Bayolojia ya Moyo).

Seli maalum za jozi zinazopatikana kwenye sehemu ya atiria iitwayo fundo la SA (fundo la sinasi) hutuma mawimbi ya umeme kwenye misuli ya moyo wako ili kuifanya ibane.

Mfumo wa kuendesha moyo wako una vijisehemu vidogo vya tishu kama nyaya za umeme. Mfumo wa upitishaji hubeba ishara za kidhibiti mapigo ya moyo kutoka kwenye nodi ya SA hadi kwenye sehemu zingine za moyo wako. Sharti mawimbi yafike kwenye seli zote za misuli ya moyo kwa wakati ufaao ili moyo wako upige inavyofaa sukuma damu.

Kizuizi cha moyo ni nini?

Kizuizi cha moyo ni kuchelewa au kizuizi katika mfumo wa upitishaji wa moyo wako ambacho kinasababisha mdundo wa moyo usio wa kawaida. Kuna aina nyingi tofauti za kizuizi cha moyo.

  • Baadhi ya aina za kizuizi cha moyo hazisababishi dalili

  • Aina zingine za kizuizi cha moyo hukupatia kipimo cha mapigo ya moyo ya kasi ya chini ambayo hukufanya uhisi uchovu na kizunguzungu na zinaweza kusababisha uzirai

  • Madaktari wanabaini kizuizi cha moyo kwa kutumia elektrokadiogramu (ECG/EKG)

  • Watu walio na aina fulani ya kizuizi cha moyo wanahitaji kidhibiti mapigo ya moyo

Je, ni nini husababisha kizuizi cha moyo?

Mfumo wa upitishaji wa moyo wako hubeba ishara za umeme kutoka kwenye atriamu kupitia kwenye njia inayoitwa nodi ya AV (nodi triskupidia). Nodi ya AV hudhibiti jinsi mawimbi hupita kutoka sehemu za juu za moyo wako (atiria) kwenda zile za chini (ventrikali). Kutoka kwenye nodi ya AV, ishara hupitia kwenye vifungu kadhaa vya ufumwele (matawi ya vifungu) kabla zienezwe kupitia kwenye ventrikali zako. Kizuizi cha moyo kinaweza kutokea katika sehemu yoyote ya mfumo wa upitishaji.

Baadhi ya watu wanazaliwa wakiwa na kizuizi cha moyo. Watu wengine wanapata kizuizi cha moyo baadaye kwenye maisha. Vizuizi vya moyo vinaweza kusababishwa na uharibifu kutokana na:

Aina za kizuizi cha moyo ni zipi?

Madaktari hupanga vizuizi vya moyo kulingana na sehemu ya upitishaji ambayo imehusishwa na jinsi ambayo ni kali.

Maeneo 2 makuu ya kizuizi cha moyo ni:

  • Kizuizi cha triskupidia (AV)

  • Kizuizi cha tawi la kifungu

Kizuizi cha triskupidia (AV) ni nini?

Kizuizi cha AV hutokea katika au karibu na nodi ya AV. Vizuizi vya AV vina daraja 3, kulingana na jinsi ambavyo ni kali:

  • Daraja ya 1: Kila msukumo wa umeme hupunguza kasi tu kwa sehemu ya sekunde kwa vile unapitia kwenye moyo wako (kipimo cha mapigo ya moyo wako ni ya kawaida)

  • Daraja ya 2: Baadhi ya ishara hazipiti kwenye nodi ya AV na moyo wako huruka midundo ingine

  • Daraja ya 3: Hakuna ishara zinapita kwenye nodi ya AV na moyo wako unaweza kusita au kudunda polepole kupita kiasi ambayo ni hatari

Kizuizi cha tawi la kifungu ni nini?

Kizuizi cha tawi la kifungu hutokea kwenye vifungu vya ufumwele vya mfumo wa upitishaji kwenye ventrikali zako. Kuna tawi la kifungu la kushoto na tawi la kifungu la kulia. Kizuizi cha tawi la kifungu la kushoto kwa sana huwa sugu zaidi kwa sababu kwa kawaida kinasababishwa na ugonjwa wa moyo wa muda mrefu.

Dalili za kizuizi cha moyo ni zipi?

Vizuizi zaidi vya moyo havisababishi dalili. Ikiwa una kizuizi cha moyo sugu, unaweza kuhisi uchovu na kizunguzungu na unaweza kuzirai.

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nina kizuizi cha moyo?

Daktari huhisi mapigo yako na kufanya:

ECG ni kipimo cha haraka, kisicho na uchungu ambacho hupima mawimbi ya umeme ya moyo kwa kutumia vibandiko na nyaya kwenye kifua, mikono na miguu.

Je, madaktari wanatibu vipi kizuizi cha moyo?

Aina nyingi za kizuizi cha moyo hazihitaji matibabu. Lakini unaweza kuhitaji matibabu ya ugonjwa wa moyo ambao ulisababisha kizuizi cha moyo wako.

Hata hivyo, ikiwa una kizuizi cha moyo cha AV cha daraja la 2 au la 3, unaweza kuhitaji kidhibiti mapigo ya moyo. Kidhibiti cha mapigo ya moyo ni kifaa kidogo cha umeme ambacho madaktari huweka kwenye kifua au tumbo yako ili kutoa ishara ya wakati wa kudunda kwa moyo wako.