Mshtuko wa Takadia ya Ventrikali ya Juu ya Moyo (SVT, PSVT)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Moyo wako ni msuli unaosukuma damu kwenye mwili wako. Mapigo ya moyo wako ni jinsi moyo wako unavyodunda. Moyo wako unapaswa kuwa na mapigo ya mara kwa mara, yenye mdundo, kama jinsi saa inavyosonga.

Moyo wako una sehemu nne. Atiria ni sehemu mbili za juu. Ventrikali ni sehemu mbili za chini. Atiria husukuma damu kwenye ventrikali. Ventrikali husukuma damu kwenye mapafu na mwili wote (rejelea pia Bayolojia ya Moyo).

Seli maalum za jozi zinazopatikana kwenye sehemu ya atiria iitwayo fundo la SA (fundo la sinasi) hutuma mawimbi ya umeme kwenye misuli ya moyo wako ili kuifanya ibane.

Mfumo wa kuendesha moyo wako una vijisehemu vidogo vya tishu kama nyaya za umeme. Mfumo wa uendeshaji hubeba mawimbi ya seli za jozi kwenye moyo wako wote. Sharti mawimbi yafike kwenye seli zote za misuli ya moyo kwa wakati ufaao ili moyo wako upige inavyofaa sukuma damu.

mshtuko wa ventrikali za juu za moyo (SVT, PSVT) ni nini?

SVT ni aina ya mdundo wa moyo usio wa kawaida. Katika SVT, kipimo cha mapigo ya moyo wako kwa ghafla huenda haraka zaidi na kisha kurejea kawaida.

  • STV ni ya kawaida lakini kipimo cha mapigo ya moyo ya haraka ambayo huanzia na kuisha kwa ghafla

  • Unaweza kuhisi moyo wako ukienda mbio au kugonga kwa nguvu, shida ya kupumua na kuwa na maumivu ya kifua

  • SVT inafanya usihisi vizuri lakini kwa kawaida si hatari

  • Hutokea kwa sana kwa watu wenye umri mdogo na katika mazoezi makali

  • Madaktari wanaweza kukupa dawa ili kusitisha kipindi hicho

Je, nini husababisha SVT?

Kwa kawaida SVT inasababishwa na kutokuwa kawaida kwa mfumo wa upitishaji wa moyo wako. Katika SVT, ishara za umeme zinazuiwa kwenye mzunguko ambao huenda kwa mviringo. Ishara zinazozunguka hufanya moyo udunde kwa kawaida lakini kwa kasi ya juu, takriban mara 160 hadi 220 kwa kila dakika. Katika SVT, ishara zinazozunguka ziko juu ya ventrikali. Katika takakadia ya ventrikali, mdundo usio wa kawaida unasababishwa na tatizo kwenye ventrikali zako.

Mara nyingi wakati una SVT, kipimo cha mapigo ya moyo na mdundo wako ni wa kawaida. Kisha kwa ghafla mdundo wa moyo wa mapema huchochea mzunguko wa umeme usio wa kawaida. Pindi inapochochewa, mzunguko huu wa umeme usio wa kawaida husababisha moyo kudunda haraka zaidi. Kwa ghafla hivyo, moyo hurejea katika mapigo na mdundo wake wa kawaida.

Je, dalili za SVT ni zipi?

Kwa kawaida kipimo cha mapigo ya moyo ya haraka huanzia na kuisha kwa ghafla. Inaweza kudumu dakika chache hadi saa nyingi. Huenda ukahisi:

  • Midundo ya moyo inayogonga au kukimbia

  • Udhaifu

  • Wepesi wa kichwa

  • Kuishiwa na pumzi

  • Maumivu ya kifua

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina SVT?

Daktari huhisi mapigo yako na kufanya:

ECG ni kipimo cha haraka, kisicho na uchungu ambacho hupima mawimbi ya umeme ya moyo kwa kutumia vibandiko na nyaya kwenye kifua, mikono na miguu.

Je, madaktari hutibu vipi SVT?

Ili kupunguza mapigo ya moyo wako, daktari wako huenda akakuomba ujaribu mojawapo ya yafuatayo:

  • Kulazimisha kama vile unapata tabu kujisaidia

  • Sugua shingo yako chini ya taya yako

  • Weka uso wako kwenye bakuli la maji ya barafu

Pata msaada wa kimatibabu ikiwa:

  • Hauwezi kupunguza kasi ya kipimo cha mapigo ya moyo

  • Una dalili kali zaidi

  • Kipimo cha mapigo ya moyo wako cha haraka kinadumu zaidi ya dakika 20

Kwa kawaida madaktari wanaweza kupunguza kasi ya kipimo cha mapigo ya moyo wako kwa upesi kwa kukupea dawa moja kwa moja kwenye mshipa wako (dawa ya IV).

Je, nini maana ya matibabu ya kuondoa tishu?

Ikiwa unapata dalili kali mara kwa mara, madaktari wanaweza kukupendekezea ufanyiwe utaratibu wa uondoaji wa tishu. Uondoaji tishu ni matibabu ya kuharibu tishu ya moyo isiyo ya kawaida.

Daktari kwanza hufanya upimaji wa kieletrofiziolojia, ambao ni sawa na kuingiza katheta kwenye moyo. Daktari huingiza mrija mwembamba unaoweza kupinda (katheta) ndani ya mshipa mkubwa wa damu (kwa mfano, kwenye mguu wako) na kuuunganisha hadi kwa moyo wako. Katheta ina elektrodi kwenye ncha yake ambayo hurekodi mawimbi ya umeme ya moyo wako kutoka ndani. Katheta pia inaweza kutuma mawimbi ya umeme kwa moyo wako kuona mapigo yake.

Ikiwa kipimo kinaonyesha kuwa sehemu ndogo zaidi ya tishu ya moyo inasababisha SVT, kutoa tishu mara nyingi hurekebisha tatizo la mdundo. Madaktari hutumia katheta inayotoa mkondo wa umeme wa masafa ya juu ili kuharibu tishu zinazosababisha tatizo.

Ikiwa kuondoa kwa kufyonza kwa katheta hakufai, madaktari wanaweza kukutibu kwa dawa ili kuzuia mapigo ya moyo ya haraka kurejea.