Biolojia ya Moyo

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024
Nyenzo za Mada

Je, moyo ni nini?

Moyo ni kiungo chenye uwazi kilichoundwa kwa misuli. Moyo na mishipa ya damu ni sehemu ya mfumo wa moyo na mishipa.

  • Moyo wako husukuma damu kupitia mishapa yako ya damu

  • Damu hubeba oksijeni na virutubishi hadi sehemu zote za mwili wako

  • Moyo wako unapaswa kudunda bila kuacha maisha yako yote na usipumzike kamwe

Kila dakika, moyo wako hudunda mara 70 na kusukuma kiasi cha galoni 1 (lita 4) za damu. Moyo wako hudunda kwa nguvu na kusukuma kwa nguvu wakati ukifanya mazoezi, wakati mwili wako unapohitaji oksijeni zaidi. Unapokagua mapigo yako, unapima kipimo cha mapigo yako ya moyo, au idadi ya mapigo kwa dakika.

Damu inayosafiri mwilini mwako hupeleka oksijeni na virutubishi kwa tishu na viungo vyako. Uchafu kutoka kwenye tishu na viungo hivyo hubebwa na damu hadi kwenye mapafu na figo ili viondolewe mwilini.

Je, moyo hufanyaje kazi?

Moyo ni pampu ya damu. Ni pampu 2 zilizounganishwa—moja ipo upande wa kushoto wa moyo na nyingine upande wa kulia.

  • Pampu ya upande wa kulia hupokea damu kutoka kwenye mwili wako na kuisukuma kwenye mapafu yako ambapo hubeba damu

  • Pampu ya upande wa kulia hupokea damu iliyojaa oksijeni kutoka kwenye mapafu na kuisukuma mwilini kote

Ili, kusukuma damu, moyo wako una:

  • Nafasi nne tupu (chemba) kwa ajli ya mtiririko wa damu

  • Vali nne za moyo ili kuhakikisha damu inatiririka katika uelekeo sahihi

  • Mfumo wa umeme wa kuijulisha misuli ya moyo wakati wa kukaza

  • Mishipa ya damu kwa ajili ya kulisha misuli ya moyo wenyewe

A Look Into the Heart

This cross-sectional view of the heart shows the direction of normal blood flow.

Chemba za moyo ni nini?

Moyo una vyumba 4 (chemba), viwili upande wa kulia na viwili upande wa kushoto. Chemba za moyo wako hulegea, kujaa damu na kukaza ili kusukuma damu itoke.

  • Chemba mbili za juu (atriamu ya kulia na atriamu ya kushoto) huruhusu damu kuingia kwenye moyo

  • Chemba mbili za chini (ventrikali ya kulia na kushoto) husukuma damu nje

Vali za moyo zina kazi gani?

Moyo wako una vali 4 ambazo hudhibiti mtiririko wa damu. Vali hufunguka kuruhusu damu itoke kwenye chemba moja na kuingia chemba inayofuata au kwenye mshipa wa damu. Vali hufunga ili kuzuia damu isirudi nyuma hadi kwenye chemba isiyo sahihi.

Ukiweka kichwa chako juu ya kifua cha mtu na kusikiliza mapigo yake ya moyo, unasikia sauti za vali za moyo zikifunguka na kufunga.

Mfumo wa umeme wa moyo ni nini?

Moyo wako unapaswa kuwa na mapigo ya mara kwa mara, yenye mdundo, kama jinsi saa inavyosonga:

  • Mdundo wa moyo wako unadhibitiwa na seli za kidhibiti mapigo ya moyo kwenye moyo wako

  • Seli za kidhibiti mapigo ya moyo hutuma ishara za kawaida za umeme kwa misuli ya moyo wako ubane

  • Ishara hupitishwa kwenye tishu zinazoitwa mfumo wa kuendesha moyo

Kuna seli maalum za kidhibiti mapigo ya moyo kwenye sehemu ya moyo wako inayoitwa kifundo cha SA. Seli za kidhibiti mapigo ya moyo zina mdundo wao halisia wa mawimbi 60 hadi 100 kwa dakika. Neva kwenye ubongo wako hutuma ujumbe kwa seli zikizielekeza kuongeza au kupunguza kasi.

Mfumo wa kuendesha moyo wako una vipande vidogo vya tishu vinavyofanana na nyaya za umeme. Mfumo wa uendeshaji hubeba mawimbi ya seli za jozi kwenye moyo wako wote. Mfumo wa kuendesha moyo wako hujumuisha lango kuu linaloitwa kifundo cha AV. Nodi ya AV hudhibiti jinsi mawimbi hupita kutoka sehemu za juu za moyo wako (atiria) kwenda zile za chini (ventrikali). Mfumo wa kuendesha moyo wako unapokuwa unafanya kazi vizuri, ishara hufikia kila seli za misuli ya moyo wako kwa wakati sahihi. Moyo wako kisha hutoa pigo zuri, thabiti ambalo husukuma damu vizuri.

Kwanini moyo unahitaji mishipa ya damu?

Kama ilivyo kwa misuli yote, moyo unahitaji damu ya kutosha ili kufanya kazi. Unaweza kufikiri kwamba, kwa sababu moyo umejaa damu, hauhitaji usambazaji wa damu unaojitegemea. Hata hivyo, damu inayosukumwa kupitia moyo hailishi misuli ya moyo. Badala yake misuli ya moyo inalishwa na mishipa yake ya damu.

  • Mishipa ya damu ya moyo inaitwa ateri za moyo

Koronari ni neno linalomaanisha moyo.

Moyo unaweza kupata hitilafu gani?

Unaweza kupata tatizo la sehemu yoyote ya moyo: