Angina ni nini?

Angina ni maumivu, hisia ya usumbufu, au shinikizo kwenye kifua chako linalotokea wakati moyo wako haupati oksijeni ya kutosha. Ukosefu wa oksijeni husababishwa na ateri za moyo kubanwa au kuzibika (ugonjwa wa ateri za moyo). Angina mara nyingi huwa ni ishara ya tahadhari ya shambulio la moyo.

Kusambazia Moyo Damu

Sawa na tishu nyingine yoyote mwilini, msuli wa moyo sharti upokee damu yenye oksijeni, na uchafu uchujwe kupitia damu. Ateri ya kulia na ya kushoto, ambayo hutoka kwenye aota nje ya moyo, huingiza damu yenye oksijeni kwenye moyo. Ateri ya kulia hugawanyika kuwa ateri ya kando na ateri ya nyuma upande wa chini, iliyopo kwenye sehemu ya nyuma ya moyo. Ateri ya kushoto (inayojulikana kwa kawaida ateri kuu ya moyo ya kushoto) hugawanyika kuwa ateri inayozunguka moyo na ateri ya kushoto inayoshuka upande wa mbele. Mishipa ya moyo hubeba damu iliyo na uchafu kutoka kwenye misuli ya moyo na kuielekeza kwenye mshipa mkubwa ulio sehemu ya nyuma ya moyo unaoitwa sanasi ya moyo, ambayo hurejesha damu kwenye ateri ya kulia.

Je, nini husababisha angina?

Kisababishi cha angina kilichozoeleka sana ni wembamba wa ateri zinazobeba damu kwenda kwenye moyo wako (ateri za moyo) Hali hiyo ya wembamba mara nyingi husababishwa na atherosklerosisi, ambao mara nyingi huitwa kugandamana kwa ateri Utando wa mafuta hurundika na kuziba ateri zako taratibu na kupunguza au kuzuia kabisa mtiririko wa damu. Musuli wa moyo wako usipopata damu ya kutosha, hali hiyo husababisha maumivu.

Angina inaweza pia kusababishwa na mkazo wa ateri ya moyo, ubanaji wa ghafla wa ateri. Dawa fulani haramu kama vile kokeni zinaweza kusababisha mkazo.

Anemia sugu (kiwango cha chini cha damu) huongeza hatari ya kupata angina. Ukiwa na anemia, unakuwa na seli zilizopungua za kubeba oksijeni.

Atherosklerosisi
Mshipa wa Damu wa Kawaida na Mshipa wa Damu Uliozibika Kiasi
Mshipa wa Damu wa Kawaida na Mshipa wa Damu Uliozibika Kiasi

In people with atherosclerosis, patchy deposits of fatty material (atheromas or atherosclerotic plaques) develop in the walls of medium-sized and large arteries, leading to reduced or blocked blood flow.

... soma zaidi
Utando Kwenye Mishipa ya Damu
Utando Kwenye Mishipa ya Damu

This photo shows an atherosclerotic plaque (atheroma; see arrow) visible in an artery.

BSIP VEM/SCIENCE PHOTO LIBRARY

Mashapo ya Mafuta kwenye Mshipa wa Moyo
Mashapo ya Mafuta kwenye Mshipa wa Moyo
Kwa kawaida, mishipa ya moyo hubeba damu yenye oksijeni hadi kwenye moyo. Kwa ugonjwa wa mishipa inayosambaza oksijeni ... soma zaidi

Je, ni zipi dalili za angina?

Huenda ukahisi:

  • Kuhisi hali isiyo nzuri, shinikizo, au maumivu kwenye sehemu ya katikati ya kifua

  • Maumivu hayo yanaweza kusambaa kwenye bega, mkono, au kwenye koo, taya au meno yako

Angina kawaida huja unapofanya mazoezi mazito, kwa mfano, kwa kupanda ngazi au kupanda kilima. Hupotea baada ya dakika chache ukipumzika. Kawaida, unapata angina kila wakati unapofanya kiasi kile kile cha juhudi. Kwa mfano, unaweza kupata angina kila mara unapopanda kilima fulani. Kadiri ateri zako za moyo zinavyokuwa nyembamba, utapata angina bila hata kutumia nguvu nyingi. Kwa mfano, ikiwa ulipata angina yako ya kwanza kwa kupanda makundi 2 ya ngazi, baadaye unaweza kuipata kwa kupanda kundi 1 tu la ngazi.

Angina ambayo huja bila kutumia nguvu yoyote au inayozidi kwa haraka sana ni:

Angina isiyo thabiti ni tahadhari kwamba huenda unakaribia kupata mshtuko wa moyo.

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nini angina?

Ikiwa una dalili zinazoashiria angina, madaktari watafanya vipimo, kama vile:

  • Kipimo cha shinikizo—kipimo cha kubaini ikiwa moyo wako unapata damu ya kutosha unapofanya kazi nzito (ukihitaji kusukuma damu upesi), kama vile unapofanya mazoezi

  • ECG/EKG—kipimo kinachopima shughuli za umeme za moyo wako, ambazo zinaweza kuwa si za kawaida ukiwa na ugonjwa wa ateri za moyo

  • Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta)—kipimo cha picha cha kuchunguza kugandamana kwa ateri za moyo

Ikiwa angina yako imekithiri au inazidi, madaktari wanaweza kufanya:

Katika uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa kutumia katheta, madaktari huweka katheta ndefu nyembamba (tyubu ndogo inayopindika) kwenye ateri ya mkono au mguu wako, kuelekea kwenye moyo wako na ndani ya kila ateri yako ya moyo kisha wanadunga dutu ya kutofautisha inayoonekana kwenye eksirei.

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa angina?

Madaktari watakupatia matibabu ya:

  • Wakati unapopata angina

  • Kuzuia angina

  • Tatizo linalosababisha angina

Ukipata angina, madaktari watakuelekeza umeze:

  • Tembe za nitroglycerin tablets au unyunyizie chini ya ulimi wako

Nitroglycerin inapaswa kufanya kazi kwa dakika chache.

Ili kuzuia angina, madaktari wanaweza kukupatia:

  • Tembe za nitroglycerin au viraka vya ngozi vinavyofanya kazi kwa muda mrefu

  • Dawa za kuzuia moyo wako usifanye kazi kwa bidii sana

Ili kutibu tatizo linalosababisha angina yako, kwa kawaida madaktari hukupatia:

Daktari pia atakuruhusu ubadili tabia zozote zinazoumiza moyo wako, kama vile kuvuta sigara, kutofanya mazoezi, na kutokula lishe bora.

Kulingana na kiasi cha kugandamana kwa ateri zako za moyo, huenda daktari akafanya upasuaji kukwamua ateri yako. Wanaweza kufanya upasuaji wa kufungua mshipa au kuunda mkondo mpya wa damu (pia inajulikana kama kupandikizwa kwa ateri ya moyo au kupachikwa kwa ateri ya moyo).

Wakati wa upasuaji wa kufungua mshipa:

  • Daktari hutia mrija mwembamba, unaoweza kupinda (katheta) kwenye mshipa wa sehemu ya juu ya mguu wako (kinena) au kwenye kifundo cha mkono

  • Katheta inasukumwa ndani kwenye ateri hadi kwenye moyo wako kisha kwenye moja ya ateri za moyo

  • Puto ndogo kwenye ncha ya katheta inatiwa hewa

  • Puto husukuma na kuzibua mshipa

  • Kisha daktari anatia mrija wenye wavu (kipanuzi) mwisho wa katheta na kuisogeza sehemu iliyozibwa.

  • Mrija wenye wavu husaidia kupanua sehemu iliyozibwa

Wakati wa upasuaji wa kupandikiza mshipa:

  • Daktari huchukua kipande cha ateri au mshipa usio na tatizo kutoka sehemu nyingine ya mwili wako

  • Anapandikiza ncha moja ya kipande hicho cha ateri au mshipa kwenye aota yako (mshipa mkuu unaobeba damu kutoka kwenye moyo hadi sehemu nyingine zote za mwili)

  • Anapachika upande wa pili wa ateri yako iliyoziba bila kupitia sehemu hiyo

  • Kisha damu yako inatiririka kupitia mkondo huu mpya, bila kizuizi

Kutibu angina
Kipanuzi cha Kufungua Mshipa wa Damu
Kipanuzi cha Kufungua Mshipa wa Damu
Upasuaji wa kufungua mshipa
Upasuaji wa kufungua mshipa
Moyo ni msuli unaopiga na kusukuma damu kwenye mwili wote. Ateri za moyo husambazia moyo wenyewe oksijeni na virutubish... soma zaidi
Upandikizaji wa Mishipa ya Moyo (CABG)
Upandikizaji wa Mishipa ya Moyo (CABG)

In coronary artery bypass grafting (CABG), doctors take an artery or vein from another part of the body to connect the aorta (the major artery that takes blood from the heart to the rest of the body) to a coronary artery past the point of its blockage. Blood flow is thus rerouted, skipping over (bypassing) the narrowed or blocked area.

... soma zaidi