Muhtasari kuhusu Anemia

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2024

Anemia ni nini?

Anemia ni kutokuwa na seli nyekundu za damu za kutosha au hemoglobini. Seli nyekundu za damu hubeba oksijeni kutoka kwenye mapafu yako kwenda kwenye ogani zako zote. Hemoglobini ni dutu iliyo ndani ya seli nyekundu za damu ambazo ndizo zinabeba oksijeni.

  • Unapokuwa na seli nyekundu za damu chache au hemoglobini kidogo sana, damu yako haiwezi kuchukua oksijeni ambayo mwili wako unahitaji

  • Anemia husababisha uchovu na udhaifu

  • Kuna sababu nyingi za anemia

  • Ni muhimu kupima anemia kadiri unavyokuwa na umri mkubwa kwa sababu unaweza kufupisha maisha yako

Ni nini husababisha anemia?

Sababu za anemia ni pamoja na:

  • Kupoteza damu nyingi sana kwa sababu ya jeraha, kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi, au matatizo ya njia ya umeng'enyaji au mkojo (kuvuja damu sugu)

  • Kutotengeneza seli nyekundu za damu za kutosha kwa sababu mwili wako unapungukiwa madini chuma, vitamini B12, au folate, au kwa sababu una lukemia au saratani nyingineyo

  • Mwili wako kuharibu seli nyekundu za damu nyingi sana

Je, dalili za anemia ni zipi?

Dalili zinategemea ni jinsi gani ugonjwa wako wa anemia ni mkubwa kiasi gani.

Anemia ndogo inasababisha:

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Ngozi kuonekana hafifu

Anemia kubwa inasababisha:

  • Kujisikia kuzimina na kizunguzungu

  • Kuhisi kiu

  • Kutokwa jasho

  • Dhaifu, mapigo ya moyo ya haraka

  • Misuli ya miguu kukaza wakati wa mazoezi

  • Kuishiwa na pumzi

  • Maumivu ya kifua

Madaktari wanajuaje kuwa nina anemia?

Madaktari hufanya kipimo cha damu ili kupima viwango vyako vya hemoglobini na seli nyekundu za damu. Wanaweza kufanya vipimo vingine ili kujua sababu ya anemia.

Je, madaktari wanatibu vipi anemia?

Ikiwa tatizo la afya linasababisha wewe kuwa na anemia, madaktari wanatibu tatizo hilo la afya. Tiba inategemea aina ya anemia uliyonayo. Madaktari wanaweza kutibu anemia kwa kutumia:

  • Virutubisho vya madini chuma, vikitumiwa kama vidonge au IV (mojaa kwa moja kwenye mishipa yako)

  • Virutubisho vingine, kama vile vitamini B12 au folate

  • Kuongeza damu ya seli nyekundu za damu, kwa anemia mbaya

  • Dawa zinazosababisha mwili wako kutengeneza seli nyekundu za damu zaidi