Hali Isiyo ya Kawaida ya Uterasi Kuvuja Damu (AUB)

(Hali Isiyo ya Kawaida ya Uterasi Kuvuja Damu)

Imepitiwa/Imerekebishwa Nov 2023

Je, hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu ni nini?

Uterasi yako (mfuko wa uzazi) kwa kawaida huvuja damu wakati wa hedhi yako ya kila mwezi. Hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu ni hali ya kuvuja damu ambayo ni tofauti na vipindi vyako vya kawaida vya hedhi.

  • Unaweza kuvuja damu kati ya vipindi vya hedhi, kipindi ambacho hudumu kwa muda mrefu kuliko kawaida, kuvuja damu nyingi wakati wa hedhi, au kuvuja damu baada ya kuacha kupata hedhi

  • Hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu husababishwa na matatizo ya viwango vya homoni za kike za estrojeni na projesteroni

  • Ni nadra sana, hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu kusababishwa na uvimbe kwenye uterasi, ikijumuisha fibroidi na saratani

  • Hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu hutokea zaidi miongoni mwa vijana (ambao wameanza kupata hedhi) na wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 45 (ambao wanakaribia ukomo wa hedhi)

  • Madaktari wanaweza kukupa homoni au dawa nyingine ili kudhibiti kuvuja damu kwako

Je, ni nini husababisha hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu?

Hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu mara nyingi husababishwa na matatizo ya viwango vya homoni zako za kike. Hii inaweza kutokea:

Maradhi ya tezi dundumio na matatizo ya tezi ya pituitari pia yanaweza kuathiri homoni zako za kike na kusababisha kuvuja damu.

Wakati mwingine, kuvuja damu kwenye kizazi kusiko kawaida husababishwa na uvimbe ndani au karibu na uterasi yako, kama vile:

Je, dalili za hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu ni zipi?

Kwa wanawake walio na hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu, kuvuja damu kunaweza kutofautiana na vipindi vya kawaida vya hedhi kwa njia zifuatazo:

  • Hutokea mara nyingi zaidi (tofauti ya chini ya siku 24)

  • Inatofautiana kwa idadi ya siku inayodumu

  • Inadumu zaidi ya siku 8

  • Hutokea kati ya hedhi au haitokei mara kwa mara

  • Inahusisha upotezaji wa damu nyingi sana

Kupoteza damu nyingi kunaweza kupelekea kuwepo kwa kiwango cha chini cha damu (anemia), jambo ambalo linaweza kusababisha ujihisi dhaifu na kuchoka.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu?

Madaktari kwa kawaida hufanya vipimo ili kutafuta maradhi ambayo yanaweza kuwa yanasababisha kuvuja damu kwako, na ni pamoja na:

  • Vipimo vya damu, ikiwa ni pamoja na kiwango cha damu na viwango vya homoni fulani

  • Kupima ujauzito

  • Atrasonografia ya kutumia kifaa kiwekwacho ukeni (madaktari wanapoweka kifaa cha kupima kwa kupiga picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwenye uke wako ili kuangalia uterasi, ovari, mlango wa kizazi na uke wako)

Kama una viashiria vya hatari ya saratani au ikiwa kuna mabadiliko fulani yanayoonekana kwenye uchunguzi wa kipimo cha picha kinachotumia mawimbi ya sauti, daktari wako anaweza pia kufanya:

  • Histeroskopia (kuangalia ndani ya uterasi yako kwa kutumia bomba la kuangalia)

  • Utoaji wa kipande cha tishu kwa ajili ya uchunguzi—kuchukua sampuli ya tishu kutoka kwenye utando wa uterasi na kuichunguza kwa kutumia darubini

Je, madaktari hutibu vipi hali isiyo ya kawaida ya uterasi kuvuja damu?

Kwanza, kwa kawaida madaktari:

  • Hukupa dawa ya kudhibiti damu kuvuja, kama vile dawa za kuzuia mimba au homoni zingine mbalimbali za kike, au wakati mwingine NSAID (dawa za kupunguza maumivu zisizo za steroidi) au dawa inayodhibiti uvimbe au asidi ya traneksamiki

Iwapo dawa itashindwa kuzuia hali isiyo ya kawaida ya uteresi yako kuvuja damu, madaktari wanaweza kufanya utaratibu kama vile:

  • Kukwaruza utando wa uterasi yako ili kuondoa tishu—huu unaitwa D na C (kupanua na kukwangua)

  • Kuondoa utando wa uterasi kwa kuugandisha au kuuchoma moto—hii inaitwa uondoaji wa tishu kwenye endometria

Ikiwa matibabu yaliyo hapo juu hayatasitisha uvujaji damu wako au ikiwa vipimo vitaonyesha saratani, madaktari wanaweza kufanya upasuaji ili kuondoa uterasi yako. Upasuaji huo unaitwa histerektomia.