Kuzuizi cha Utumbo

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Ni nini maana ya kuzuizi cha utumbo (utumbo uliozibwa)?

Una utumbo mdogo na utumbo mpana. Utumbo mdogo ni tyubu ndefu iliyojikunja ambayo huunganisha tumbo yako na utumbo mpana. Utumbo mpana ni mfupi lakini mpana zaidi na unatoka mwishoni mwa utumbo mdogo hadi kwenye rektamu. Matumbo yako hupokea chakula na majimaji kutoka kwenye tumbo yako. Yanameng'enya na kufyonza sehemu kubwa ya vitu hivi. Kinachosalia huondoka mwilini kama kinyesi (haja kubwa) kupitia kwenye rektamu na tundu la haja kubwa.

Utumbo mdogo na mpana unaweza kuzibwa.

  • Kisababishi kikubwa zaidi cha utumbo uliozibwa kwa watu wazima ni tishu za makovu kutokana na upasuaji, ngiri, na uvimbe

  • Chakula na majimaji haviwezi kupita kwenye utumbo uliozibwa

  • Utumbo wako huvimba unapojazwa kwa chakula, majimaji na gesi

  • Unapata maumivu ya tumbo, kuhisi kichefuchefu na unaweza kutapika

  • Madaktari hupata uzibaji kwa kufanya eksirei

  • Huenda ukahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuondoa uzibaji

  • Hali hiyo isipotibiwa, utumbo unaweza kupasuka na kusababisha kuvimba na maambukizi ndani ya tumbo yako

  • Utumbo uliozibwa ukipasuka (kutoboka) na kuambukiza sehemu za ndani ya tumbo yako, hali hiyo inaweza kukufanya mgonjwa sana na inaweza kukuua

The Digestive System

Utumbo uliozibwa husababishwa na nini?

Kwa watoto, matumbo yaliyozibwa husababishwa na:

  • Kasoro fulani za kuzaliwa

  • Mekoni ngumu (kinyesi cha kijani kilichokolea kinachotengenezwa ndani ya matumbo ya mtoto kabla hajazaliwa)

  • Kupinda kwa kitanzi cha utumbo

  • Kipande chembamba au kinachokosekana cha matumbo

  • Kuteleza kwa sehemu moja ya utumbo kwenda kwa nyingine (hali iitwayo intasosepsheni)

  • Kitu ambacho mtoto amemeza

Kwa watu wazima, matumbo yaliyozibwa husababishwa na:

  • Tishu za kovu kutokana na upasuaji wa tumbo wa awali

  • Ngiri

  • Saratani

  • Bonge gumu la kinyesi

Dalili za utumbo uliozibwa ni zipi?

Dalili za utumbo uliozibwa ni pamoja na:

  • Maumivu ya kusokota tumboni mwako

  • Kuvimba tumbo

  • Kutohisi njaa

  • Kutapika

  • Kushindwa kutoa kinyesi au gesi

Wakati mwingine damu huacha kufikia sehemu fulani ya utumbo uliozibwa. Hali hii inapotokea, sehemu ya utumbo itakufa na huenda ukapata:

  • Maumivu makali yasiyobadilika

  • Homa kutokana na maambukizi

  • Shinikizo la chini la damu na ogani kuacha kufanya kazi (sepsisi)

Je, madaktari wanawezaje kujua iwapo nina utumbo uliozibwa?

Madaktari wakishuku kuwa una utumbo uliozibwa, huwa wanafanya:

Je, madaktari wanatibu vipi tatizo la utumbo uliozibwa?

Madaktari watakulaza hospitalini na:

  • Wakuzuie usile wala kunywa chochote

  • Watapitisha tyubu kupitia pua lako hadi kwenye utumbo (tyubu ya NG) ili kufyonza kila kitu kilicho nyumba ya uzibaji

  • Watakupatia majimaji moja kwa moja kupitia mshipa (IV)

Wakati mwingine uzibaji hutoweka baada ya kutumia tyubu hiyo ya kufyonza. Uzibaji usipotoweka, huenda ukahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuondoa uzibaji.