Ngiri kwenye Ukuta wa Tumbo

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Je, uvimbe wa ngiri ni nini?

Ngiri ni uvimbe wa ogani unaochomoza kupitia misuli au tishu zinazoishikilia mahali pake.

Kuna aina nyingi tofauti za uvimbe wa ngiri. Ngiri zinazotokea sana hupatikana kwenye ukuta wa tumbo.

Ngiri ya Kinena
Ficha Maelezo
Picha hii inaonyesha matumbo yaliyosukumwa nje katika ukuta wa tumbo hadi kwenye sehemu ya kinena, na hivyo kusababisha uvimbe kutokea chini ya ngozi.

Ni nini maana ya ngiri ya ukuta wa tumbo?

Ngiri ya ukuta wa tumbo ni uvimbe unaochomoza kwenye tumbo lako. Uvimbe huo unaochomoza husababishwa na utumbo mdogo unaposukuma kupitia shimo ndogo au sehemu dhaifu katika ukuta wa tumbo yako.

  • Ngiri ya ukuta wa tumbo wakati mwingine huunda uvimbe unaochomoza ambao unaweza kuuona na huenda ukasababisha maumivu au usisababishe maumivu

  • Ngiri za ukuta wa tumbo hutokea sana, haswa kwa wanaume

  • Kubeba vitu vizito au kufanya kazi nzito kunaweza kusababisha uvimbe uonekane mkubwa zaidi

  • Madaktari hutibu ngiri kwa kufanya upasuaji

Zipi ni aina za ngiri za ukuta wa tumbo?

Ngiri hupewa majina kulingana na mahali zilipo. Ngiri za ukuta wa tumbo zinaweza kujitokeza katika sehemu nyingi tofauti:

  • Ngiri ya kinena: kwenye mkunjo wa kinena chako au kwenye korodani (kifuko kinachozingira pumbu zako)

  • Ngiri ya utumbo: kwenye sehemu ya kitovu, inatokea sana kwa watoto

  • Ngiri ya sehemu ya kati ya tumbo: kwenye sehemu ya katikati ya tumbo lako, juu ya kitovu na chini ya mbavu zako

  • Ngiri ya paja: chini kidogo ya mkunjo wa kinena chako katikati ya sehemu ya juu ya paja lako

  • Ngiri iliyotokana na upasuaji: katika sehemu ambapo ukuta wa tumbo lako ulikatwa kwa ajili ya upasuaji (hali hii inaweza kutokea miaka mingi baada ya upasuaji)

Sehemu hizi zote ni sehemu dhaifu kwenye ukuta wa tumbo yako. Shimo linaweza kutokea kivyake au unapofanya shughuli ya kukaza misuli sana.

Uvimbe wa ngiri kufungwa hutokea pale vitanzi vya utumbo wako vinakwama kwenye uvimbe wa ngiri. Hali hii inaweza kuziba utumbo wako.

Uvimbe wa ngiri uliobanwa hutokea pale ambapo utumbo wako umebanwa kabisa na kuzuia usambazaji wa damu. Sehemu ya utumbo wako ambayo haipati damu ya kutosha inaweza kupasuka na kufa na isipotibiwa, inaweza kukuua.

"Ngiri ya kispoti" si ngiri haswa. Ni msuli uliochanika katika sehemu ya chini ya tumbo lako ambao unaweza kusababisha maumivu kwenye sehemu hiyo kama ilivyo kwa ngiri halisi.

Je, dalili za ngiri kwenye ukuta wa tumbo ni zipi?

Kwa kawaida, dalili ya pekee ya ngiri ni uvimbe unaochomoza mahali ngiri ilipo. Huenda ukaeza kuona uvimbe unaochomoza wakati tu unainua kitu au unapokaza misuli. Wewe au daktari wako anaweza kusukuma uvimbe huo urudi mahali unapofaa.

Ngiri zilizofungamana haziwezi kusukumwa zirudi mahali zinapofaa na zinaweza kusababisha maumivu zaidi.

Ngiri zinazozuia mtiririko wa damu haziwezi kusukumwa zirudi mahali zinapofaa na zinaweza kusababisha dalili:

  • Maumivu ya kudumu yanayozidi kuwa mabaya kadri muda unavyosonga

  • Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika

  • Mwasho uvimbe unapoguswa

  • Wakati mwingine, uvimbe huwa na wekundu

Ngiri za kufungamana na kusokotwa zinaweza kuziba utumbo wako kiasi kwamba chakula na majimaji yashindwe kupenya. Kikwazo hiki huitwa kuzuizi cha utumbo. Kizuizi cha utumbo hukufanya uhisi kichefuchefu tumboni na kusababisha tumbo lako kuvimba. Ni tatizo la dharura.

Madaktari wanawezaje kujua iwapo nina ngiri ya ukuta wa tumbo?

Madaktari hutambua uwepo wa ngiri ya ukuta wa tumbo kulingana na uchunguzi. Wanaweza pia kufanya kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti au uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) iwapo wanataka kuwa na uhakika kuwa dalili zako hazitokani na kitu kingine.

Je, madaktari hutibu vipi ngiri ya ukuta wa tumbo?

Madaktari hutibu ngiri yako kulingana na mahali ilipo na dalili ulizo nazo. Baadhi ya ngiri huachwa zilivyo. Ngiri zingine huhitaji upasuaji kabla hazijasababisha matatizo. Lakini madaktari hufanya upasuaji mara moja ikiwa ngiri imefungamana au inazuia mtiririko wa damu.

Kwa watoto, ngiri zilizo kwenye sehemu ya kitovu hutoweka bila matibabu.