Kutoboka kwa Njia ya Mmeng'enyo wa Chakula

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Utobokaji ni hali ya kupata tundu.

Njia ya mmeng'enyo wa chakula ni kikundi cha ogani zenye njia ya kupitisha chakula unapomeza na kukimeng'enya. Ogani hizi ni sehemu ya njia ya mmeng'enyo wa chakula:

Mfumo wa Kusaga Chakula

Je, ni nini maana ya kutoboka kwa njia ya mmeng'enyo wa chakula?

Kutoboka kwa njia ya mmeng'enyo wa chakula ni tundu kwenye ogani yako yoyote ya njia ya mmeng'enyo wa chakula.

  • Majeraha, magonjwa fulani, au kumeza vitu fulani kunaweza kusababisha shimo kwenye njia ya mmeng'enyo wa chakula

  • Chakula, juisi za utumbo au uchafu hupenya kwenye shimo hilo na kuingia kwenye kifua au tumbo yako na kukufanya mgonjwa sana

  • Utakuwa na maumivu makali ya ghafla kwenye kifua au tumbo yako

  • Madaktari hufanya eksirei na wakati mwingine uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta)

  • Kutoboka ni dharura ya kimatibabu na utahitaji kufanyiwa upasuaji mara moja

  • Bila matibabu, unaweza kufariki

Je, ni nini husababisha kutoboka kwa njia ya mmeng'enyo wa chakula?

Visababishi vya kutoboka hutegemea mahali tundu lilipo kwenye njia ya mmeng'enyo wa chakula. Husababishwa na:

Zipi ni dalili za njia ya mmeng'enyo wa chakula iliyotoboka?

Dalili za kutoboka kwa njia ya mmeng'enyo wa chakula zinajumuisha:

  • Maumivu makali ya ghafla kwenye tumbo au kifua chako

  • Kutokwa jasho

  • Tumbo inayohisi maumivu na ambayo ni ngumu inapoguswa

  • Kuhisi mgonjwa tumboni

  • Kutapika

Madaktari wanawezaje kujua iwapo njia yangu ya mmeng'enyo wa chakula imetoboka?

Madaktari watafanya:

Madaktari hutibu vipi kutoboka kwa njia ya mmeng'enyo wa chakula?

Madaktari hutibu kutoboka kwa njia ya mmeng'enyo wa chakula kwa kutumia:

  • Upasuaji wa dharura wa kufunga shimo na kuzuia majimaji na vitu vilivyo kwenye matumbo visipenye

  • Majimaji na dawa za kuua bakteria unazopewa kupitia mshipa wako (IV)