Utumbo Mdogo

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Mfumo wako wa usagaji chakula hugawanya chakula kuwa virutubishi tofauti ambavyo hutumika mwilini.

Njia ya mmeng'enyo wa chakula (pia inaitwa njia ya utumbo na tumbo au GI) ni mrija mtupu ambao chakula hupitia unapokimeza, hukimeng'enywa, na kisha uchafu kutolewa kama kinyesi.

Je, utumbo mdogo ni nini?

Utumbo wako mdogo, pia hujulikana kama matumbo madogo, ni sehemu ya njia ya mmeng'enyo wa chakula. Huunganisha tumbo lako na utumbo mpana. Virutubishi vingi hunyonywa kwenye utumbo mdogo.

Utumbo wako mdogo una sehemu tatu:

  • Duodeni

  • Jejunamu

  • Ileamu

Duodeni ni sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo wako na imeungana na tumbo lako. Chakula na vimiminiko hutoka tumboni na kuingia kwenye duodeni ili viendelee kusagwa. Juisi za usagaji wa chakula zinazotoka kwenye kongosho na nyongo (majimaji ya kijani ambayo husaidia kumeng'enya mafuta) kutoka kwenye kibofu nyongo na ini huingia kwenye duodeni yako kupitia mabomba madogo yanayoitwa mifereji. Juisi hizi husaidia kuvunja vunja chakula na pia kuzimua asidi ya tumboni. Kuta za utumbo mdogo hutengeneza kemikali zinazoitwa vimeng'enyo ambazo husaidia kusaga chakula.

Jejunamu na ileamu ni sehemu za 2 na 3 za utumbo mdogo. Pia hunyonya virutubishi

Kuta za utumbo mdogo zina utando wa misuli ambayo hukaza ili kusukuma chakula kipite.

Kufikia Utumbo Mdogo