Nyenzo za Mada

Je, ini ni nini?

Ini lako ni kiungo cha ukubwa wa mpira wa miguu upande wa kulia wa tumbo lako, chini kidogo ya kiwambo chako (misuli iliyo chini ya kifua chako inayosaidia kupumua) na inalindwa na mbavu zako za chini za kulia.

  • Ini hukusaidia kusaga chakula na kutengeneza dutu ambazo mwili wako unazihitaji

  • Ini linahusika katika michakato mbalimbali katika mwili wako

  • Kunywa pombe nyingi kwa muda mrefu kunaweza kuharibu ini

Kufikia Ini

Je, ini hufanya kazi gani?

Ini ni kama kiwanda cha mwili wako cha kuzalisha kemikali. Hutengeneza dutu nyingi muhimu ikijumuisha:

  • Nyogo, majimaji ya umeng'enyaji ambayo huvunjavunja mafuta

  • Protini ambazo husadia damu yako kuganda

  • Lehemu, ambayo mwili wako unahitaji ili kuunda homoni fulani

Mambo mengine ambayo ini linafanya ni pamoja na:

  • Kuhifadhi sukari na kuiachia pale ambapo mwili wako unahitaji nishati ya ziada

  • Kuvunjavunja dawa, sumu, na dutu zingine ili mwili wako uviondoe

Je, nyongo ni nini?

Nyongo ni majimaji ya kumeng'enya chakula ambayo ni mazito, yenye rangi ya njano-kijani yanayotengenezwa kwenye ini lako. Nyongo hutiririka kupitia mirija kwenye ini lako iitwayo mirija ya nyongo. Kisha nyongo hutiririka nje ya ini kupitia mrija mkubwa wa nyongo. Nyongo huenda moja kwa moja kwenye utumbo wako au kwenye kibofu nyongo ili kuhifadhiwa mpaka pale inapohitajika.

Kwenye matumbo, nyongo hukusaidia kufyonza mafuta unayokula.

Je, ini linaweza kupata matatizo gani?

Matatizo ya ini lako ni pamoja na:

Kirosisi ni ya kudumu, lakini mara nyingi unakuwa na tishu za ini zenye afya za kuendelea kufanya kazi ya ini. Kirosisi kali inaweza kusababisha:

  • Shinikizo la juu la damu kwenye ini, hali inayoitwa shinikizo la juu la damu kwenye mshipa wa langu

Vitu vingi vinavyoharibu ini lako huingilia jinsi linavyotengeneza na kusafirisha nyongo. Matatizo ya kutengeneza na kusafirisha nyongo yanaweza kusababisha ngozi na macho yako yageuka rangi na kuwa ya manjano (homa ya nyongo ya manjano) kwa sababu una kiasi kikubwa cha kemikali inayoitwa bilirubini, ambayo mwili wako huitumia kutengeneza nyongo.

Ikiwa ini lako limeharibiwa kwa kiasi kikubwa, unaweza kuhitaji kupandikizwa ini.