Kibofu nyongo

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2024

Je, kibofu nyongo ni nini?

Kibofu nyongo ni kifuko kidogo kilicho upande wa kulia wa tumbo lako chini ya mbavu zako. Ni ogani ambapo mwili wako uhifadhi nyongo kabla ya kwenda kwenye utumbo. Nyongo ni kiowevu cha kusaga chakula ambacho husaidia kumeng'enya mafuta kwenye chakula.

Uchunguzi wa Ini na Kibofu nyongo

Je, kibofu nyongo hufanya kazi gani?

Kibofu nyongo chako uhifadhi nyongo, majimaji ya umeng'enyaji ambayo hutengenezwa na ini lako.

  • Unapokula kitu, mwili wako hupeleka ishara kwa kibofu nyongo ili kikaze na kusukuma nyongo kwenye utumbo wako.

Kwa sababu nyongo nayo pia inaweza kutiririka moja kwa moja kutoka kwenye ini lako hadi kwenye utumbo wako, unaweza kuishi bila kibofu nyongo chako.

Je, nyongo ni nini?

Nyongo ni majimaji ya kumeng'enya chakula ambayo ni mazito, yenye rangi ya njano-kijani. Nyongo hutiririka kupitia mirija kwenye ini lako iitwayo mirija ya nyongo. Kisha nyongo hutiririka nje ya ini kupitia mrija mkubwa wa nyongo. Nyongo huenda moja kwa moja kwenye utumbo wako au kwenye kibofu nyongo ili kuhifadhiwa.

Kwenye matumbo, nyongo hukusaidia kufyonza mafuta unayokula.

Je, kibofu nyongo kinaweza kupata matatizo gani?

Matatizo makuu unayoweza kuyapata kwa kibofu nyongo chako ni:

Mawe ya nyongo ni mabonge ya vitu vigumu yanayoweza kutokea kwenye kibofu nyongo chako na kuzuia mtiririko wa nyongo. Ikiwa yatasababisha dalili, madaktari wanaweza kuondoa mawe hayo na kibofu nyongo chako.

Wakati mwingine kibofu nyongo chako kinaweza kuvimba pasipo kuwa na mawe ya nyongo.