Mawe ya nyongo

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Mawe ya nyongo ni nini?

Mawe ya nyongo ni vitu vigumu vinavyoweza kujitengeneza kwenye kibofu nyongo. Kibofu nyongo chako ni kiungo ambapo mwili wako unatunza nyongo. Nyongo ni kiowevu kimeng'enyaji ambacho husaidia kuvunja mafuta kuwa chakula kabla hayajaenda kwenye utumbo.

  • Kwa kawaida mawe ya nyongo huwa yanakaa kwenye kibofu nyongo chako na hayasababishi matatizo

  • Wakati mwingine, mawe ya nyongo yana kwangua kibofu nyongo (huitwa kolekitisi) au yanazuia mfereji unaotoka kwenye kibofu nyongo kwenda kwenye utumbo na kusababisha maumivu ya tumbo la juu yanayoweza kudumu kwa saa kadhaa

  • Madakatari hufanya kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti, kipimo kinachotumia mawimbi ya sauti kutengeneza picha, ili kuona mawe ya nyongo

  • Mawe ya nyongo ni kawaida sana kwa wanawake na watu wenye umri mkubwa

  • Mawe ya nyongo yanasababisha maumivu au matatizo mengineyo, madaktari wanaweza kuondoa kibofu nyongo chako

Je, mawe ya nyongo husababishwa na nini?

Mawe ya nyongo husababishwa na dutu fulani zinazokusanya na kutengeneza mabonge kwenye nyongo katika kibofu nyongo chako.

Dutu hizi zina uwezekano mkubwa wa kutengeneza mawe ya nyongo ikiwa kibofu nyongo chako hakifanya kazi vizuri na hakiondoi nyongo kwa kawaida.

Ni zipi hatari zinazohusiana na mawe ya nyongo?

Una uwezekano mkubwa wa kupata mawe ya nyongo ikiwa:

  • Ni mwanamke

  • Una umri wa zaidi ya miaka 65

  • Mmarekani wa Asili ya India

  • Una unene kupita kiasi

  • Umepoteza uzani mkubwa kwa haraka sana

  • Una wanafamilia ambao walikuwa na mawe ya nyongo

  • Unakula mlo wenye mafuta na lehemu nyingi

Je, dalili za mawe ya nyongo ni zipi?

Mawe mengi ya nyongo hayaonyeshi dalili.

Unaweza kuwa na dalili ikiwa mawe ya nyongo yanachubua kibofu nyongo chako yanaziba neli inayotoka kwenye kibofu nyongo kwenda kwenye utumbo. Dalili hizi zinajumuisha:

  • Maumivu makali kwenye upande wa juu wa tumbo lako, kwa kawaida upande wa kulia

  • Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika

  • Homa

  • Homa ya nyongo ya manjano (wakati ngozi yako na sehemu nyeupe za macho yako hugeukia kuwa za rangi ya manjano)

Dalili zinaweza kuwa mbaya zaidi baada ya kula mlo mkubwa.

Maumivu yanaweza kuwa makali sana hadi kupelekwa hospitalini kitengo cha dharura. Lakini yanaweza kuondoka huenda yakarudi au yasirudi.

Ikiwa maumivu hayaondoko, unaweza kuwa na matatizo makubwa kama vile:

  • Kolekitisi au mfereji uliozibwa unaohitaji kufanyiwa upasuaji

  • Tundu kwenye ukuta wa kibofu nyongo chako

  • Matatizo kwenye ini lako, kongosho au viungo vingine kwenye tumbo lako

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina mawe ya nyongo?

Ili kujua kama kuna mawe nyongo, madaktari:

  • Wanafanya kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwenye eneo la tumbo lako ili kuunda picha ya kibofu nyongo na ogani zingine

  • Wakati mwingine, wanafanya MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku), kipimo maalumu ili kuunda picha ya kina zaidi ya viungo vyako

  • Wanafanya vipimo vya damu ili kuchunguza ini lako (vipimo vya ini)

Je, madaktari wanatibu vipi mawe ya nyongo?

Mawe ya nyongo ambayo hayaonyeshi dalili kwa kawaida hayahitaji kutibiwa.

Ili kutibu mawe ya nyongo yanayosababisha maumivu, madaktari wanafanya upasuaji ili kuondoa kibofu nyongo chako. Kufanya upasuaji, kwa kawaida madaktari wanatumia upasuaji unaotumia laparoskopi. Daktari atakudunga tumboni na kuingiza mrija usiopinda wa kutazama (laparoskopi) ndani ya mwili wako. Atakudunga sehemu moja au nyingine mbili ili kuingiza vifaa vinavyohitajika kukata kibofu nyongo chako. Kisha kibofu nyongo chako kitatolewa kupitia tundu hilo dogo.

Wakati mwigine hali yako inapokuwa si ya dharura na upasuaji unaweza kuwa hatari, madakatri wanaweza kukupa dawa ili kujaribu kuyavunja na kuyayeyusha taratibu mawe ya nyongo yako. Si mara zote dawa hizi zinafanya kazi.