Skorosingi Kolanjaitisi ya Msingi

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Skorosingi kolanjaitisi ya msingi ni nini?

Skorosingi kolanjaitisi ya msingi ni ugonjwa wa muda mrefu ambao unasababisha kuvimba, makovu na kufanya mifereji ya nyongo kuwa myembamba.

Mfereji wako wa nyongo ni neli zinazobeba nyongo kutoka kwenye ini lako kwenda kwenye utumbo wako. Nyongo ni majimaji mazito yenye rangi ya ukijani yanayosaidia katika umeng'enyaji wa chakula. Ndani ya ini lako kuna mifereji midogo ya nyongo. Nje ya ini lako kuna miferaji mikubwa ya nyongo inayounganisha ini lako na utumbo.

  • Ikiwa una skorosingi kolanjaitisi ya msingi, mfereji wako wa nyongo unazibwa na hatimaye ini lako linaacha kufanya kazi

  • Primary sclerosing cholangitis inapatikana sana kwa watu wenye ugonjwa wa uchochezi wa matumbo, hasa wanaume walio na umei wa miaka 40

  • Dalili za kwanza ni udhaufu, uchovu na ngozi inayowasha

  • Mfereji wa nyongo uliozibwa unaweza kusababisha saratani ya mfereji wa nyongo na kirosisi

  • Madaktari wanatibu skorosingi kolanjaitisi ya msingi kwa kutumia dawa za mwasho na wakati mwingine upasuaji ili kufungua mfereji wa nyongo au kupandikiza ini

Nini kinachosababisha skorosingi kolanjaitisi ya msingi?

Madaktari hawana uhakika ni nini hasa kinachosababisha cholangitisi ya sklerosi ya msingi, lakini kuna uwezekano kuwa ni ugonjwa wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili (ugonjwa unaosababisha mfumo wako wa kingamwili kushambulia tishu zake).

Una uwezekano wa kuupata iwapo:

  • Ugonjwa wa uchochezi wa matumbo, hasa kolaitisi ya vidonda

  • Una watu katika familia yako wenye ugonjwa huo

Je, dalili za skorosingi kolanjaitisi ya msingi ni zipi?

Dalili za skorosingi kolanjaitisi ya msingi hujumuisha:

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Ngozi inayowasha

  • Macho na ngozi ya manjano (homa ya nyongo ya manjano)

  • Wakati mwingine, maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo lako

Baadaye unaweza kuwa na:

Ini kushindwa kufanya kazi kwa kawaida hutokea karibu miaka 12 baada ya kugundulika.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina skorosingi kolanjaitisi ya msingi?

Madaktari wanahisi kuwa una skorosingi kolanjaitisi ya msingi kutokana na dalili ulizo nazo na hali isiyo ya kawaida wanayoiona kwenye vipimo vya damu ya ini. Ili kuwa na uhakika, watafanya:

  • Kupiga picha kwa mawimbi ya sauti mifereji ya nyongo

  • Aina maalumu ya MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) inayoitwa MRCP (upigaji picha kwa mvumo wa kolangiopankretografia) ambayo inajikita kwenye mifereji ya nyongo yako

  • Vipimo maalumu vya damu

Je, madaktari wanatibu vipi skorosingi kolanjaitisi ya msingi?

Hakuna tiba ya skorosingi kolanjaitisi ya msingi.

Ikiwa huda dalili zozote, madaktari watafanya vipimo vya damu mara mbili kwa mwaka ili kuona ini lako linafanya kazi vizuri kiasi gani.

Ikiwa una dalili, madaktari wanatibu skorosingi kolanjaitisi ya msingi kwa kutumia:

  • Dawa za kupunguza mwasho na kutibu maambukizi

  • Hatua za kufungua mfereji wa nyongo yako uliofungwa

  • Kubadilisha ini

Ninaweza kupata wapi taarifa zaidi kuhusu skorosingi kolanjaitisi ya msingi?