Kolaitisi ya Vidonda

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Njia ya mmeng'enyo wa chakula ni mkondo ambao chakula hupitia mwilini mwako baada ya kukila. Chakula huanzia kinywani mwako (kula) hadi kwenye tundu lako la haja kubwa (kupitisha kinyesi). Utumbo wako ni mrija mrefu katika mfumo wa umeng’enyaji chakula unaounganisha tumbo lako na tundu lako la haja kubwa. Humeng'enya chakula na kufyonza virutubishi.

Una utumbo mdogo na utumbo mpana. Utumbo mdogo, au utumbo mwembamba, ni mrefu sana na wenye mikunjo mingi. Utumbo mpana, pia huitwa koloni au utumbo mkubwa, ni mfupi na mpana.

Je, kolaitisi ya vidonda ni nini?

Kolaitisi ya vidonda ni ugonjwa wa muda mrefu ambao husababisha utumbo wako mpana (utumbo mkubwa) kuvimba. Hauathiri utumbo wako mdogo. Kolaitisi ya vidonda ni mojawapo kati ya magonjwa mawili ya ugonjwa wa uchochezi wa matumbo. Ugonjwa huo mwingine wa ugonjwa wa uchochezi wa matumbo ni ugonjwa wa Crohn.

  • Kolaitisi ya vidonda ni ugonjwa wa uchochezi wa matumbo

  • Dalili hutokea na kuondoka na zinajumuisha mikakamao ya tumbo, haja ya mara kwa mara ya kutoa kinyesi na kuhara damu

  • Madaktari wataangalia kinyesi chako na kutumia mfereji wa kutazama kuangalia utumbo wako

  • Madaktari hutumia matibabu kudhibiti kuvimba kwa utumbo wako, kutuliza dalili na kurekebisha viowevu na virutubishi vilivyopotezwa

  • Kolaitisi ya vidonda ya muda mrefu huongeza hatari yako ya kupata saratini ya utumbo mpana

Kolaitisi ya vidonda inaweza kuanza katika umri wowote lakini kwa kawaida huanza kabla ya umri wa miaka 30.

Je, nini husababisha kolaitisi ya vidonda?

Madaktari hawajui ni nini husababisha kolaitisi ya vidonda. Inaweza kuwa ni jkwa sababu ya tatizo kwa mfumo wako wa kingamwili ambalo linasababisha utumbo wako kuhisi vibaya na kuvimba. Kolaitisi ya vidonda inaweza kuwa inarithishwa kwenye familia na hupatikana zaidi kwa watu kutoka jamii ya Kiyahudi ambao familia zao zinatoka Ulaya Mashariki.

Je, dalili za kolaitisi ya vidonda ni zipi?

Dalili za kolaitisi ya vidonda hutokea na kupotea. Kuibuka kunaweza kuwa kali kwa siku au wiki chache na kisha kuisha au angalau kuwa vizuri kwa muda. Kwa watu wengi, dalili huendelea kujitokeza na kutoweka maisha yao yote.

Kwa kawaida, kuibuka huanzia polepole. Dalili zinajumuisha:

  • Haja thabiti ya kutoa kinyesi

  • Mikakamao midogo kwenye tumbo yako ya chini

  • Damu na makamasi kwenye kinyesi chako

Kuibuka kunaweza kuwa kwa ghafla na kali, hivyo kusababisha:

  • Kuharisha hatari sana mara nyingi pamoja na makamasi na damu

  • Kuvuja damu nyingi kutoka kwenye tundu lako la haja kubwa

  • Homa kali

  • Maumivu ya tumbo

Wakati mwingine katika hali mbaya ya kuibuka kwa hali hiyo, utumbo wako mpana huvimba sana na unaweza kupata shimo dogo (utoboka). Utoboaji huruhusu kinyesi kuingia kwenye tumbo yako, ambayo inaweza kusababisha maambukizi ya kutishia maisha (peritonitis).

Ikiwa una kolaitisi ya vidonda kwa muda mrefu, unaweza kuwa na:

  • Upele kwenye ngozi

  • Vidonda vya mdomo

  • Maumivu ya viungo

  • Macho chungu, nyekundu

  • Matatizo kwa ini na kibofu nyongo chako

  • kiwango cha chini cha damu (anemia)

  • Kupungua uzani

  • Hatari iliyoongezeka ya saratani ya utumbo mpana

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kolaitisi ya vidonda?

Madaktari wataingiza mfereji mwembamba, mwepesi ulio na kamera ndogo kupitia kwenye tundu lako la haja kubwa ili kuangalia utumbo wako (kolonoskopia) ili:

  • Kuangalia kiwangu cha uvimbe uliopo

  • Kuchukua sampuli za makamasi au kinyesi

  • Kuondoa sampuli za tishu kutoka kwenye sehemu zilizovimba na kuziangalia kwa kutumia hadubini (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi)

Huenda daktari pia:

Wakati mwingine ni ngumu kwa madaktari kujua tofauti kati ya kolaitisi ya vidonda na ugonjwa wa Crohn wa utumbo mpana kwa sababu dalili zake nyingi hufanana.

Je, madaktari hutibu vipi kolaitisi ya vidonda?

Hakuna tiba ya kolaitisi ya vidonda. Matibabu mengi yanaweza kusaidia na dalili.

Dawa zinaweza:

  • Kukomesha maumivu ya tumbo na kuharisha

  • Kupunguza uvimbe kwenye utumbo wako

  • Kubadilisha jinsi mfumo wetu wa kingamwili unavyofanya kazi

Matibabu mengine ni pamoja na:

  • Kunywa viowevu vya kutosha

  • Kutumia virutubishi vya madini chuma, kalsiamu na vitamini D

  • Kuepuka kula njugu na matunda mabichi na mboga wakati unakabiliwa na kulipuka kwake

  • Kujaribu lishe yenye haina bidhaa za maziwa ili kuona kama inatuliza dalili

  • Kutotumia dawa fulani ambazo zinaweza kusababisha kuibuka, kama vile dawa za kutuliza maumivu zinazoitwa NSAID (dawa za kupunguza uvimbe isiyo na asteroidi)

  • Kuepuka mfadhaiko

Ikiwa dawa hazifanyi kazi—au baadaye sana ili kupunguza hatari yako ya saratani ya utumbo mpana—upasuaji unaweza kufanywa ili kuondoa utumbo wako mpana. Wakati mwingine baada ya upasuaji una ileostomia. Ileostomia ni mpenyo kwenye tumbo yako ya chini uliounganishwa na sehemu ya mwisho ya utumbo wako mdogo. Kinyesi chako hutokea kwenye ileostomia hadi kwenye mkoba wa plastiki. Wakati mwingine daktari anaweza kufanya utaratibu maalumu ambao huondoa utumbo wako mpana lakini haihitaji ileostomia.

Ikiwa haujafanyiwa upasuaji, madaktari watafanya kolonoskopia mara kwa mara ili kuangalia dalili za mapema za saratani.