Ugonjwa wa Crohn

(Granulomatasi Ileitis; Granulomatasi Ileokolitisi; Enteritisi ya Kanda)

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Njia ya mmeng'enyo wa chakula ni mkondo ambao chakula hupitia mwilini mwako baada ya kukila. Chakula huanzia kinywani mwako (kula) hadi kwenye tundu lako la haja kubwa (kupitisha kinyesi). Utumbo wako ni mrija mrefu katika mfumo wa umeng’enyaji chakula unaounganisha tumbo lako na tundu lako la haja kubwa. Humeng'enya chakula na kufyonza virutubishi.

Una utumbo mdogo na utumbo mpana. Utumbo mdogo, au utumbo mwembamba, ni mrefu sana na wenye mikunjo mingi. Utumbo mpana, pia huitwa koloni au utumbo mkubwa, ni mfupi na mpana.

Ugonjwa wa Crohn ni nini?

Ugonjwa wa Crohn ni uvimbe wa muda mrefu kwenye utumbo wako. Ugonjwa wa Crohn ni mojawapo ya magonjwa mawili yanayoitwa ugonjwa wa uchochezi wa matumbo. Ugonjwa mwingine wa uchochezi wa utumbo ni kolaitisi ya vidonda.

Ugonjwa wa Crohn kwa kawaida huathiri utumbo mdogo. Lakini unaweza kuathiri utumbo mpana au utumbo mpana na mdogo.

  • Ugonjwa wa Crohn ni ugonjwa wa uchochezi wa matumbo

  • Kisababishaji hakijulikani, lakini inaweza kuwa ni kwa sababu ya tatizo kwa mfumo wako wa kingamwili

  • Dalili huja na kuisha na zinaweza kujumuisha kuhara, maumivu ya mkakamao kwenye tumbo yako, homa, kutohisi njaa na kupungua uzani

  • Madaktari hutumia kolonoskopia na vipimo vya kupiga picha ili kutambua ugonjwa wa Crohn

  • Hakuna tiba ya ugonjwa wa Crohn, lakini matibabu kwa dawa na wakati mwingine upasuaji unaweza kupunguza dalili

Je, nini husababisha ugonjwa wa Crohn?

Madaktari hawajui ni nini husababisha ugonjwa wa Crohn. Inaweza kuwa ni tatizo kwa mfumo wako wa kingamwili ambalo linasababisha utumbo wako kuhisi vibaya na kuwa na uvimbe.

Hatari ya ugonjwa wa Crohn inaongezeka ikiwa wewe:

  • Una watu kwenye familia yako walio na ugonjwa huo

  • Ni Myahudi na familia yako inatoka Ulaya Mashariki

  • Kuvuta sigara

  • Wewe ni mwanamke na unatumia dawa za kuzuia mimba

Dalili za ugonjwa wa Crohn ni zipi?

Dalili huja na kuondoka. Kwa kawaida ni kali kwa siku au wiki chache na kisha husisha au angalau huwa nzuri kwa muda. Kwa watu wengi, dalili huendelea kujitokeza na kutoweka maisha yao yote.

Dalili za kawaida zaidi kwa watu wazima zinajumuisha:

  • Kuhara, ambako wakati mwingine kuna damu

  • Maumivu ya tumbo kukakamaa

  • Homa

  • Kukosa hamu ya kula

  • Kupungua uzani

Ikiwa kuibuka ni kali, unaweza kuwa na:

Ikiwa una ugonjwa wa Crohn kwa muda mrefu, unaweza kuwa na:

  • Upele kwenye ngozi

  • Maumivu ya viungo na kuvimba

  • Macho mekundu

  • Matatizo ya ini na kibofu nyongo

  • Vidonda kwenye tundu lako la haja kubwa, na wakati mwingine kukatika kwenye utando wa tundu la haja kubwa

  • Hatari iliyoongezeka ya saratani kwenye utumbo wako

Watoto wanaweza kuwa na maumivu ya tumbo, kuhara na homa, lakini wanaweza pia kuwa na:

  • Kukua polepole

  • Viungo vilivyovimba

  • Uchovu (kuhisi ukiwa dhaifu na kuchoka kote)

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa Crohn?

Madaktari hufanya vipimo kulingana na dalili zako na jinsi zinatokea kwa ghafla:

  • Maumivu ya tumbo makali, ya ghafla: Uchunguzi wa kompyuta (tomografia ya kompyuta) au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ya tumbo yako

  • Maumivu ya tumbo yanayokuja na kuisha kwa muda: Wakati mwingine, eksirei au uchunguzi wa kompyuta wa tumbo lako baada ya wewe kunywa kiowevu ambacho huonyesha sehemu za utumbo au kumeza kapsuli maalum iliyo na kamera ndogo zaidi na kupiga picha inapopitia kwenye njia yako ya mmeng'enyo wa chakula

  • Kuharisha: Kuangalia kwenye utumbo mpana wako kwa kutumia kolonoskopia (daktari huingiza mfereji mwembamba, mwepesi ulio na kamera kupitia kwenye tundu lako la haja kubwa ili kuangalia kwenye utumbo wako)

Daktari pia watafanya vipimo vya damu. Vipimo vya damu haviwezi kutambua ugonjwa wa Crohn lakini wanaweza kujua kama una matatizo fulani.

Wakati ugonjwa wa Crohn unaathiri utumbo mpana pekee, wakati mwingine ni vigumu kwa madaktari kujua tofauti kati ya ugonjwa wa Crohn wa utumbo mpana na kolaitisi ya vidonda kwa sababu dalili nyingi hufanana.

Madaktari wanatibu aje ugonjwa wa Crohn?

Hakuna tiba ya ugonjwa wa Crohn. Matibabu yanaweza kusaidia kupunguza uvimbe na kutuliza dalili.

Dawa zinaweza:

  • Kukomesha maumivu ya tumbo na kuharisha

  • Kupunguza uvimbe kwenye utumbo wako

  • Kubadilisha jinsi mfumo wetu wa kingamwili unavyofanya kazi

Madaktari wanaweza kupendekeza viowevu maalum ambavyo vina virutubishi vya ziada ndani yake, haswa kwa watoto wanakua polepole.

Madaktari pia watakuomba:

  • Uache kuvuta sigara kwa sababu watu ambao huvuta sigara wana uwezekano mkubwa wa kufanya dalili zao zirudi baada ya matibabu

  • Kutumia virutubishi kama vile madini chuma, kalsiamu na virutubishi vya vitamini D

  • Epuka ulaji wa njugu na matunda mabichi na mboga wakati unakabiliwa na kulipuka kwake

  • Kujaribu lishe ambayo haina bidhaa za maziwa ili kuona kama inatuliza dalili

  • Kutotumia dawa fulani ambazo zinaweza kusababisha kuibuka, kama vile dawa ya kutuliza maumivu zinazoitwa NSAID

  • Kuepuka mawazo

Watu wengi walio na ugonjwa wa Crohn wanahitaji upauaji wakati mmoja. Katika upasuaji huu, madaktari hutoa sehemu ya utumbo wako. Hii husaidia na dalili. Nusu ya watu ambao wamefanyiwa upasuaji wanahitaji upasuaji wa pili baadaye.