Je, mpasuko wa tundu la haja kubwa ni nini?
Mpasuko wa tundu la haja kubwa ni kuchanika kwa utando wa tundu lako la haja kubwa (shimo lililo kwenye matako yako ambapo kinyesi hutokea).
Ni nini husababisha mpasuko wa tundu la haja kubwa?
Visababishaji mpasuko wa tundu la haja kubwa ni pamoja na:
Kupitisha kinyesi kubwa au kigumu
Kinyesi nyororo zaidi kwa marudio
Kuweka kitu kwenye tundu lako la haja kubwa, kama vile wanasesere wa ngono
Kuvimba kwa sehemu zingine za utumbo wako mpana (kolaitisi)
Wakati mwingine, ngono kupitia kwenye tundu la haja kubwa
Dalili za mpasuko wa tundu la haja kubwa ni zipi?
Kwa kawaida dalili hufanyika wakati au pindi baada ya kupitisha kinyesi na zinaweza kujumuisha:
Maumivu kwenye tundu lako la haja kubwa
Kuvuja damu (kiwango kidogo)
Wakati mwingine, mwasho
Maumivu yanaweza kudumu kutoka dakika kadhaa hadi saa kadhaa na hutokea tena wakati unapitisha kinyesi zaidi.
Mipasuko ya tundu la haj kubwa ambayo inasababisha dalili kwa chini ya wiki 6 inaitwa ya muda mfupi. Ile inasababisha dalili kwa muda mrefu inaitwa ya muda mrefu.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina mpasuko wa tundu la haja kubwa?
Kwa kawaida madaktari wanaweza kujua una mpasuko kwa kuangalia tu kwenye tundu lako la haja kubwa.
Wakati mwingine, watahitaji kufanya uchunguzi kwenye rektamu kwa kutumia kidole chenye glovu au anoskopi (mfereji mfupi madaktari hutumia kuangalia kwenye tundu la haja kubwa). Ikiwa kuna kuvuja damu, madaktari huangalia kwenye utumbo wa chini kwa kutumia skopu ndefu ili kuona kama kuna kisababishaji kingine cha kuvuja damu huko.
Madaktari hutibu vipi mpasuko wa tundu la haja kubwa?
Ili kurahisisha kupata haja kubwa (kutoa kinyesi), unaweza:
Kutumia dawa ili kufanya kinyesi chako kile nyororo
Kula ufumwele zaidi kama vile matunda na mboga au kutumia virutubishi vya ufumwele
Wakati mwingine, kutumia kitu ambacho kinasaidia kusogeza utumbo kwa ajili ya tatizo la kufunga choo (tatizo kupitisha kinyesi)
Kutumia dawa ya kupaka au mishumaa ili kulainisha tundu lako la haja kubwa
Ili kusaidia kupunguza maumivu, unaweza kuhitaji:
Kutumia dawa ya kupaka iliyo na dawa ya kufanya ganzi
Keti kwenye karai iliyo tu na maji yenye joto ya kutosha kufunika tundu lako la haja kubwa (tiba ya kukaa kwenye maji ya moto) kwa dakika 10 au 15 mara chache kwa siku
Spasm za tundu la haja kubwa ni nini?
Mipasuko ya tundu la haja kubwa inaweza kusababisha musuli kwenye tundu lako la haja kubwa liwe na mkakamao (spasm). Spasm za tundu la haja kubwa ina maumivu. Zinaweza pia kuwekea kikomo mtiririko wa damu kwenye tundu la haja kubwa. Ukosefu wa mtiririko wa damu huzuia mpasuko wa tundu la haja kubwa kupona. Ili kusitisha spasm na kusaidia mpasuko kupona, madaktari wanaweza:
Kukupea krimu ya kuweka kwenye tundu lako la haja kubwa ili kutuliza misuli
Kukudunga dawa kwenye tundu lako la haja kubwa ili kutuliza misuli
Kufanya upasuaji ili kunyoosha au kutoa musuli kwenye tundu lako la haja kubwa ikiwa mpasuko hauponi kwa kutumia matibabu mengine