Je, bawasiri ni nini?
Bawasiri ni mishipa iliyovimba kwenye ukuta wa rektamu na tundu lako la haja kubwa. Rektamu yako ni sehemu ya mwisho ya mfumo wako wa usagaji chakula ambapo kinyesi (mavi) yanahifadhiwa hadi uyapitishe. Tundu lako la haja kubwa ni tundu lililo kwenye matako ambapo kinyesi hutoka nje.
Mishipa iliyovimba inasababishwa na shinikizo la juu sana kwenye mshipa
Bawasiri inaweza kuwa nje ya rektamu na tundu la haja kubwa ambapo unaweza kuziona (bawasiri za ndani) au kuvimba nje ya tundu la haja kubwa (bawasiri za nje)
Bawasiri inaweza kusababisha maumivu na kuvuja damu
Dalili nyingi huisha bila matibabu
Je, nini husababisha bawasiri?
Shinikizo kwenye mishipa kwenye rektamu au tundu lako la haja kubwa inaweza kusababisha bawasiri. Shinikizo hili linaweza kutokana na:
Kuwa na uzani mkubwa kupita kiasi
Ujauzito
Kuinua vitu kubwa
Kufunga choo (tatizo kupitisha kinyesi) au kuhara (kinyesi chenye majimaji, chepesi) kwa muda mrefu
Kuketi kwa choo kwa muda mrefu au kusukuma kwa nguvu sana unapopitisha kinyesi
Dalili za bawasiri ni zipi?
Dalili za bawasiri zinaweza kujumuisha:
Uvimbe kwenye tundu lako la haja kubwa, ambao unaweza kuwa na maumivu au kuvimba
Kuvuja damu kutoka kwenye tundu la haja kubwa au rektamu kukiwa na au bila maumivu, haswa unapopitisha kinyesi
Ute (majimaji mazito) kwenye rektamu yako ambao hukufanya uhisi kana kwamba umemaliza kujisaidia
Kuwasha
Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina bawasiri?
Madaktari wanaona bawasiri za nje kwa urahisi. Wanaweza kutumia anoskopi (mfereji mfupi ambao madaktari hutumia kuangalia rektamu yako) ili kuona bawasiri za ndani.
Ikiwa unavuja damu kutoka kwenye tundu la haja kubwa au rektamu yako, madaktari wanaweza kuangalia utumbo wako wa chini kwa kutumia skopu ndefu ili kuona kama kuna kisababishaji kingine cha kuvuja damu.
Je, madaktari wanatibu vipi bawasiri?
Bawasiri zinahitaji matibabu pekee ikiwa zinasababisha dalili.
Matibabu ili kusaidia na dalili yanajumuisha:
Kifanyaji kinyesi kiwe nyororo
Vitu vya kufanya kinyesi kiwe chororo ikiwa umefungika choo
Kuketi kwenye karai iliyo na maji moto tu ya kutosha kufunika tundu lako la haja kubwa (tiba ya kukaa kwenye maji ya moto) kwa dakika 10 hadi 15 mara chache kwa siku
Dawa za maumivu
Krimu ya kufanya ganzi unayoweka kwenye tundu lako la haja kubwa
Matibabu ili kuondoa bawasiri zinaweza kujumuisha:
Sindano ambayo inasababisha kishikizo kwenye bawasiri na kuiharibu
Kutumia joto, mkondo wa umeme au leza ili kuharibu bawasiri hio
Kufunga bawasiri kwa kutumia bendi maalum ya mpira, ambayo hufanya bawasiri ianguke
Wakati mwingine, upasuaji ili kuondoa bawasiri
Wakati mwingine, upasuaji ili kuondoa damu iliyoganda kwenye bawasiri ambayo inasababisha maumivu makali
Ni nini naweza kufanya ili kuzuia bawasiri?
Ili kuzuia bawasiri kurejea, hata baada ya matibabu, unapaswa:
Kula chakula chenye fumwale zaidi
Kunywa vinywaji kwa wingi
Mazoezi
Kwenda kwenye choo unapohisi kuwa unapaswa uende—usisubiri
Usiketi chooni kwa muda mrefuau kukaza ili kupitisha kinyesi
Weka tundu lako la haja kubwa likiwa safi