Endoskopia

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Endoskopi ni nini?

Endoskopi ni kifaa ambacho madaktari hutumia kuangalia ndani ya mwili wako. Endoskopi inaweza pia kutumiwa kufanya vipimo na kutibu magonjwa.

Endoskopi ni bomba ambayo ina mwangaza na kamera ya video ndogo kwenye sehemu ya mwisho. Skopu hizo zina shimo ndani. Madaktari wanaweza kupitisha vifaa kupitia kwake ili kufanya vipimo na kutibu matatizo.

Endoskopi inaweza:

  • Haipindiki, imetengenezwa na metali ambayo haikunjiki

  • Inayopindika, ili ziweze kupindika kwenye kona kama nyoka

Endoskopi za ukubwa tofauti zinatumiwa kwa aina tofauti za mwili. Ukubwa ambao daktari hutumia unalingana na ni sehemu gani ya mwili wako inahitaji kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa. Kwa mfano, zinaweza kuwa:

  • Fupi na nyembamba: Kwa pua na sehemu ya nyuma ya koo yako (nasofarenogolaringoskopi)

  • Ndefu na nyembamba: Kwa ajili ya njia za upumuaji (bronkoskopi)

  • Fupi na pana: Kwa sehemu ya chini ya utumbo wako mpana (sigmoidoskopia)

  • Ndefu na pana: Kwa ajili ya tumbo yako (endoskopia ya juu) na utumbo (kolonoskopia)

Endoskopia ni nini?

Endoskopia ni kipimo chochote ambapo madaktari wanatumia bomba ya kutazama ili kupata mwonekano wa karibu wa sehemu ya ndani ya mwili wako. Endoskopia mara nyingi humaanisha kipimo ambacho madaktari hutazama kwenye njia yako ya mmeng'enyo wa chakula (utumbo au njia ya GI) kwa kutumia endoskopi inayoweza kunyumbulika.

Madaktari wanafanya aina mbili kuu za endoskopia ya GI:

  • Endoskopia ya juu—bomba inayoingia mdomoni mwako na chini kwenye umio wako, kuangalia umio, tumbo na sehemu ya utumbo mdogo wako

  • Endoskopia ya chini (kolonoskopia)—bomba inayoingia kwenye tundu lako la haja kubwa ili kuangalia rektamu na utumbo mpana

Sigmoidoskopia ni aina ya endoskopia ya GI ya chini ambapo daktari hutumia bomba fupi na huangalia tu sehemu ya chini ya utumbo wako mpana.

Viewing the Digestive Tract with an Endoscope

A flexible tube called an endoscope is used to view different parts of the digestive tract. When passed through the mouth (as shown on the left), an endoscope can be used to examine the esophagus, stomach, and some of the small intestine. When passed through the anus (right), an endoscope can be used to examine the rectum and the entire large intestine.

Kwa nini madaktari hufanya endoskopia?

Madaktari hufanya endoskopia ya GI ili kupata na mara nyingi kutibu matatizo kwenye umio, tumbo, utumbo na rektamu yako. Hata kama hauonyeshi dalili, madaktari wanaweza kufanya endoskopia ili kuchunguza matatizo makali kama vile saratini ya utumbo mpana, ambayo inaweza kutibiwa ikipatikana.

Madaktari wanaweza kutumia endoskopia ili:

  • Kujua ni kwa nini unapata dalili fulani

  • Kukagua watu wa umri fulani kwa matatizo—kwa mfano, ikiwa uko zaidi ya miaka 45, madaktari wanaweza kufanya kolonoskopia ili kuchunguza kama una saratini ya utumbo mpana

  • Kutibu matatizo fulani kwa kutumia zana ndogo ambazo zinaweza kutoshea kwenye endoskopia

Baadhi ya taratibu ambazo madaktari wanaweza kufanya kupitia kwenye endoskopia zinajumuisha:

  • Kutoa kipande kidogo cha tishu ili kukipima (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi)

  • Kutoa vinyama, kama vile polipu kwenye utumbo wako mpana

  • Kundunga sindano yenye dawa, kwa mfano, dawa ambayo husitisha kuvuja damu kutokana na kidonda

  • Kusitisha kuvuja damu kwa kutumia leza, joto au umeme

Je, nitawezaje kuwa tayari kwa ajili ya endoskopia ya juu?

  • Itakulazimu uache kula na kunywa kabla ya kipimo—daktari wako atakwambia ni lini haswa

  • Daktari wako atakueleza ikiwa unaweza kumeza dawa zako za kawaida asubuhi ya uchunguzi

Je, nitawezaje kuwa tayari kwa ajili ya endoskopia ya chini (kolonoskopia)?

  • Utakunywa viwevu pekee siku moja kabla ya kipimo, hakuna vyakula vigumu

  • Itakulazimu uache kula na kunywa usiku kabla ya kipimo—daktari wako atakwambia ni lini haswa

  • Daktari wako atakueleza ikiwa unaweza kumeza dawa zako za kawaida asubuhi ya uchunguzi

  • Utakunywa dawa ili kutoa kinyesi (mavi) nje ya utumbo wako siku kabla ya kipimo—dawa zinaweza kuwa tembe, viowevu unavyokunywa au kiowevu unaingiza kwenye tako lako (enema)

Ni nini hufanyika wakati nina endoskopia?

Wakati wa endoskopia ya juu au kolonoskopia, unalala chini na vifaa vinaambatishwa kwenye mwili wako ili kupima shinikizo la damu, mdundo wa moyo wako na kiwango cha oksijeni kwenye damu yako wakati wa kipimo.

  • Utawekwa IV kwenye mkono wako kwa ajili ya viowevu na dawa

  • Kwa endoskopia ya juu, madaktari watakuweka dawa ya kufanya ganzi kwenye koo yako

  • Utapewa dawa ya IV ili kufanya utulie na kuwa mtulivu au kukuweka usingizini

Daktari ataingiza bomba polepole kwenye mwili wako.

Daktari wako ataweza kuona matatizo kama vile:

  • Wekundu

  • Vidonda vilivyo wazi (vidonda)

  • Kuvimba

  • Vishikizo visivyo vya kawaida

Utando na tabaka za ndani zaidi za mfumo wako wa utumbo (isipokuwa sehemu ya chini ya tundu lako la haja kubwa) hazina neva ambazo zinahisi uchungu, kwa hivyo hautahisi uchungu kama hautakuwa usingizini wakati wa vipimo hivi.

Endoskopia ya juu huchukua takriban dakika 15 hadi 30. Kolonoskopia inaweza kuchukua muda mrefu zaidi. Baada ya kuamka na kuhisi kuwa kawaida, utaweza kwenda nyumbani na rafiki au mwanafamilia na kupumzika hadi siku inayofuata.

Endoskopia ni salama?

Endoskopia kwa kawaida ni salama sana. Matatizo ni ya nadra lakini yanaweza kujumuisha:

  • Kuhisi mchovu kutokana na dawa ya kutuliza

  • Kuhisi vibaya kwenye sehemu ya mwili ambayo ilichunguzwa

  • Kiwango kidogo cha kuvuja damu

  • Jeraha kwenye sehemu iliyochunguzwa

  • Kujikuna koo baada ya endoskopia ya juu

  • Kupitisha gesi nyingi sana baada ya endoskopia ya chini

Mpigie simu daktari wako mara moja ikiwa una yoyoye ya dalili hizi baada ya endoskopia:

  • Homa

  • Maumivu makali kwenye tumbo yako

  • Maumivu ya kifua au kukosa pumzi

  • Kutapika, haswa ikiwa yana ueusi au damu

  • Damu kwenye kinyesi au kinyesi cheusi