Saratani ya Utumbo Mpana

(Saratani ya Utumbo Mpana na Rektamu)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Koloni yako ni utumbo wako mpana. Rektamu yako ni mfuko ulio mwisho wa utumbo mpana ambako kinyesi huhifadhiwa hadi unapokwenda msalani.  

Kutambua Utumbo Mpana

Je, saratani ya utumbo mpana ni nini?

Saratani ni ukuaji wa seli mwilini kwa namna isiyoweza kudhibitiwa. Seli ni elementi ndogo zinazoshikamana kuunda viungo vya mwili wako. Seli zina majukumu maalum. Viungo tofauti vimeundwa na aina tofauti za seli. Aina yoyote ya seli inaweza kuwa yenye saratani.

Saratani ya utumbo mpana ni saratani inayoanzia kwenye utando wa utumbo wako mpana. Saratani ya rektamu inafanana sana na hiyo. Kuna baadhi ya saratani ambazo huitwa saratani za utumbo mpana na rektamu.

  • Dalili za kawaida kabisa ni kuvuja damu wakati unapopitisha kinyesi na kuhisi uchovu na kukosa nguvu

  • Kila mtu ambaye ana umri unaozidi miaka 45 anapaswa kuchunguzwa kwa ajli ya saratani ya utumbo mpana na rektamu

  • Saratani ya utumbo mpana na rektamu inayogunduliwa mapema ina uwezekano mkubwa wa kutibiwa

  • Mara nyingi madaktari huondoa saratani kwa upasuaji

Je, nini husababisha saratani ya utumbo mpana?

Saratani ya utumbo mpana na rektamu husababishwa na ukuaji ambao hauwezi kudhibitiwa wa seli katika utando wa utumbo mpana au rektamu. Una uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya utumbo mpana na rektamu ikiwa:

  • Una polipu (ukuaji usio wa kawaida) kwenye utumbo wako mpana

  • Una ugonjwa wa utumbo mpana kama vile kolaitisi ya vidonda au ugonjwa wa Crohn

  • Unakula kiasi kikubwa cha mafuta na vyakula vya viwandani na huli vyakula vyenye nyuzi

  • Una wanafamilia ambao wamewahi kuwa na saratani ya utumbo mpana na rektamu au polipu ya utumbo mpana

Zipi ni dalili za saratani ya utumbo mpana?

Saratani ya utumbo mpana hukua taratibu na haisababishi dalili kwa muda mrefu. Dalili zinaweza kujumuisha:

  • Kukosa nguvu na kuhisi uchovu—kwa baadhi ya watu hii ndiyo dalili pekee

  • Maumivu ya tumbo

  • Kufunga choo (Kushindwa kupitisha kinyesi)

  • Damu kwenye kinyesi chako

  • Kuhisi kama vile rektamu yako si tupu kabisa baada kujisaidia

Wakati mwingine saratani huziba utumbo mpana wako, na unapata dalili za kuziba kwa matumbo, kama vile kutapika, au maumivu ya kukakamaa kwa tumbo au tumbo kuvimba.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina saratani ya utumbo mpana?

Ikiwa una dalili ambazo madaktari wanadhani zinaweza kuwa za saratani ya utumbo mpana, kwa kawaida watafanya: 

  • Kolonoskopia, ambayo pia huitwa endoskopia ya chini

Ikiwa kolonoskopia itaonyesha saratani, basi kwa kawaida madaktari hufanya:

Madaktari wanafanyaje uchunguzi wa saratani ya utumbo mpana?

Kwa sababu saratani ya utumbo mpana huwapata watu wengi, madaktari wanashauri vipimo vya uchunguzi vya saratani kabla ya saratani kusababisha dalili. Kuchunguza saratani ya utumbo mpana mara nyingi huanza katika umri wa miaka 45 lakini mapema ikiwa una sababu fulani zenye hatari zaidi. Zungumza na daktari wako kuhusu ni lini unahitaji kuanza uchunguzi.

Vipimo vya uchunguzi vinajumuisha:

  • Kupima kinyesi chako ili kugundua uwepo wa damu ambayo huwezi kuiona

  • Sigmoidoskopia (madaktari hutumia bomba lenye kupinda la kuangalia ambalo hupitishwa kwenye tundu la haja kubwa ili kutazama sehemu ya chini ya utumbo wako mpana)

  • Kolonoskopia (ili kuwa na mtazamo kamili zaidi wa utumbo kuliko inavyowezekana kwa kutumia sigmoidoskopia, mdaktari hufunga kamera kwenye bomba jembamba, jepesi na kulipitisha kwenye tundu la haja kubwa ili kukagua utumbo mpana wako wote)

  • Kolonografia ya CT (uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) ili kuangalia utumbo wako mpana baada ya kunywa kiowevu maalum na kujaza utumbo wako mpana hewa, jambo ambalo husaidia uchukuaji wa picha)

Je, madaktari hutibu vipi saratani ya utumbo mpana?

Madaktari hutibu saratani ya utumbo mpana kwa kutumia:

  • Upasuaji wa kuondoa sehemu ya utumbo mpana yenye saratani na kuunganisha mwisho wa sehemu mbili zilizokatwa

  • Wakati mwingine, tibakemikali baada ya upasuaji

Kuelewa kolostomia

Katika kolostomia, utumbo mpana (koloni) hukatwa. Sehemu ya mwisho ya utumbo mpana yenye afya, ambayo hutangulia kabla ya kizuizi, huletwa kwenye tabaka la juu la ngozi kupitia uwazi ambao umetengenezwa kwa njia ya upasuaji kwenye ukuta wa tumbo. Kisha hushonwa kwenye ngozi ya uwazi. Kinyesi hupita katika uwazi na kuingia kwenye mfuko wa kutumika mara moja. Kolostomia huruhusu sehemu ya utumbo mpana iliyobaki kupumzika wakati mtu huyo akipata afueni. Baada ya mtu kupona kutokana na upasuaji na utumbo mpana kupona, ncha 2 zinaweza kuunganishwa tena ili kinyesi kipite kawaida.

Kwa saratani ya rektamu, madaktari wanaweza kufanya:

Ikiwa madaktari watapaswa kuondoa rektamu yako, kwa kawaida utahitaji kolostomia. Kwa kolostomia, madaktari hushikiza upande wa mwisho wa utumbo wako mpana kwenye ukuta wa uwazi wa tumbo lako. Kinyesi hutoka kwenye uwazi huu na kuingia kwenye mfuko wa plastiki wa kolostomia. Mpira hubandikwa kwenye tumbo lako kwa kutumia gundi na unaubadilisha pale unapojaa.

Baada ya matibabu yako, madaktari wataendelea kukuhudumia na kukagua afya yako kwa vipimo vya mara kwa mara, kama vile: