Kolekitisi

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Kolekitisi ni nini?

Kolekitisi ni hali ya kuvimba kwa kibofu nyongo chako. Kibofu nyongo chako ni kifuko kilicho chini ya ini lako ambapo mwili wako unahifadhi nyongo. Nyongo ni kiowevu cha kusaga chakula ambacho husaidia kumeng'enya mafuta kwenye chakula.

  • Ikiwa una kolekitisi, huenda ukawa na maumivu ya tumbo ambayo yandumu kwa zaidi ya saa 6, kuwa na homa na kuhisi kichefuchefu

  • Madaktari kwa kawaida wanachunguza kolekitisi kwa kufanya uchunguzi wa kibofu nyongo chako kwa kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti

  • Madaktari hutibu kolekitisi kwa kufanya upasuaji ili kuondoa kibofu nyongo chako

  • Kolekitisi inakuwa katika hali mbaya ikiwa inaanza kwa ghafula na kuisha kwa muda mfupi

  • Kolekitisi inakuwa sugu baada ya kupata mashambulizi kadhaa ya kolekitisi mbaya

  • Katika kolekitisi sugu, kibofu nyongo kinakwa na kovu na hakifanyi kazi vizuri kama kilivyokuwa kikifanya lakini baado kinasababisha maumivu

Je, kolekitisi husababishwa na nini?

Kisababishi kikuu cha kolekitisi ni mawe ya nyongo. Mawe ya nyongo ni vitu vigumu vinavyoweza kujitengeneza kwenye kibofu nyongo chako. Unaweza kupata mashambulizi ya kolekitisi wakati ambapo jiwe la nyongo linaziba mrija uvimbe. Mfereji wa sisti ni neli ambayo inatoa nyongo kwenye kibofu nyongo kwenda kwenye utumbo mwembamba. Mrija unapokuwa umezibwa, majimaji hayawezi kutoka kwenye kibofu nyongo chako. Majimaji yanasugua kibofu nyongo chako na kufanya kivimbe na kuuma.

Wakati mwingine jiwe la nyongo linatoka kwa kupita kwenye utumbo mwembamba au kurudi kwenye kibofu nyongo. Hali hii inafanya kibofu nyongo chako kutoa maji na maumivu yanatoweka. Hata hivyo, jiwe lilelile au jiwe jingine linaweza kuziba kibofu nyongo chako na kufanya ushambuliwe tena.

Kolekitisi inaweza pia kusababishwa na maambukizi au uvimbe kwenye kibofu nyongo lakini hali hizi ni nadra.

Kolekitisi kali

Kolekitisi bila mawe ya nyongo huitwa kolekitisi kali. Badala ya mawe ya nyongo, una vitu vidogovidogo kwenye kibofu nyongo chako ambavyo vinatengeneza kitu kama uchafu wa majimaji. Mashambulizi ya kolekitisi kali yanaweza kuchochewa na:

  • Upasuaji mkubwa

  • Majeraha makubwa, kuungua au maambukizi kwenye damu (sepsis)

  • Kulishwa kupitia mshipa kwa muda mrefu

  • Kutokula kwa muda mrefu

  • Tatizo kwenye mfumo wa kingamwili

Dalili za kolekitisi ni zipi?

Kolekitisi inaweza kutokea ghafula (kali) au kwa kujirudia kwa muda mrefu (sugu).

Dalili za kolekitisi mbaya:

  • Maumivu yasiyokoma kwenye upande wa kulia wa eneo la tumbo kwa zaidi ya saa 6, yanakuwa makali zaidi kwa kukandamiza au kuvuta pumzi ndefu, maumivu yanaweza kwenda kwenye bega lako la kulia na mgongoni

  • Kurusha na kuhisi kichefuchefu

  • Homa na mzizimo

Kwa kawaida shambulizi linadumu kuanzia karibu dakika 30 hadi siku 2 au 3. Lakini mashambulizi yanaweza kuwa makali na yakadumu kwa muda mrefu.

Watu wenye umri mkubwa (zaidi ya miaka 55) wanaweza kuwa na dalili tofuati za kolekitisi kali. Hizi zinaweza kujumuisha:

  • Kutohisi njaa

  • Kuhisi uchovu au udhaifu

  • Kutapika

Watu wenye umri mkubwa huenda wasipate homa.

Mwone daktari ikiwa dalili zako zinadumu kwa zaidi ya saa kadhaa au ikiwa una zozote kati ya dalili hizi:

  • Maumivu yanayozidi kuwa makali

  • Homa kali

  • Macho au ngozi ya njano

  • Mkojo wenye rangi nyeusi kinyesi (haja kubwa) chenye rangi nyeupe

Dalili za kolekitisi sugu:

  • Mashambulizi ya kujirudia ya kolekitisi kali

  • Maumivu ambayo yanaweza kuwa makali kidogo na ambayo hayawezi kudumu kama ilivyo kwa kolekitisi kali.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kolekitisi?

Madaktari wanaangalia iwapo dalili zako zinasababishwa na kolekitisi kwa kufanya:

  • Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa kibofu nyongo chako— kipimo kinachotumia mawimbi ya sauti kutengeneza picha iliyo kwenye mwendo

  • Kolesintigrafia ni kipimo ambacho kwacho kitu kinadungwa kwenye mishipa yako na kuwaruhusu madaktari kuona iwapo kuna kitu kinaziba kibofu nyongo chako

  • Vipimo vya damu

  • Uchanganuzi wa CT (topografia ya kompyuta), kipimo maalumu cha eksirei ambacho kinatengeneza picha ya kina ya ogani zako

Madaktari wanatibu vipi kolekitisi?

Kwa kawaida madaktari wanafanya upasuaji ili kuondoa kibofu nyongo chako.

Utabaki hospitalini. Hutaweza kula wala kunywa. Madaktari pia watakupa:

  • Majimaji kwenye mshipa wako

  • Dawa za kuua bakteria

  • Dawa za maumivu

Kwa kawaida madaktari huwa wanaondoa kibofu nyongo kwa haraka (ndani ya saa 24 hadi 48 baada ya dalili kuanza) ikiwa:

  • Una kolekitisi kali na hatari ya upasuaji ni ndogo

  • Zaidi kwa umri

  • Una kisukari

  • Unaweza kuwa na matatizo makubwa

  • Una kolekitisi kali

Wakati mwingine madaktari wanakupatia viowevu kwa njia ya mishipa, dawa za kuua bakteria na dawa ya maumivu kisha kusubiri wiki kadhaa au zaidi kabla ya kufanya upasuaji. Lakini kwa kawaida, kufanya upasuaji mapema ni bora zaidi kwako.

Kufanya upasuaji wa kibofu nyongo, kwa kawaida madaktari wanatumia upasuaji unaotumia laparoskopi. Daktari atakudunga tumboni na kuingiza mrija usiopinda wa kutazama (laparoskopi) ndani ya mwili wako. Atakudunga sehemu moja au nyingine mbili ili kuingiza vifaa vinavyohitajika kukata kibofu nyongo chako. Kisha kibofu nyongo chako kitatolewa kupitia tundu hilo dogo.