Sepsisi na mshtuko wa sepsisi ni nini?
Sepsis ni wakati ambapo vijidudu (bakteria) vinaingia kwenye mtririko wa damu na kuchochea athari kali mwilini kote. Sepsisi inapokuwa kali, mojawapo kati ya ogani zako inaweza kuacha kufanya kazi. Kwa mfano, figo yako inaweza kuacha kutengeneza mkojo, au mapafu yako yanaweza kuacha kutoa oksijeni.
Mshtuko wa sepsisi ni aina hatari sana ya sepsisi. Una shinikizo la damu la chini sana (shoti), na ogani zako nyingi zinaacha kufanya kazi. Septic shock inaweza kuwa ya kufisha.
Sepsisi inasababishwa na maambukizi ya bakteria wanaoenea kwenye mtiririko wako wa damu
Watu wenye mfumo wa kingamaradhi ambao ni dhaifu au magonjwa fulani, kama vile kisikari au kirosisi ya ini, wana uwezekano mkubwa wa kupata sepsisi
Madaktari wanapaswa kutibu sepsisi na mshtuko wa sepsisi mapema kadiri iwezekanavyo kwa kutumia dawa za kuua bakteria na viowevu vingi vya IV (moja kwa moja kwenye mishipa yako)
Nini kinachosababisha sepsisi?
Sepsisi kwa kawaida inasababishwa na maambukizi ya bakteria. Maambukizi yanaweza kuanzia sehemu yoyote ya mwili wako, ikiwa ni pamoja na:
Mapafu
Kibofu cha mkojo au figo
Tumbo
Ngozi
Wakati mwingine bakteria wanaingia kupitia kathita ya IV iliyotumika kutoa viowevu na dawa.
Ikiwa maambukizi yataenea kwenye mtiririko wa damu na kusababisha mwili wako kutoa mjibizo, una sepsisi.
Bakteria hatari sana ambao wanasababisha sepsisi kwa kawaida wanapatikana hospitalini.
Dalili za sepsisi na mshtuko wa sepsisi ni zipi?
Sepsisi
Kwa kawaida sepsisi husababisha halijoto kuwa juu. Huenda pia:
Kutetemeka, mzizimo, na udhaifu
Mapigo ya moyo ya haraka
Kupumua haraka
Huenda pia ukawa na dalili za maambukizi yaliyosababisha sepsisi yako. Kwa mfano, ikiwa una maambukizi ya mapafu, unaweza kukohoa na kupumua kwa shida.
Septic shock
Ikiwa una septic shock, una shinikizo la damu la chini ambalo halipungui kwa kupewa matibabu. Huenda pia:
Mkanganyiko na udhaifu
Ngozi ambayo kuwa moto ukiigusa
Mapigo ya moyo ya haraka ya kudunda
Kupumua kwa haraka au kupumua kwa shida
Mkojo kidogo
Baadhi ya watu wenye septic shock watakufa kwa sababu yake.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina sepsisi?
Mwanzoni, inaweza kuwa vigumu kugundua sepsisi. Madaktari wanaweza kujua una sepsisi kulingana na dalili zako na kwa kufanya vipimo vya damu kuangalia bakteria. Watafanya pia vipimo vya damu ili kuangalia jinsi ogani zako zinavyofanya kazi. Haiko dhahiri maambukizi yanatoka wapi, wanaweza pia kufanya vipimo vya picha:
MRI (picha inayoonyesha sehemu ya ndani ya mwili wako)
Madaktari wanatibu vipi sepsisi?
Madaktari wanatibu sepsisi hospitalini kwa kutumia dawa za kuua bakteria moja kwa moja na viowevu vinatolewa kupitia mishipa (IV). Ikiwa una Septic shock, madaktari wanaweza pia:
Kukupa dawa ili kupandisha shinikizo lako la damu.
Kukupatia oksijeni ili kukusaidia upumue au hata kukuweka kwenye mashine ya kupumulia
Kukuweka kwenye mashine ya kusafisha damu
Kuondoa chochote kinachosababisha maambukizi, kama vile mrija wa IV ulioambukizwa
Kufanya upasuaji ili kuondoa usaha au kuondoa tishu zilizoambukizwa
Ikiwa una sepsisi, uwezekano wa kupata nafuu na kuepuka sepsisi mbaya na mshtuko wa sepsisi ni mkubwa ikiwa utapata matibabu mapema. Madaktari wanafuata taratibu za kina ili kutoa matibabu sahihi haraka kadiri iwezekanavyo.