Mfumo wako wa usagaji chakula hugawanya chakula kuwa virutubishi tofauti ambavyo hutumika mwilini.

Njia ya mmeng'enyo wa chakula (pia inaitwa njia ya utumbo na tumbo au GI) ni mrija mtupu ambao chakula hupitia unapokimeza, hukimeng'enywa, na kisha uchafu kutolewa kama kinyesi.

Je, tumbo ni nini?

Tumbo lako ni sehemu ya njia ya mmeng'enyo wa chakula. Tumbo ni kiungo kikubwa, chenye uwazi ambacho kina kuta za zenye misuli. Chakula na vimiminiko ambavyo humeza huena kwenye tumbo lako kutoka kwa umio yako.

Utando wa seli za tumbo lako huachia:

  • Ute

  • Asidi ya tumboni

  • Kimeng'enya cha kusaga chakula kinachoitwa pepsini

Ute hulinda tumbo lako dhidi ya asidi ya tumboni. Dawa fulani (kama aspirini) na baadhi ya vijidudu vinaweza kufanya ute uache kufanya kazi yake na kusababisha vidonda vya tumbo.

Asidi ya tumboni ni asidi ya haidrokloriki. Asidi husaidia kuvunja vunjachakula.

Kimeng'enya cha pepsini huvunja protini, kama vile protini zinazopatikana kweye nyama.

Misuli ya tumboni mwako hukaza na kulegea ili kuchanganya chakula na asidi na vimeng'enya (juisi za tumbo). Uchanganyaji huu na juisi za tumbo huvunja vunja chakula hadi kuwa kimiminiko ambacho mwili wako unaweza kunyonya. Misuli pia husaidia kutoa chakula kwenye tumbo hadi kwenye utumbo mdogo.

Kufikia Tumbo