Mfumo wako wa usagaji chakula hugawanya chakula kuwa virutubishi tofauti ambavyo hutumika mwilini. Hujumuisha njia ya mmeng'enyo wa chakula pamoja na ogani ambazo ziko nje ya njia ya mmeng'enyo wa chakula lakini zenye kusaidia umeng'enyaji wa chakula.

Njia ya mmeng'enyo wa chakula (pia inaitwa njia ya utumbo na tumbo au GI) ni mrija mtupu ambao chakula hupitia unapokimeza, hukimeng'enywa, na kisha uchafu kutolewa kama kinyesi.

Je, kongosho ni nini?

Kongosho lako ni kiungo cha mfumo wa usagaji wa chakula. Ipo nyuma ya tumbo na huunganika na utumbo mdogo kupitia mpira mdogo, wenye uwazi unaoitwa mfereji wa kongosho.

Kongosho ina kazi mbili za msingi.

  • Kuunda juisi za usagaji wa chakula

  • Kuunda homoni

Juisi za usagaji wa chakula hutiririka kupitia mfereji wa kongosho hadi kwenye utumbo mdogo. Juisi husaidia kuvunja vunja chakula na kuzimua asidi ya tumboni.

Kongosho yako huachia homoni moja kwa moja katika mtiririko wa damu. Homoni ni kemikali zinazochochea seli au tishu nyingine kufanya kazi. Insulini ni homoni muhimu inayotengenezwa na kongosho yako. Insulini hudhibiti namna mwili wako unavyoshughulika na sukari (glukosi). Pasipo uwepo wa insulini ya kutosha, utapata kisukari.

Kutambua Kongosho Ilipo