Utumbo Mpana

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Mfumo wako wa usagaji chakula hugawanya chakula kuwa virutubishi tofauti ambavyo hutumika mwilini.

Njia ya mmeng'enyo wa chakula (pia inaitwa njia ya utumbo na tumbo au GI) ni mrija mtupu ambao chakula hupitia unapokimeza, hukimeng'enywa, na kisha uchafu kutolewa kama kinyesi.

Je, utumbo mpana ni nini?

Utumbo mpana, ambao pia huitwa utumbo mkubwa au koloni, ni sehemu ya njia ya mmeng'enyo wa chakula. Huunganisha utumbo wako mdogo na rektamu yako. Kidole tumbo chako ni kibomba mfano wa kidole kilichounganishwa na sehemu ya utumbo mpana. Kidole tumbo kinaweza kupata maambukizi na kusababisha ugonjwa wa kidole tumbo/kibole.

Chakula kilichosagwa huwa katika hali ya kimiminiko kinapofika kwenye utumbo mpana. Kazi ya msingi ya utumbo mpana ni kunyonya kiasi kikubwa cha maji hayo na kuunda kinyesi kigumu.

Kiasi kikubwa cha bakteria huishi kwenye utumbo mpana. Bakteria hizi ni muhimu na husaidia. Hutengeneza dutu fulani muhimu, kama vile vitamini K. Pia bakteria walio kwenye utumbo wako mpana wanaweza kuunda gesi. Hata hivyo, bakteria wengine ambao wanaweza kuingia kwenye utumbo wako mpana wanaweza kukufanya uumwe kwa gastroenteraitisi.

Kutambua Utumbo Mpana